Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akitoa Msaada wa vifaa vya Shule, Madaftari na Kalamu kwa wanafunzi ambao wanaishi katika Mazingira Magumu wanaosoma katika Shule ya Sekondari Chamaguha, (kushoto) ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, ametoa msaada wa vifaa vya Shule, kwa wanafunzi ambao wanaishi katika mazingira magumu, katika shule za Msingi na Sekondari Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza mara baada ya kutoa msaada huo, amesema siyo watoto wote wazazi wao wanauwezo wa kuwanunulia vifaa vyote vya shule, na hivyo kuamua kutoa msaada wa Sare za shule, madaftari, na kalamu, kwa wanafunzi ambao wanaishi katika mazingira magumu ili wafurahie masomo yao.
"Nimefarijika kuona hali ya uandikishaji wanafunzi siyo mbaya, naomba wazazi waendelee kuleta watoto wao shuleni, elimu ni bure na hakuna ulipaji wa Ada," alisema Mjema.
"Natoa agizo kwa Wakuu wa Shule na Walimu, marufuku kurudisha wala kukataa kupokea wanafunzi ambao hawana sare za shule, wapokeeni waanze masomo, wakati wazazi wao wakiendelea kutafuta fedha za kuwanunulia sare hizo," aliongeza.
Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, aliwataka wanafunzi wasome kwa bidii na kuacha utoro ili watimiza ndoto zao, wakati Serikali ikiendelea kuwaboreshea mazingira mazuri ya kusoma.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ushirika Manispaa ya Shinyanga Pendo Peter, alisema mataraijio ya kuandikisha wanafunzi wa awali ni 75 lakini wameandikisha 43, darasa la kwanza matarajio 125 na wameandikisha 69, ambapo bado zoezi la uandikisha linaendelea.
Aidha, Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Chamaguha Manispaa ya Shinyanga Jonas Kapezi, alisema katika shule hiyo walipewa wanafunzi waliofaulu kidato cha kwanza 109, lakini hadi sasa wameandikisha wanafunzi 32 huku bado wakiendelea na zoezi hilo la kuandikisha wanafunzi.
Nao baadhi wanafunzi ambao wamepewa msaada huo wa vifaa vya Shule, zikiwamo sare za shule, Madaftari, na Kalamu, wamempongeza Mkuu huyo wa Mkoa, huku wakiahidi kusoma kwa bidii na kutimiza ndoto zao.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza mara baada ya kumaliza kutoa msaada wa vifaa vya shule, kwa wanafunzi ambao wanaishi katika mazingira magumu, pamoja na kukagua hali ya uandikishaji wanafunzi mashuleni.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akisisitiza baadhi ya wanafunzi ambao wanasoma katika Shule ya Msingi Ushirika wasome kwa bidii na kutimiza ndoto zao.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye ziara hiyo ya kuona hali ya uandikishaji wanafunzi na kutoa msaada wa vifaa vya shule kwa wanafunzi ambao wanaishi katika mazingira magumu.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, akizungumza kwenye ziara hiyo ya kuona hali ya uandikishaji wanafunzi na kutoa msaada wa vifaa vya shule kwa wanafunzi ambao wanaishi katika mazingira magumu.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Chamaguha wakisikiliza Nasaha za viongozi.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Chamaguha wakiendelea kusikiliza Nasaha za viongozi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akitoa Msaada wa vifaa vya Shule, Madaftari na Kalamu kwa wanafunzi ambao wanaishi katika Mazingira Magumu ambao wanasom katika Shule ya Msingi Ushirika Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akitoa Msaada wa vifaa vya Shule, Madaftari na Kalam kwa wanafunzi ambao wanaishi katika Mazingira Magumu wanaosoma katika Shule ya Sekondari Chamaguha, (kushoto) ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Zoezi la utoaji msaada wa vifaa vya shule likiendelea kwa wanafunzi ambao wanasoma katika magumu katika shule ya Sekondari Chamaguha.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Chamaguha Manispaa ya Shinyanga wakifurahia kusoma bila msongamano katika vyumba vipya ya Madarasa vilivyojengwa wa fedha za UVIKO-19.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Chamaguha wakiwa katika vyumba vipya vya Madarasa ya fedha za UVIKO-19.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (kushoto) wakipiga picha ya pamoja na kufurahi na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Chamaguha.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko na Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, wakipiga picha ya pamoja na walimu wa Shule ya Sekondari Chamaguha.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA.