Mwakilishi wa Mfuko wa Ruzuku wa wanawake Tanzania WFT mkoani Shinyanga Glory Mbia, akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto wilayani Shinyanga.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
MRADI wa kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto umezinduliwa kwa awamu ya tatu Rasmi Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Uzinduzi huo umefanyika leo Januari 13.2021 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo, na kuhudhuliwa na Mashirika mbalimbali yasiyo ya kiserikali, dawati la jinsia, watendaji wa Kata, maofisa maendeleo ya jamii, pamoja na vyombo vya habari, mradi ambao umefadhiliwa na Mfuko wa Ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT)-TRUST.
Mwakilishi wa mfuko huo (WFT) mkoani Shinyanga Glory Mbia, akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, amesema wametoa kiasi cha fedha Sh. milioni 170 kwa Mashirika Saba, dawati la jinsia, chama cha Waandishi wa habari mkoani Shinyanga, Radio Faraja, na Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, ambapo kila mmoja amepewa fedha zake na eneo la kwenda kuutekeleza mradi huo.
"Matarajio yetu kwenye utekelezaji wa mradi huu, ni kuleta mabadiliko chanya ndani ya jamii, kupunguza ama kutokomeza kabisa matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto," alisema Mbia.
Naye Mgeni Rasmi Stewart Makali, ambaye ni Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, akimwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, amewataka wadau hao wakazitumie fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa, na kuibadilisha jamii kuachana na matukio ya ukatili.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya maendeleo ya jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Deus Mhoja, alisema hali ya matukio ya ukatili wa kijinsia wilayani humo siyo mbaya, ikilinganishwa na miaka ya nyuma ambapo hali ilikuwa siyo nzuri.
Alitaja matukio ambayo bado yapo ndani ya jamii, kuwa ni ulawiti wa watoto, ubakaji, vipigo, mimba na ndoa za utotoni, ambayo ndiyo wanashirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo kuyatokomeza, yakiwamo mashirika yasiyo ya kiserikali na vyombo vya habari.
Nao waandishi wa habari, ambao ni miongoni mwa wanufaika wa Ruzuku hiyo Sh.milioni 16.7

, wameomba ushirikiano kutoka kwa viongozi wakati wa utekelezaji wa mradi huo, kuanzia ngazi ya Kata na wasiwanyime taarifa wala kutopokea simu.
Mradi huo wa kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto wilayani Shinyanga, utakelezwa na mashirika yafuatayo likiwamo wa Thubutu Afrika Intiatives, WEADO, Rafiki SDO, Yawe, GCI, Agape, Chama Cha waandishi wa habari mkoani Shinyanga, Radio Faraja, dawati la jinsia, pamoja na Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, na utakoma Rasmi June mwaka huu, ambapo mashirika mengine mradi huo utaisha March.
Mradi huo wa kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto wilayani Shinyanga, utakelezwa na mashirika yafuatayo likiwamo wa Thubutu Afrika Intiatives, WEADO, Rafiki SDO, Yawe, GCI, Agape, Chama Cha waandishi wa habari mkoani Shinyanga, Radio Faraja, dawati la jinsia, pamoja na Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, na utakoma Rasmi June mwaka huu, ambapo mashirika mengine mradi huo utaisha March.
Mwakilishi wa Mfuko wa Ruzuku wa wanawake Tanzania WFT mkoani Shinyanga Glory Mbia, akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto wilayani Shinyanga.
Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Stewart Makali, akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo.
Mwakilisha wa RPC Mkoa wa Shinyanga Monica Sehere ambaye ni msimamizi mkuu wa madawati ya jinsia kutoka Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo.
Mkuu wa Idara ya maendeleo ya jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Deus Mhoja, akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo.
Afisa maendeleo ya jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omary, akiwasilisha taarifa ya shughuli za utekelezaji wa mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto wilayani humo kupitia fedha za Ruzuku walizopewa na WFT.
Mkuu wa dawati la jinsia mkoani Shinyanga Analyse Kaika, akiwasilisha taarifa ya shughuli za utekelezaji wa mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto wilayani Shinyanga kupitia fedha za Ruzuku walizopewa na WFT.
Mariamu Maduhu kutoka Shirika la RAFIKI SDO, akiwasilisha taarifa ya shughuli za utekelezaji wa mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto wilayani Shinyanga kupitia fedha za Ruzuku walizopewa na WFT.
Afisa miradi kutoka Shirika la WEADO Salome Shangari, akiwasilisha taarifa ya shughuli za utekelezaji wa mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto wilayani Shinyanga kupitia fedha za Ruzuku walizopewa na WFT.
Mkurugenzi wa Shirika la AGAPE John Myola, akiwasilisha taarifa ya shughuli za utekelezaji wa mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto wilayani Shinyanga kupitia fedha za Ruzuku ambazo watapewa na WFT ikiwa kwa wasasa wapo kwenye mazungumza ya mwisho.
Mratibu wa Chama cha Waandishi wa habari mkoani Shinyanga Estomine Henry, akiwasilisha taarifa ya shughuli za utekelezaji wa mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto wilayani Shinyanga kupitia fedha za Ruzuku walizopewa na WFT.
Mratibu wa vipindi kutoka Radio Faraja Simeo Makoba, akiwasilisha taarifa ya shughuli za utekelezaji wa mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto wilayani Shinyanga kupitia fedha za Ruzuku walizopewa na WFT.
Uwasilishaji wa Taarifa za utekelezaji wa mradi wa kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto wilayani Shinyanga, kupitia fedha za Ruzuku kutoka WFT ukiendelea katika Shirika la GCI
Uwasilishaji wa Taarifa za utekelezaji wa mradi wa kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto wilayani Shinyanga, kupitia fedha za Ruzuku kutoka WFT ukiendelea katika Shirika la YAWE.
Mwenyekiti wa Baraza la watoto Kata ya Iselamagazi Lucy Patric akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo.
Uzinduzi wa mradi wa kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto wilayani Shinyanga ukiendelea.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA.