POLISI DAWATI LA JINSIA WATAKIWA KUTUNZA SIRI MADHULA WA MATUKIO YA UKATILI



Kamishina msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga (ACP)Joseph Paulo, akizungumza kwenye utoaji wa mafunzo kazini kwa Askari ambao ni watendaji wa dawati la jinsia.


Na Marco Maduhu, SHINYANGA


WATENDAJI wa Dawati la Jinsia kutoka Jeshi la Polisi Shinyanga, wametakiwa wawe wasiri wanapokuwa wakihudumia madhula wa matukio ya ukatili wa kijinsia, hasa wale ambao hufanyiwa vitendo vya kingono ikiwamo ubakwaji.

Kamishina msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Joseph Paul, amebainisha hayo leo Januari 24,2022 kwa niaba ya Kamanda wa Jeshi hilo mkoani humo George Kyando, kwenye utoaji wa mafunzo kazini kwa Askari ambao ni watendaji wa dawati la jinsia, wakati akitoa mada ya maadili ya Jeshi la Polisi.

Amesema watendaji wa dawati la jinsia, wanapaswa wawe na usiri mkubwa, sababu wana hudumia watu ambao wamefanyiwa vitendo vibaya ikiwamo ubakwaji, hali ambayo ina hitaji usiri ili kutoendelea kuumiza madhula.

"Madhula wa matukio ya ukatili wanapokuja kutoa taarifa kwenye dawati, wamekuja kupata msaada na wanahitaji kufarijiwa, hivyo mnatakiwa muwe wasiri sana na wenye huruma, na kuwapatia huduma haraka ili wapate haki yao," alisema Paul.

Naye Mrakibu msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Revocatus Msami, alitaja madhara ya kutotunza siri za madhula, kuwa ni dawati kutoaminiwa tena, kuharibu upelelezi, kushamili kwa uharifu, kuleta usaliti, uhasama ndani ya jamii na hata kusababisha mauaji.

Aidha, Mrakibu msaidizi wa Polisi Mkoa upande wa Polis Jamii Monica Sehere, alisema dawati la jinsia jukumu lake jingine kubwa ni kutoa elimu ya ukatili, ili kupunguza matukio hayo ndani ya jamii, pamoja na utoaji wa ushahidi mahakamani.

Kwa upande wake Mrakibu msaidizi wa Polisi Mkuu wa idara ya Sayansi jinai, Juma Bahati, alitoa wito kwa Madhula ambao wamefanyiwa vitendo vya ubakwaji, kuwa wasiwe wanaoga ili kutoharibu ushahidi, bali wafike kwenye dawati wakiwa hivyo hivyo, na kwenda kufanyiwa vipimo vya uchunguzi na kuchukua vinasaba vya mhusika wa tukio hilo.

Mafunzi hayo ya Askari Polisi ambao ni watendaji wa dawati la Jinsia, yamefanyika ikiwa ni maandalizi ya kuanza kutekeleza mradi wa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto wilayani Shinyanga, kwa ufadhili wa mfuko wa ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT).


Kamishina msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Joseph Paulo, akizungumza kwenye utoaji wa mafunzo kazini kwa Askari ambao ni watendaji wa dawati la jinsia na kutoa mada ya maadili ya Jeshi la Polisi.

Mrakibu msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Revocatus Msami, akitoa mada kwenye mafunzo hayo.

Mrakibu msaidizi wa Polisi Mkoa upande wa Polisi Jamii Monica Sehere, akitoa mada juu ya majukumu ya dawati la jinsia.

Mrakibu msaidizi wa Polisi Mkuu wa Idara ya Sayansi Jinai, akitoa mada, jinsi ya kutunza ushahidi wa makosa ya jinai hasa kwa madhula wa matukio ya ubakwaji na mauaji.

Mkaguzi wa Jeshi la Polisi Marco Masunzu, akitoa mada ya sheria ya makosa ya jinai.

Wakili wa Serikali Shani Wampumbulya, akitoa mada ya sheria ya mtoto ya mwaka 2009.

Mratibu wa dawati la jinsia Mkoa wa Shinyanga Analyse Kaika akizunguma kwenye mafunzo hayo.

Mratibu wa dawati la jinsia wilaya Brihgtone Rutajama akizungumza kwenye mafunzo hayo.

Askari wa dawati la jinsia wakiwa kwenye mafunzo.

Mafunzo yakiendelea.

Mafunzo yakiendelea.

Mafunzo yakiendelea.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464