RC MJEMA AENDESHA KIKAO BODI YA BARABARA, AKEMEA UTUPAJI TAKATAKA KWENYE MITARO

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akizungumza kwenye kikao cha Bodi ya Barabara.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, amekemea tabia ya baadhi ya wananchi mkoani humo, kutupa takataka kwenye mitaro, hali ambayo inasababisha mifereji kuziba na kushindwa kupitisha maji, ambayo hukosa njia na kuharibu miundombinu ya barabara, na kuingiza gharama Serikali ya kutenga fedha kila mwaka za matengenezo ya barabara.


Mjema amebainisha hayo leo Januari 18, 2022, wakati akifungua kikao cha bodi ya barabara mkoa, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa, na kuhudhuliwa na Wabunge, Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi, Wenyeviti wa Halmashauri, Meya wa Manispaa ya Shinyanga na Kahama, Katibu wa CCM Mkoa Donald Magesa na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho. aliwataka wananchi wa mkoa huo kuitunza miundombinu ya barabara, Mitaro na Madaraja ambayo yanatekelezwa, ili idumu kwa muda mrefu kuwahudumia, pamoja na kuacha kutupa takataka kwenye mitaro ya maji ili maji yapite na kutoharibu barabara.

“Barabara hizi zinajengwa kwa fedha nyingi sana, lakini baadhi ya wananchi wanatupa takataka kwenye mitaro, na kusababisha maji kushindwa kupita, na hatimaye kuharibu barabara, na kusababisha Serikali kuingia gharama ya matengezo ya mara kwa mara, fedha ambazo tunge elekeza kwenye miradi mingine ya maendeleo,”alisema Mjema.

Aidha, aliwaagiza Wakala wa Barabara Tanzania TANROADS, TARURA na Wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia sheria za kudhibiti uharibifu wa miundombinu ya barabara kwa kuzuia shughuli za binadamu kufanyika kandokando ya barabara, upitishaji wa mifugo na kuzuia magari yenye uzito mkubwa.

“Rais Samia alishasema barabara zote zilindwe na zidumu kwa muda mrefu kuwa hudumia wananchi zaidi ya miaka 30, hivyo viongozi tunapaswa kuzilinda barabara hivi, pamoja kudhibiti ung’oaji wa alama za usalama barabarani,,”alisema Mjema.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa, aliagiza katika utekelezaji wa miradi ya miundombinu hiyo ya barabara, mitaro, na madaraja, isimamiwe kikamilifu ili ijengwe kwa ubora unaotakiwa pamoja na kukamilishwa kwa wakati

Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akichangia kwenye kikao hicho, aliwataka Wakala wa Barabara Tanzania TANROADS pamoja na Tarura, wawe wanawapatia kazi Wakandarasi ambao wapo katika maeneo yao, ili wapate kuwabana vizuri katika utekelezaji wa miradi hiyo ya barabara.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga akizungumza kwenye kikao hicho, aliwataka pia Wakala wa Barabara Tanzania TANROADS na Tarura wanapotoa kazi zao wawe wanawapatia Wakandarasi ambao wanauwezo wa kufanya kazi hizo.

“Mheshimiwa mwenyekiti kuna Mkandarasi ambaye atatekeleza ujenzi wa Barabara kwa kiwando cha Changarawe kutoka Kahama hadi Kakola Bulyanhuru kilomita 70 Mkandarasi huyo nazani hana uwezo siridhiki na kazi zake ipo siku nita msweka ndani,”alisema Kiswaga.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo, akizungumza kwa niaba ya wabunge wenzake mkoani Shinyanga, alisema katika suala la kiuchumi ubora wa miundombinu ya barabara ni muhimu sana, huku akiguasia pia utekelezaji wa Barabara kwa kiwango cha Lami kutoka Kolandoto hadi Lalago ijengwe haraka ambapo tayari imeshategewa fedha Shilingi bilioni 2.4.

Kaimu Meneja Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoani Shinyanga Mhandisi Ferdinand Mdoe, akisoma taarifa ya utekelezaji wa miundombinu ya barabara mkoani humo, alisema katika bajeti ya mwaka wa fedha (2021-2022) waliomba Sh. bilioni 13.7 kwa ajili ya matengenezo ya barabara, lakini wakapewa Sh.bilioni 12.2.

Alisema katika bajeti ya mwaka wa fedha (2022-2023) wameomba tena kiasi cha fedha Sh. bilioni 13.7 kwa ajili ya matengezo ya miundombinu ya barabara, pamoja na fedha za maendeleo ya barabara Shilingi bilioni 2.7.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akizungumza kwenye kikao cha Bodi ya Barabara.

Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Donald Magesa, akizungumza kwenye kikao cha Bodi ya Barabara.

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza kwenye kikao cha Bodi ya Barabara.

Mbunge wa Jimbo la Kahama Jumanne Kishimba, akichangia kwenye kikao cha Bodi ya Barabara.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akichangia hoja kwenye kikao cha Bodi ya Barabara.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga, akichangia hoja kwenye kikao cha Bodi ya Barabara

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje, akichangia hoja kwenye kikao cha Bodi ya Barabara.

Kaimu Meneja Wakala wa Barabara Tanzania TANROADS Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Ferdnand Mdoe, akisoma taarifa ya TANROADS kwenyue kikao hicho.Meneja wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Oscar Gilbert, akisoma Taarifa ya TARURA kwenye kikao hicho.Wabunge wakiwa kwenye kikao cha Bodi ya Barabara, kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani, katikati ni Mbunge wa Kahama Jumaanne Kishimba, na kulia ni Mbunge wa Msalala Idd Kassim.

Wakuu wa wilaya wakiwa kwenye kikao cha Bodi ya Barabara, (kushoto) ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga, (katikati) Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude (kulia) ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.

Wakurugenzi wakiwa kwenye kikao cha Bodi ya Barabara.

wajumbe wakiwa kwenye kikao cha Bodi ya Barabara.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea. Kikao kikiendelea.

Kikao kikiendelea.

 

Kikao kikiendelea.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

 

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464