Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Staricko Meshack akizungumza na Wanajumuia wa Chuo Kikuu Iringa wakati msafara wa kuadhimisha siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia ukiwa chuoni hapo.
Wanajumuiya wa Chuo Kikuu Iringa wakichangia mawazo kuhusu ukatili wa kijinsia wakati msafara wa kupinga Ukatili wa Kijinsia ulipopita chuoni hapo katika kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili huo.
Baadhi ya wananchi na wanachuo wa Chuo Kikuu Iringa wakifuatilia mjadala na matukio mbalimbali wakati msafara wa kupinga Ukatili wa Kijinsia ulipopita chuoni hapo katika kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili huo.
Na Witness Masalu, Iringa.
Wakati
Tanzania ikiwa ndani ya kipindi cha maadhimisho ya Siku 16 za kupinga
ukatili wa kijinsia, imebainika kuwa asilimia 33 ya wanavyuo nchini
wamekumbana na ukatili wa kijinsia.
Hayo
yamebainika katika msafara wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia
unaoendelea ukishirikisha watumishi wa sekta mbalimbali Serikalini na
wadau wa Maendeleo .
Akizungumza katika msafara huo kwenye Chuo Kikuu cha Iringa
Dkt.
Othman Ahmed kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, amesema
idadi ya wanavyuo wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ni kubwa
hali ambayo haiwezi kuvumiliwa.
Amesema katika kila wanavyuo watatu, mmoja kati yao ni mhanga wa vitendo vya ukatili.
“Kati
ya kundi la watu watatu, mmoja wao ni mhanga wa ukatili wa kijinsia,
hivyo jamii iendelee kukemea vikali vitendo vyote vya unyanyasaji
kijinsia” alisema
Kwa
upande wake, Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo
ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Staricko Meshack amesema Serikali imetoa
mwongozo unaoelekeza vitu vya msingi vinavyotakiwa kutekelezwa endapo
mtu anafanyiwa ukatili wa kijinsia ikiwemo kuanzishwa kwa madawati ya
jinsia Vyuoni”
Naye Dennis Lekayo kutoka Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU amewaonya
Wanafunzi
wanaotumia wenzao kama chambo dhidi ya walimu wao kwa lengo la kuripoti
taarifa za rushwa na hivyo, kufikishwa TAKUKURU.
”Kumekuwa
na tabia ya wanavyuo kutafuta wanafunzi ambao wanatumika kama chambo
kuwakamata kuwatega walimu wenye misimamo mikali ili wakamatwe na
waondolewe Vyuoni,hii si nzuri” alisema
Happy
Kimaro kutoka Jeshi la Polisi, Arusha, amesema Madawati ya jinsia
yalioanzishwa yanatakiwa kutumika ipasavyo kwani madawati hayo yanafanya
kazi kwa kuzingatia usiri.
Novemba
25, mwaka huu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alizindua Kampeni ya
maadhimisho ya Siku 16 za kupinga Ukatili na kuelekeza kuazishwa kwa
madawati ya Jinsia katika vyuo vya Kati na vyuo Vikuu sambamba na
kuanzishwa kwa madawati hayo katika shule za Msingi na Sekondari ikiwa
ni njia mujarabu ya kukabiliana na ukatitili nchini.
Mwisho
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464