Header Ads Widget

RAIS SAMIA AFANYA MABADILIKO BARAZA LA MAWAZIRI, MAKATIBU WAKUU, KUAPISHWA JANUARI 10 CHAMWINO IKULU DODOMA

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza jipya la Mawaziri na Makatibu wakuu.
 
Akitangaza mabadiliko hayo leo Jumamosi Januari 8, 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga amesema Rais amefanya mabadiliko ya muundo katika wizara tatu.

Rais Samia amefanya mabadiliko hayo ikiwa anatimiza ahadi yake ya kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri.
 
MAWAZIRI WAPYA WATANO NI
 
 Nape Nnauye (Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari), Hamad Masauni (Mambo ya Ndani), Dk Pindi Chana (Sera Bunge na Uratibu), Anjelina Mabula (Ardhi) na Husein Bashe (Kilimo).

Rais Samia pia ameteua manaibu waziri wapya katika wizara tano.

Manaibu waziri hao wapya walioteuliwa ni pamoja na Anthony Mavunde (Kilimo), Jumanne Sagini (Mambo ya Ndani) Dkt.  Lemomo Kiruswa (Madini), Ridhiwani Kikwete (Ardhi) na Atupele Mwakibete (Ujenzi na Uchukuzi).
 






 

Post a Comment

0 Comments