Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akiwa ameshikilia Kombe la ushindi kwa Stand United baada ya kutwaa Ubingwa wa Michuano ya Gold fm Champions League daraja la tatu mkoa wa Shinyanga baada ya kuifunga bao 1 kwa 0 timu ya Isabilo FC
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Stand United FC imetwaa Ubingwa wa Michuano ya Gold fm Champions League daraja la tatu mkoa wa Shinyanga baada ya kuifunga bao 1 kwa 0 timu ya Isabilo FC kutoka halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama.
Stand United FC imetwaa ubingwa huo leo Ijumaa Desemba 17,2021 mbele ya Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema huku ikikabidhiwa Kombe na zawadi ya shilingi milioni tatu wakati washindi wa pili Isabilo FC wakiondoka na kitita cha shilingi milioni moja.
Kufuatia ushindi huo sasa Stand United itauwakilisha mkoa wa Shinyanga katika mashindano ya Mabingwa wa mikoa mbalimbali ili kumpata bingwa atakayefanikiwa kwenda kucheza Ligi Daraja la Pili.
Mchezo kati ya Isabilo FC na Stand United ulivuta hisia za maelfu ya mashabiki wa soka mkoa wa Shinyanga wakati vuta nikuvute zikiendelea katika kinyang'anyiro hicho ambapo katika kipindi cha kwanza hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake hadi kipindi cha pili dakika ya 75 mchezaji wa Stand United Jacob Nyoapu alipoipatia goli timu yake.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary ameipongeza Stand United kwa ushindi huo huku akiushukuru uongozi wa Gold Fm kwa kudhamini mashindano hayo ikiwa ni sehemu ya kuthamini na kujali michezo mkoani Shinyanga.
"Tunawashukuru sana Gold Fm kwa kudhamini mashindano haya, kitendo cha kudhamini michezo inaonesha ni kwa kiasi gani mnathamini michezo. Namuomba mwenyezi Mungu aibariki Gold Fm, iendelee Ku Shine! (Kung'ara) chini ya uongozi wa mwanamke shupavu Mkurugenzi Neema Mghen", amesema Omary ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo mkoa wa Shinyanga.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA), Said Mankiligo ameishukuru Gold Fm kwa kutoa zaidi ya shilingi Milioni 36 kudhamini Ligi hiyo illiyofanyika kwa muda wa siku 95 huku akiahidi kuweka nyasi za bandia katika uwanja wa taifa Kahama.
Mkurugenzi wa Gold Fm, Neema Mghen amesema wamedhamini mashindano kupitia kipindi chao cha michezo 'Sports Planet' kwani wanajali michezo huku akiwashukuru wananchi kuyapokea mashindano hayo ya Gold Fm Champions League.
"Mshindi Stand United Fc tunampatia Kombe na zawadi ya shilingi milioni tatu na mshindi wa pili Isabilo Fc anapata zawadi ya shilingi milioni 1. Lakini pia tumetoa medali mbalimbali kwa wachezaji, magolikipa,makocha,waamuzi,timu na vikundi vya hamasa", amesema Mghen.
Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akikabidhi Kombe la ushindi kwa Kapteini wa Stand United, Boniphace Juma baada ya kutwaa Ubingwa wa Michuano ya Gold fm Champions League daraja la tatu mkoa wa Shinyanga baada ya kuifunga bao 1 kwa 0 timu ya Isabilo FC
Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akikabidhi fedha shilingi Milioni 3 kwa Stand United baada ya kutwaa Ubingwa wa Michuano ya Gold fm Champions League daraja la tatu mkoa wa Shinyanga baada ya kuifunga bao 1 kwa 0 timu ya Isabilo FC
Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akizungumza baada ya Stand United kutwaa Ubingwa wa Michuano ya Gold fm Champions League daraja la tatu mkoa wa Shinyanga baada ya kuifunga bao 1 kwa 0 timu ya Isabilo FC

Mkurugenzi wa Gold Fm, Neema Mghen akizungumza baada ya Stand United kutwaa Ubingwa wa Michuano ya Gold fm Champions League daraja la tatu mkoa wa Shinyanga baada ya kuifunga bao 1 kwa 0 timu ya Isabilo FC

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA), Said Mankiligo akizungumza baada ya Stand United kutwaa Ubingwa wa Michuano ya Gold fm Champions League daraja la tatu mkoa wa Shinyanga baada ya kuifunga bao 1 kwa 0 timu ya Isabilo FC
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akizungumza baada ya Stand United kutwaa Ubingwa wa Michuano ya Gold fm Champions League daraja la tatu mkoa wa Shinyanga baada ya kuifunga bao 1 kwa 0 timu ya Isabilo FC
Wachezaji wa Stand United wakipiga picha ya pamoja baada ya kutwaa Ubingwa wa Michuano ya Gold fm Champions League daraja la tatu mkoa wa Shinyanga baada ya kuifunga bao 1 kwa 0 timu ya Isabilo FC
Wachezaji wa Stand United wakipiga picha ya pamoja baada ya kutwaa Ubingwa wa Michuano ya Gold fm Champions League daraja la tatu mkoa wa Shinyanga baada ya kuifunga bao 1 kwa 0 timu ya Isabilo FC
Wachezaji wa Stand United wakifurahia baada ya kutwaa Ubingwa wa Michuano ya Gold fm Champions League daraja la tatu mkoa wa Shinyanga baada ya kuifunga bao 1 kwa 0 timu ya Isabilo FC
Wachezaji wa Stand United wakifurahia baada ya kutwaa Ubingwa wa Michuano ya Gold fm Champions League daraja la tatu mkoa wa Shinyanga baada ya kuifunga bao 1 kwa 0 timu ya Isabilo FC
Kikosi cha Isabilo Fc
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando akisalimiana wa wachezaji wa timu ya Isabilo FC
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando akisalimiana waamuzi mchezo wa Isabilo FC vs Stand United
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando akizungumza na wachezaji kabla ya mechi
Mashabiki wa Soka wakifuatilia mtanange kati ya Isabilo fc na Stand United Fc.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog