Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Sophia Mjema akikabidhi pikipiki kwa maofisa wa mifugo kutoka halmashauri nne za Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa shughuli zao.
Maaofisa Mifugo kutoka Halmashauri nne za Mkoa wa Shinyanga wakiwa wakipokea pikipiki kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Na Kareny Masasy
MKUU wa mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema amekabidhi pikipiki 12 kwa maafisa mifugo wa halmashauri nne lengo kuwarahisishia kufika kwenye maeneo ya wafugaji walio pembezoni nakujua changamoto zinazo wakabili na sio kwenda kuzibebea abiria nakufanya biashara.
Kila halmashauri itapata pikipiki tatu ambazo ni Kishapu,Msalala,Ushetu na Shinyanga vijijini.
Mjema amesema hayo jana wakati akikabidhi pikipiki hizo kwa maafisa mifugo hao huku akieleza kuwa serikali imeliona suala la changamoto na haitaki kusikia malalamiko kutoka kwa wafugaji kuwa hawajatembelewa wakati usafiri wamepata.
“Ni suala la kumpongeza Rais wetu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kutukumbuka na kutuondolea changamoto moja kwa nyingine nasi tunasema hatuta muangusha katika utekelezaji wa kuwatumikia wananchi kwani pikipiki hizi zifanye kazi yake iliyokusudiwa sio kuzifanya bodaboda”.amesema Mjema.
Ofisa mifugo mkoa wa Shinyanga Dioniz Gutav amesema kuwa pikipiki 12 zilizotolewa ni matumaini watawafikia wafugaji kwenye maeneo yao kutoa elimu kwani kuna majosho 39 ambayo wanatakiwa kuyatumia ili kuwaondoa wadudu kupe ambao wamekuwa wakishambulia ngo’mbe.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464