Mwonekano wa jengo la ujenzi la kituo cha afya Salawe katika ziara ya Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Alhamisi 27,januari,2022.
Na Kareny Masasy.
Kamati
ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Shinyanga haijaridhishwa na
kasi ya ujenzi wa majengo ya upasuaji,mochwari na wodi ya mama na mtoto
kituo cha afya Salawe katika Halmashuri ya wilaya ya Shinyanga licha ya serikali kutoa kiasi cha fedha Shs milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya.
Hayo yamelezwa,Janauri 27,2022 wakati ziara ya Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi ya Mkoa wa Shinyanga,ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Bw,Mabala Mlolwa.Kamati hiyo ilieleza kuwa hajaridhishwa na hatua za ujenzi wa kituo hicho kulingana na maeneo mengine kuwa yamekwisha kamilisha ujenzi wa vituo vya afya.
Kamati ya Siasa ya CCM ilieleza kuwa hali ya ucheleweshaji wa ujenzi wa kituo cha afya cha Salawe unatokana na kamati ya afya ya kituo hicho kukwamisha juhudi za haraka za ujenzi huo kwa ajili ya manufaa ya wananachi wa kata ya Salawe.
Kamati hiyo ya CCM ilitoa maagizo kwa kamati ya afya kuchukua hatua za haraka za ukamilishaji wa ujenzi wa kituo cha afya salawe kwa ajili ya kutoa huduma za afya kwa wakazi wa salawe.
Aidha,Mary Shausi ambaye ni Mtendaji wa kata ya Salawe akitoa taarifa mbele
ya wajumbe wa kamati hiyo amesema kuwa walipokea kiasi cha fedha
kwa ajili ya mradi huo ila wanatarajia kukamilisha ifikapo mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu.