JESHI LA POLISI LIMEWAASA MADAKTARI NA WATAALAM WENGINE KUTOA USHAHIDI KWA KESI ZA UKATILI WA KIJINSIA.

 

 

 

 

Wadau wa ukatili kutoka taasisi mbalimbali mkoa wa Shinyanga walioshiri kikao cha thathimini dhidi ya vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto kilichoendeshwa na jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga.

 Mwandishi wetu.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limewaasa madaktari na wataalam mbalimbali kutoka ndani ya serikali na sekta binfasi kutoa ushirikiano kwa kitengo cha Upepelezi wa Sayansi ya Jinai kwa matukio ya ukatili wa jinsia dhidi ya ubakaji, ulawiti, mauaji, vipigo, wizi wa watoto na lugha chafu mitandaoni ili kuweza kutoa ushahidi na vielelezo ili kutokwamisha ucheweshaji wa hukumu za kesi zote za ukatili wa kijinsia zilizofunguliwa mashauri kwa vyombo vya Mahakama.

Hayo yameelezwa leo Januari 26,2022 na Ally Ngosha Omary, Mkuu wa Upepelezi wilaya ya Shinyanga, katika Kikao cha Tathimini dhidi ya Vitendo vya Ukatili kwa wanawake na watoto kilichofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa ufadhili wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (Women Fund Tanzania -Trust) ambapo Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ni mdau anaye tekeleza Mradi wa kutokomeza ukatili katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa kupatiwa ruzuku ya Shs. Milioni 8.

Ally Ngosha alisema wataalam mbalimbali kutoka serikali na sekta binafsi ni vema kuwa tayari kutoa ushahidi na vielezo kwa kitengo cha upepelezi ili kuweza kusaidia kesi dhidi za wanawake na watoto kwenda vizuri na kuacha kuwa na hofu ya kuelezea ushahidi wao juu ya jambo ambalo wanalifahamu kwa kina.

Aidha, Ngosha alijaribu kuonesha moja ya kikwazo alichokutana nacho kwa mtumishi wa serikali ambaye ni afisa kilimo aliyekata kuthibitisha kitaalam juu ya uwepo wa mmea wa bangi katika shamba la mtuhumiwa aliyekuwa chini ya jeshi la polisi.

Ngosha alisema, madaktari ni watu muhimu sana dhidi ya kesi za ukatili ni wajibu wao kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi bila kuweka vikwazo ili kusaidia uchunguzi wa matukio ya ukatili wa jinsia dhidi ya wanawake na watoto kwa kuwa yatari kutoa maelezo ya kitaalam mahakamani pindi wanapohitajika kama sehemu ya ushahidi.

“Kesi za ukatili wa kijinsia zina mlolongo mrefu sana zinahitajika sampuli mbalimbali za vielelezo vya kitaalam hasa kwa matukio ya ubakaji na mauaji dhidi ya wanawake na watoto” Alisema Ally Ngosha.

Kwa upande mwingine, Juma Sadiki Bahati, Mkuu wa Sayansi Jinai Mkoa wa Shinyanga ,alisistiza kuwa fomu ya PF3 ya jeshi la polisi kwa asilimia 90 inahitaji maelezo ya taarifa za daktari ili kusaidia ushahidi, Changamoto kubwa ni madaktari wengi wanaogopa kutoa ushahidi mahakamani na hivyo kutoi jaza fomu ya PF3 kikamilifu.

Naye Mwanasheria ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkoa wa Shinyanga, Immaculata Mapunda alisitiza kuwa Mahakama zinahitaji sampuli mbalimbali za kitaalam ili kusaidia utoaji wa haki kwa vyombo vya Mahakama.

 

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464