JESHI LIMETANGAZA KUPINDUA NCHI

Jeshi nchini Burkina Fasso linasema kwamba limechukua mamlaka na kumuondoa madarakani rais Roch Kabore.

Tangazo hilo lilitolewa katika runinga ya taifa na afisa mmoja wa jeshi , ambaye alisema kwamba aserikali na bunge limevunjwa.

Kufikia sasa haijulikani bwana Kabore yuko wapi , lakini afisa huyo amesema kwamba wale wote wanaozuiliwa wapo katika eneo salama.

Mapinduzi hayo yanajiri siku moja tu baada ya wanajeshi hao kudhibiti kambi za jeshi huku milio ya risasi ikisika katika mji mkuu wa Ouagadougou..

Mapema , Chama tawala cha peoples Movement PMP kilisema kwamba wote Kabore na waziri mmoja wa serikali walinusurika jaribio la mauaji.

Siku ya Jumapili, wanajeshi waasi walitaka kufutwa kazi kwa maafisa wa jeshi na kuongezwa kwa raslimali za kukabiliana na wapiganaji wa Kiislamu.

Taarifa hiyo ilitolewa na kundi ambalo halijasikika hapo awali, Vuguvugu la Patriotic for Safeguard and Restoration au MPSR, kifupi chake cha Kifaransa.


SOMA ZAIDI HAPA ;CHANZO BBC SWAHILI



Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464