Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza kwenye utiaji saini mikataba ya utekelezaji wa miradi ya maji.
Suzy Luhende, Shinyanga , Picha zote na Marco Maduhu
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, amewataka wakandarasi waliosaini mikataba ya utekelezaji wa miradi ya 10 ya maji mkoani humo yenye thamani ya Sh.bilioni 4.3 ya fedha za UVIKO-19 wahakikishe inatekelezwa kwa kiwango bora kinachotakiwa, ili iweze kudumu kwa muda mrefu na kuhudumia wananchi na vizazi vijavyo.
Mjema amewataka pia wakuu wa wilaya watoe ushirikiano wa karibu katika miradi hiyo ya maji ili wananchi waweze kupata maji ya kutosha, waondokane na adha ya ukosefu wa maji safi na salama.
Hayo ameyasema leo kwenye kikao cha kutoa taarifa na kusaini mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji ya mwaka 2021/2022 kilichofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa, ambao uliwahusisha viongozi mbalimbali, wakurugenzi, wabunge na viongozi mbalimbali kutoka ofisi ya mkoa wa Shinyanga.
"Leo mmesaini mikataba hii naomba muitekeleze kwa wakati na muitengeneze kwa kiwango zaidi na iwe endelevu kwa ajili ya vizazi vijavyo, kwani hatutaki kusikia mabomba yamekatika hovyo hovyo, hakikisheni changamoto hizo hazitokei mara kwa mara,na simamieni vizuri ili watu wasijiunganishie kiholela maji na kusababisha maji kukatika"amesema Mjema.
"Fedha hizi za Uviko 19 zilizotolewa na Rais wetu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani zisimamieni vizuri na toeni elimu kwa wananchi juu ya matumizi ya maji na kulinda miundo mbinu yake,"amesema Mjema.
Kwa upande wake Meneja wa RUWASA mkoa wa Shinyanga Mhandisi Julieth Payovela amesema mahitaji ya maji katika mkoa wa Shinyanga yanakadiliwa kufikia lita 41,893,600 kwa siku kwa wastani wa lita 25 kwa mtu, na upatikanaji wa huduma ya maji katika mkoa hadi disemba 2021 ni lita 26,556,875 sawa na asilimia 63,.39 ya mahitaji kwa siku.
Payovela amesema ujenzi wa mradi wa maji kijiji cha Mwashagi katika halmashauri ya Shinyanga mzabuni aliyeshinda ni Emirates Builders co. Ltd kutoka Dar es salaam, ujenzi wa mradi wa maji wa Bupigi Butungwa katika halmashauri ya Kishapu mzabuni ni Bent co.Ltd kutoka Dar es salaam, ujenzi wa mradi wa maji ya Mwashigini Msalala na Itumbi _ushetu Kahama mzabuni ni Tanzania Steel pipes kutoka Dar es salaam.
Aidha amesema mradi wa Nyasamba katika halmashauri ya Kishapu mzabuni ni Jonta investment Ltd, kutoka Shinyanga mradi wa maji Chibe katika manispaa ya Shinyanga, mzabuni ni Jonta Investment kutoka Shinyanga, upanuzi wa mradi wa maji Ngogwa Kitwana kwenda Wendele katika halmashauri ya manispaa ya Kahama mzabuni ni Jonta Investment Ltd kutoka Shinyanga.
Aidha katika ununuzi wa bomba za plasitc kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji Masengwa na awamu ya ll katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Bugayambelele manispaa ya Shinyanga mzabuni ni Simba Industries Ltd pipe kutoka Dar es salaam, uchimbaji mitaro na ulazaji wa bomba katika miradi wa Masengwa awamu ya ll mzabuni ni Local Fundi.
Katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mzabuni Elias Faya wa Shinyanga, na Uchimbaji wa mitaro na ulazaji wa bomba Bugayambelele manispaa ya Shinyanga mzabuni ni Local Fundi Geofley Romwand kutoka Shinyanga.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Jonta Investment John Ntalimbo Akizungumza kwa niaba ya Wakandarasi wote waliosaini mkataba huo alisema watahakikisha wanafanya kazi kwa kiwango kinachotakiwa na kwa wakati unaotakiwa, lakini aliomba ushirikiano wa karibu na serikali.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza kwenye utiaji saini mikataba ya utekelezaji wa miradi ya maji.
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Juliety Payovela, akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji kwa wananchi juu ya fedha za UVIKO-19.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Donald Magesa akizungumza kwenye hafla hiyo ya utiaji saini mikataba ya miradi ya maji.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkandarasi John Ntalimbo kutoka Kampuni ya Jontainvestment akizungumza kwa niaba ya wakandarasi wenzake kwenye hafla hiyo na kuahidi kutekeleza miradi hiyo kwa kiwango kinachotakiwa.
Zoezi la utiaji saini mikataba ya utekelezaji miradi ya maji likiendelea.

Wabunge wa Shinyanga wakishuhudia zoezi hilo la utiaji saini mikataba ya utekelezaji wa miradi ya maji.
ushuhudiaji zoezi la utiaji saini mikataba ya utekelezaji wa miradi ya maji likiendelea.

Picha ya pamoja ikipigwa.
Picha ya Pamoja ikipigwa.
Picha zote na MARCO MADUHU, SHINYANGA
Picha zote na MARCO MADUHU, SHINYANGA