Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga yatoa onyo kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri
Na Chibura Makorongo,
Shinyanga WAMILIKI wa vyombo vya usafiri mkoa wa Shinyanga na mikoa jirani wametahadharishwa kuwa chombo chochote kitakacho kamatwa na muhamiaji haramu kita taifishwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa Idara ya uhamiaji mkoani hapa Rashidi Mageta alipokuwa akiongea Shinyanga press club blog tarehe 23,Desemba 2021 ofisini kwake katika salamu za sikukuu za krismasi na mwaka mpya alisema idara yake inakuja ki mkakati zaidi baada ya kugundua kuna biashara haramu inafanyika.
Alisema kuwa tumegundua kuwa kuna baadhi ya magari ya abiria husafirisha wahamiaji haramu toka nchi jirani kuleta kahama , kuna majenti wao wapo na majina yao tunayo hivyo usafiri wowote utakao bainika kufanya hivyo watataifisha gari hilo,watumishi watakao kuwemo humo wata shitakiwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
Idara ya uhamiaji kuanzia sasa halitakuwa na huruma baada ya kutoa semina ya mwaka mmoja juu ya uelewa wa sheria za uhamiaji na madhara ya kuachia watu wasio fahamika wanakotoka na sifa zao,yeyote atakaye bainika mahakamani tu’
‘Sheria ya Uhamiaji N0 6 ya mwaka 1995 inayotoa adhabu kali kwa watu wanao safirisha raia wa kigeni nchini wasio kuwa na vibali, wamiliki wa vyombo hivyo sasa wakae tayari kama hawata waonya watumishi wao kutojiusisha na vitendo hivyo’ alisema Mageta.
Alizitaja njia na maeneo wanayo pitia kuwa ni Benaco mkoani Kagera kwa raia toka Rwanda kupitia Runzewe,Ushirombo, Kahama na Kwenda Kagongwa ,Itobo Nzega , na nyingine maeneo ya Isaka,Tinde mpaka Nzega pia njia kuu zinazo ingilia mkoa wetu za Kishapu,Maganzo ,Korandoto Shinyanga mjini.
Aidha mkuu huyo wa idara hiyo aliwapongeza wananchi wote na viongozi na watendaji wa vijiji na mitaa kwa ushirikiano walio utoa kwa idara hiyo baada ya semina zilizo kuwa zikitolewa kwa kuweza kufanikisha maswala ya utoaji wa taarifa hizo za wahamiaji haramu katika mkoa wetu.
Na kamanda huyo alisema kwa muda furani vijana wetu baadhi yao waliokuwa chuoni likizo kwao hazita kuwepo wamerudi mipaka yote ya mkoa njia zote za usafiri na ukaguzi wa kushitukiza ndani ya magari yote ya mizigo na abiria na watakuwepo usiku na mchana, mkoa wetu sio maficho wala njia ya kupitishia watu hao.
Idara inatoa wito kwa wananchi wote kuendelea kushirikiana na si kwa kutoa taarifa yeyote kwenye maeneo yao pindi wanapo mtilia shaka mtu yeyote hatua stahiki zitafuata mara moja AMANI YA NCHI YETU NI JUKUMU LA KILA MTANZANIA hiyo ni kaulimbiyu ya idara Shinyanga.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464