Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akizungumza na Waandishi wa Habari wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu programu Jumuishi ya malezi, makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto, leo tarehe 10 Disemba, 2021 Jijini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii
Mwajuma Magwiza akielezea umuhimu wa vyombo ya habari katika kutekeleza
programu Jumuishi ya malezi, makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto
katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wandishi wa Habari leo tarehe 10
Disemba, 2021 Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa umoja wa Vyama vya Waandishi wa
Habari nchini (UTPC) Abubakar Karsan akielezea kazi iliyofanywa na
Waandishi wa Habari wa masuala ya watoto waliojengewa uwezo, wakati wa
ufunguzi wa mafunzo Kwa Waandishi hao kuhusu programu Jumuishi ya
malezi, makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto Jijini Dodoma leo tarehe
10 Disemba, 2021.Waandishi wa Habari wanaopata mafunzo ya kuwajengea
uwezo kuhusu programu Jumuishi ya malezi, makuzi na Maendeleo ya awali
ya mtoto wakifuatilia matukio hotuba ya ufunguzi kutoka Kwa mgeni Rasmi
Mhe. Mwanaidi Ali Khamis leo tarehe 10 Disemba, 2021 Jijini Dodoma.
Na Mwandishi wetu, Dodoma
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.
Mwanaidi Ali Khamis amesema zaidi ya watoto milioni 2.6 wa chini ya
miaka mitano wamedumaa na zaidi ya watoto 270 wa umri huo hupoteza maisha kila mwaka kutokana na lishe duni.
Akifungua
mafunzo ya kuwajengea uwezo Waandishi wa habari kuhusu programu
Jumuishi ya malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto leo tarehe 10
Desemba, Jijini Dodoma Mhe. Mwanaidi amesema Mikoa inayongoza kwa
upatikanaji wa chakula ndiyo ina changamoto hiyo ya lishe.
"Tanzania
ni moja kati ya nchi za Afrika yenye idadi kubwa ya ya watoto wenye
utapiamlo. Idadi kuwa ya watoto hao ni katika mikoa ya Dar es salaam,
Kagera, Kigoma, Mara, Dodoma, Geita, Tanga, Ruvuma, Mbeya, Morogoro na
Tabora,tukumbuke baadhi ya mikoa hii ina kiwango cha juu cha upatikanaji
wa chakula, programu hii inalenga kuchangia katika kumaliza changamoto
ya lishe kwa watoto wetu nchini" amesema Mhe. Mwanaidi.
Amesema
hivi sasa malezi na makuzi ya watoto hususani wa chini ya miaka 8
yanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukatili, unyanyasaji,
lishe duni na wazazi na walezi kufuatilia mienendo na usalama wa watoto.
Ameongeza
kuwa, Serikali na Wadau mbalimbali wanaendelea na juhudi za kuhakikisha
watoto wote wanakuwa na usawa katika malezi na makuzi ikiwemo
kuvisimamia vituo 5274 vya malezi ya watoto, aidha, vituo
1481
vimeanzishwa na mwaka 2021 Serikali imejenga vituo 20 Mkoani Dodoma na
vituo 10 Dar Es Salaam 10 vimeandaliwa kuwawezesha watoto chini ya miaka
5 kupata malezi na uchangamshi wa awali.
Ameongeza
pia vitendo vya ukatili kwa watoto vinarudisha nyuma jitihada za
Serikali na Wadau kuhakikisha watoto wanakua katika utimilifu wao
akitaja kwa miezi 9 kumekuwa na matukio zaidi ya 6009 hivyo Waandishi
wana nafasi kubwa kushirikiana na Mamlaka nyingine kuelimisha jamii ili
iweze kubadilika.
Kwa
upande wake, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya
Jamii Mwajuma Magwiza amesema Waandishi wa Habari ni kundi muhimu sana
katika kupeleka taarifa kwa Jamii ikiwa wataelimishwa kwani wao pia ni
sehemu ya utekelezaji.
"Tunaamini
kundi hili likipata uelewa sahihi wakati huu, hata kwenye utekelezaji
inakuwa kazi rahisi, Programu hii itazinduliwa tarehe 13 mwezi huu na
kawaida ya Wizara huwa tunaanza kujenga uwezo kwa makundi muhimu ambayo
yanatakiwa kupelekwa taarifa sahihi"Alisema
Naye
mmoja wa Waandishi hao Jaliwasom Jasson ameshukuru kwa kupata elimu na
kujengewa uwezo wakati wote wa utekelezaji wa masuala ya watoto na
kuahidi kuendelea kufanya vema zaidi katika programu hiyo ya malezi na
makuzi kwa kiwango na matokeo makubwa kwa kushirikiana na Serikali.
"Tunapokwenda
kuitekeleza programu hii tunaomba tushirikishwe katika mikoa yote
tukitumika vizuri nina uhakika elimu hii itawafikia Jamii na kuwekeza
vizuri kwa watoto wetu"
MWISHO