Na Marco Maduhu, SHINYANGA
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, ameongoza kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC), na kuagiza wanafunzi wote mkoani humo 29,757 ambao wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu, kuhakikisha wote wanaripoti shule.
Kikao hicho cha Kamati cha Ushauri ya Mkoa wa Shinyanga, kimefanyika leo Januari 19.2022 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Taasisi za Serikali, pamoja na Wabunge, Wakuu wa wilaya, Wenyeviti wa Halmashauri, Meya wa Kahama na Shinyanga, wajumbe wa Kamati ya Amani, pamoja viongozi wa CCM.
Mjema akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho, aliwaagiza viongozi mkoani humo wakiwamo Wakurugenzi, maofisa elimu na watendaji ngazi zote, kuhakikisha wanafuatilia taarifa za wanafunzi ambao wamefaulu kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu, wote waripoti shule na taarifa hiyo aipate mwezi wa Tatu.
“Mkoa wetu wa Shinyanga tulipokea fedha za Mapambano ya UVIKO-19 Shilingi bilioni 17.4 kwa ajili ya utekelezaji wa maendeleo, ambapo katika Sekta ya Elimu tulipokea Shilingi bilioni 9.1 ili kujenga vyumba vya Madarasa 453 na vyote vimekamilika kwa asilimia 100,”alisema Mjema
“Kwa upande wa ujenzi wa vyumba vya Madarasa kwa shule za Sekodari, tulijenga Madarasa 393, Shule Shikizi Madarasa 60 na yote haya yanatosha kubeba wanafunzi wote ambao wanaanza masomo mwaka huu, hivyo naagiza wanafunzi wote waliofaulu kidato cha kwanza waripoti shule na kuanza masomo,”aliongeza.
Aidha, alisema Januari 17 siku ambayo shule zimefunguliwa alipita kukagua mahudhulio ya wanafunzi mashuleni, na kuona hali yake ni nzuri siyo mbaya, na kuwasisitiza wazazi wapeleke watoto wao shule ili wakapate elimu na kutimiza ndoto zao.
Akizungumzia upande wake Sekta ya Afya, alisema Serikali mkoani walipokea Shilingi bilioni 7.7 kwa ajili ya kuboresha huduma za Afya pamoja na kujenga Majengo mapya na ununuzi wa vifaa Tiba.
“Kutokana na Rais Samia Suluhu Hassani kutoa fedha hizi nyingi za maendeleo, hivyo watu wa Shinyanga tuna kila sababu za kumshukuru Rais wetu sababu anatupenda na kututekelezea miradi mingi ya maendeleo na mingine mingi inazidi kuja, na sisi wasaidizi wake tutaendelea kuisimamia,”alisema Mjema.
Katika hatua nyingine, aliwataka maofisa kilimo mkoani humo, kuendelea kutoa elimu ya kilimo cha kisasa kwa wakulima, ili walime kisasa kwa kulima kilimo chenye Tija, na kuacha kulima kimazoea, ili wapate mavuno mengi.
Pia alisisitiza suala la upandaji miti kwa kila Kaya. Pamoja na kuacha kuharibu vyanzo vya maji, ili kuifanya Shinyanga kuwa ya kijani na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kupunguza hali ya ukame.
Naye Katibu Tawala msaidizi mipango Mkoa wa Shinyanga Mosesi Chila, akisoma taarifa ya mpango wa Bajeti ya mwaka wa fedha (2022-2023) kuwa Mkoa huo unatarajia kukusanya fedha kupitia mapato ya ndani Shilingi bilioni 27.2.
Alitaja baadhi ya vipaumbele katika utekelezaji wa Bajeti hiyo kuwa kuboresha Sekta ya kilimo, ufugaji, uvuvi, maliasili, elimu, Afya, na Maji.
Nao baadhi ya wajumbe wakichangia mada kwenye kikao hicho, kwa nyakati tofauti walimpongeza Rais Samia Suluhu Hassani, kwa kutoa fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo Sekta ya Elimu na Afya,
Aidha katika kikao hicho cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Shinyanga, ulizinduliwa pia Mpango Mkakati wa Dira ya maendeleo ya Mkoa wa mwaka wa fedha (2021-2022)-(2025-2026).
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa wa Shinyanga (RCC).
Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mabala Mlolwa, akizungumza kwenye Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Shinyanga RCC.
Kaimu Afisa elimu Mkoa wa Shinyanga Elysalver Nkanga, akiwasilisha Taarifa ya Elimu kwenye kikao hicho cha RCC.
Dk. Daniel Mzee akiwasilisha Taarifa ya Afya kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk, Yudas Ndugile kwenye kikao hicho cha RCC.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Grace Ntungi akiwasilisha Taarifa ya Shirika hilo kwenye kikao cha RCC.
Meneja Wakala wa Maji vijijini (RUWASA) Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Juliety Payovela, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji safi na salama kwenye kikao hicho cha RCC.
Meza kuu wakiwa kwenye kikao cha RCC Mkoa.
Wabunge wakiwa kwenye kikao cha RCC Mkoa, kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo, akifuatiwa na Mbunge wa Vitimaalum Santiel Kirumba, akifuatiwa na Mbunge wa Kahama Jumanne Kishimba, Mbunge wa Ushetu Emmanuel Cherehani na kulia ni Mbunge wa Ushetu Idd Kassim.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga, (kushoto) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph, Mkude kwenye kikao cha RCC Mkoa.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura (kushoto)akiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nice Munissy kwenye kikao cha RCC.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha RCC.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Buniphace Butondo, akichagia hoja kwenye kikao hicho cha RCC.
Mbunge wa Jimbo la Msalala Idd Kassim, akichangia hoja kwenye kikao hicho cha RCC.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje, akichangia hoja kwenye kikao hicho cha RCC.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza Mpango mkakati wa dira ya maendeleo wa mkoa, wa mwaka wa fedha (2021-2022-2025-2026).
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, Mpango mkakati wa dira ya maendeleo wa mkoa, wa mwaka wa fedha (2021-2022-2025-2026).
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga, Mpango mkakati wa dira ya maendeleo wa mkoa, wa mwaka wa fedha (2021-2022-2025-2026).
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, Mpango mkakati wa dira ya maendeleo wa mkoa, wa mwaka wa fedha (2021-2022-2025-2026).
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nice Munissy, Mpango mkakati wa dira ya maendeleo wa mkoa, wa mwaka wa fedha (2021-2022-2025-2026).
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, Mpango mkakati wa dira ya maendeleo wa
mkoa, wa mwaka wa fedha (2021-2022-2025-2026).
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Anderson Msumba, Mpango mkakati wa dira ya maendeleo wa
mkoa, wa mwaka wa fedha (2021-2022-2025-2026).
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kushoto) akimkabidhi Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, Mpango mkakati wa dira ya maendeleo wa mkoa, wa mwaka wa fedha (2021-2022-2025-2026).
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kulia) akimkabidhi Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Shinyanga Santiel Kirumba, Mpango mkakati wa dira ya maendeleo wa mkoa, wa mwaka wa fedha (2021-2022-2025-2026).
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kulia) akimkabidhi Mbunge wa Jimbo la Msalala Idd Kassim, Mpango mkakati wa dira ya
maendeleo wa
mkoa, wa mwaka wa fedha (2021-2022-2025-2026).
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa Sheikh Balilusa Hamis na Makamu wake Askofu Emmanuel Makala, Mpango mkakati wa dira ya
maendeleo wa
mkoa, wa mwaka wa fedha (2021-2022-2025-2026).
Na Marco Maduhu, SHINYANGA.