Picha ya jengo la hospitali ya magonjwa ya mlipuko lililojengwa eneo la Negezi kata ya Mwawaza manispaa ya Shinyanga.
Wajumbe wa Kamati ya siasi mkoa wa Shinyanga wakiwa picha ya pamoja baada ya ukaguzi wa ujenzi wa hosptali ya magonjwa ya mlipuko.
Wajumbe Wa Kamati Ya Siasa CCM Mkoa Wa Shinyanga wakitembelea kuona vyumba Vya madarasa na ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Lubaga.
Na Kareny Masasy
WAJUMBE wa kamati ya siasa ya chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga wmekagua ujenzi wa hospitali ya magonjwa ya mlipuko inayojengwa eneo la Negezi kata ya Mwawaza manispaa ya Shinyanga nakurizishwa na kasi ya ujenzi huo.
Kamati hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho mkoa Mabala Mlolwa jana walikagua miradi mbalimbali iliyopo manispaa ya Shinyanga ikiwemo ujenzi wa hospitali hiyo iliyogharimu kiasi cha zaidi ya sh Billioni moja na kukamilisha jengo.
Mlolwa amesema kuwa mradi huo umewafurahisha kwa kujengwa kwa kiwango majengo yake na kuwataka viongozi wa mkoa kuutangaza ili wananchi waweze kuelewa vizuri kweli Rais Samia Suluhu amefanya kazi kubwa anastahili kupongezwa.
“Kumekuwa na maneno kwa baadhi ya watu kuwa hatujafanya kitu leo nimejionea na kamati yangu majengo kama haya kwa mkoa wetu tulikuwa tunayaona mikoa mingine hospitali hii itasaidia kokoa maisha ya watu wengi ambao walikuwa wakipatwa na magonjwa walikuwa wakikimbilia mkoani Mwanza au Dar-es-salaam kutibiwa.” Alisema Mlolwa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jansita Mboneko katika ziara hiyo amesema kuwa mtu alivyokuwa akipatwa na magonjwa ya mlipuko mfano maambukizi ya Covid -19 ilikuwa ni changamoto kubwa alilazimika kuwekewa mitungi minane hadi kumi ya kupumulia ili kuokoa maisha lakini sasa matibabu yatapatikana hapahapa wilayani.
Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga Dkt Augostino Maufi akisoma taarifa mbele ya kamati hiyo ameeleza kuwa ujenzi huo mkataba wake ulianza rasmi mwaka jana mwezi Agosti nakutakiwa kukamilika kipindi cha miezi sita na kiasi cha zaidi ya sh Billioni moja fedha kutoka kwa wafadhili wa Global Fund na serikali zikitumika.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464