Kamayti ya siasa ikijadiliana baada ya ukaguzi wa ujenzi wa maabara katika shule ya Mwadau sekondari.
Na Kareny Masasy
KAMATI ya siasa ya chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga imerizishwa na baadhi ya miradi ya sekta ya elimu na afya inayotekelezwa kwa fedha za uviko -19 wilayani Kishapu.
kamati hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) Mabala Mlolwa na walifanya ziara jana ya kukagua ujenzi wa majengo ya wagonjwa wa n je OPD,Maabara na kichomea taka katika kituo cha afya kilichopo kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge kilichofikia asilimia 51 katika ujenzi wake,
"Ni suala la kumpongeza Rais Samia Suluhu sababu amehangaika kuzitafuta fedha ili kuhakikisha wanafunzi hawakai kwenye mrundikano tena wala chini na madarasa kuibuka kama uyoga kweli ametekeleza ilani ya chama kwa vitendo katika sekta ya elimu"amesema Mlolwa..
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude amesema kuwa shule ya sekondari zipo 32 ambapo walipokea kiasi cha sh Billioni moja kwaajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 97 ikiwa vyumba 81 vya shule ya sekondari na madarasa 16 kwenye shule shikizi na ujenzi umekamilika kwa asilimia 96.
Mkunde amesema kuwa kila siku wanapiga hatua katika kutekeleza miradi mbalimbali na pamoja na madawati yote na ofisi za walimu ambapo walitarajia kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza jumla ya wanafunzi 4456.
Mkuu wa shule ya sekondari Shinyanga (shybush) Bernard Ishengoma alisema kuwa walipewa kiasi cha sh Millioni 40 katika shule hiyo nakuweza kujenga vyumba vya madarasa mawili na madawati 80 kila darasa na ofisi moja jumla kunakuwa na vyumba vya madarasa 23.
Mkuu wa shule ya sekondari Kishapu Kaji Kapyen amesema kuwa vyumba vya madarasa vimekamilika vyote na wanafunzi 195 walipangiwa shule hiyo kutokana na takwimu hiyo na kuwepo madawati na vyumba vya madarasa hakuna mrundikano wa wanafunzi hata wakiripoti wote.