RC MJEMA AFANYA MIKUTANO YA HADHARA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI NA KUZITAFUTIA UFUMBUZI


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizitafutia ufumbuzi kero za wananchi mara baada ya kumaliza kusikiliza kwenye mkutano wake wa dhadhara katika Kata ya Bugarama Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama.

Na Marco Maduhu, KAHAMA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, amefanya mikutano miwili mikubwa ya hadhara, ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama.
Mjema amefanya mikutano hiyo ya hadhara leo Januari 14,2022 katika Kata ya Bugarama na Bulyanhuru Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama, pamoja na kukagua maandalizi ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha Lami Kilomita 1, katika eneo la Kakola- Bulyanhuru yenye thamani ya Sh.milioni 496.

Akisikiliza kero hizo na wananchi, baadhi amezitatua papo hapo, pamoja na zingine kuzielekeza kwa wataalam kutafutiwa ufumbuzi, na kuagiza mara baada ya kutatuliwa apewe taarifa zake.

"Ndugu zangu nimekuja kusikiliza kero zenu na kuzitafutia ufumbuzi, baadhi nimezitatua hapa hapa na zingine nimewaachia watalaam wazifuatilie na kuzitatua, ambapo Mkuu wa wilaya ya Kahama, atanipatia taarifa juu ya utatuzi wake, lengo tunataka wananchi waishi salama," alisema Mjema.

Aidha, aliwataka wananchi pia kupeleka watoto wao kuandikisha shule kwa ajili ya kuanza masomo Januari 17 mwaka huu, ili wakapate elimu, sababu Rais Samia Suluhu Hassani alishatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, na vimeshakamilika na kusubili wanafunzi kuvitumia ili watimize ndoto zao.

"Rais wetu Samia katoa fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa kupitia fedha za UVIKO-19 ili watoto wasome, sasa kazi iliyobaki ni ninyi wazazi kupeleka watoto shule, ili wakapate elimu," aliongeza Mjema.

Pia, aliwaonya wanaume kuacha tabia ya kurubuni wanafunzi na kuwapatia mimba za utotoni, bali wawa ache wasome na kutimiza malengo yao.

Katika hatua nyingine, aliwataka wananchi kuitunza miundombinu ya miradi mbalimbali ya maendeleo, ambayo inatekelezwa kwenye maeneo yao, ili idumu muda mrefu kuwa hudumia, pamoja na kumuunga mkono Rais Samia katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Mjema aliwasisitiza pia wananchi wajitokeza kwa wingi kupata Chanjo ya UVIKO -19, ili siku wakipata maambukizi ya virusi vya Corona wasiweze kudhulika zaidi, tofauti na wale ambao hawajapata Chanjo hiyo.

Awali wananchi wakitoa kero zao mbalimbali kwa Mkuu huyo wa Mkoa wa Shinyanga, walilalamikia huduma mbovu katika Sekta ya Afya, ambapo wagonjwa wamekuwa wakinyimwa dawa, pamoja na wale wenye kadi za bima CHF katika baadhi ya Zahanati, na kuambiwa wakanunue kwenye maduka ya watu binafsi.

Sekta nyingine iliyolalamikiwa ni elimu, kuwa hakuna walimu wa kutosha wa masomo ya Sayansi, pamoja na wazazi kutozwa fedha wakati wa zoezi la kuandikisha wanafunzi shule, na kuambiwa masomo kwa sasa ni kulipa ada, jambo ambalo Mkuu wa Mkoa alilipinga kuwa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote,

Maeneo mengine yaliyolalamikiwa ni ubovu wa miundombinu ya barabara, migogoro ya ardhi, pamoja na suala la ukosefu wa ajira kwa wazawa kwenye Mgodi wa dhahabu Bulyanhuru.

ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, alikuwa ameambatana na wataalam, Mkurugenzi wa Msalala, Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga, Mbunge wa Ushetu Emmanuel Cherehani, Mbunge wa Msalala Iddi Kassim, pamoja na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (katikati) akisikiliza kero za wananchi, kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga, (kushoto) ni Mbunge wa Jimbo la Msalala Idd Kassim.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizitafutia ufumbuzi kero za wananchi wa Bugarama Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizitafutia ufumbuzi kero za wananchi wa Bulyanhuru Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara, wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Mbunge wa Jimbo la Msalala Iddi Kassim, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara, wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emmanuel Charehani, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi wakati akiambatana na Mkuu huyo kwenye ziara zake wilayani Kahama.

Mwananchi Halfan Mjogo mkazi wa Bugarama akiwasilisha kero kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.

Mwananchi Maria Simba akiwasilisha kero kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.

Mwananchi Philipo Magendo akiwasilisha kero kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema

Mwananchi Zainab Masolwa, akiwasilisha kero kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.

Wananchi wa Bugarama wakisikiliza majibu ya kero zao, kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.

Wananchi wa Bugarama wakisikiliza majibu ya kero zao, kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.

Wananchi wa Bugarama wakisikiliza majibu ya kero zao, kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.

Wananchi wa Kakola- Bulyanhuru wakisikiliza majibu ya kero zao, kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.

Wananchi wa Kakola- Bulyanhuru wakisikiliza majibu ya kero zao, kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.

Wananchi wa Kakola- Bulyanhuru wakisikiliza majibu ya kero zao, kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.

Na Marco Maduhu, KAHAMA.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464