Wanafunzi wa kitongoji cha Nondwe kijiji cha Bukale kata ya Bulungwa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga walionufaika na shule shikizi.
Na Kareny Masasy
WANAFUNZI wa kitongoji cha Nondwe kijiji cha Bukale kata ya Bulungwa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameondolewa adha ya kutembea umbali mrefu wa zaidi ya kilomita tano kwenda shuleni.
Adha hiyo imeondolewa baada ya serikali kujenga vyumba vya madarasa viwili katika shule shikizi ambapo mwalimu mkuu wa shule ya msingi Bukale Tumaini Ongati amesema hayo jana baada ya kamati ya siasa ya chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga kutembelea shule hiyo,
Mwalimu Ongati amesema kuwa wamepokea fedha za uviko-19 kiasi cha sh millioni 40 kwaajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa viwili ambapo idadi ya wanafunzi waliopo hivi sasa ni 168 kuanzia darasa la kwanza hadi la tatu.
"Hapa hakuna darasa la awali bali kuna darasa la kwanza hadi la tatu ambapo wengi wao wameanzishwa shule wakiwa na umri wa miaka tisa na kumi hii imesabiishwa na kuwepo umbali lakini hivi sasa wazazi wamefurahi shule kuwa karibu na watoto watawaleta mapema"anasema mwalimu Ogati,
Diwani wa kata hiyo Kuluwani Mteganoni amesema kuwa changamoto iliyokuwepo ni umbali wazazi walikuwa wanahofu ya kuwapeleka watoto shule kutokana na kuwepo pori na wanyama fisi kuwajeruhi watoto'
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi( CCM) mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa amesema kuwa sasa ni jitihada za wazazi kuwapeleka watoto shule serikali imetekeleza ilani ya chama cha mapinduzi kuwa elimu watapata watoto wote kwa kuwasogezea huduma hiyo karibu wasipate vikwazo vya aina yoyote.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464