Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali linalotetea haki za wanawake na watoto la Women Elderly Advocacy and Development Organization (WEADO) Eliasenya Nnko akitoa mafunzo kwa waelimisha jamii kutoka kata ya Masengwa.
Anna Nchenye kutoka shirika la WEADO akitoa mafunzo kwa waelimisha jamii.
Suzy Butondo.
WAELIMISHA
jamii juu ya kupambana na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na
Watoto kutoka kata ya Masengwa halmashauri ya Shinyanga wamepatiwa
mafunzo ya kwenda kuelimisha jamii, ili iweze kuachana na matukio ya
ukatili.
Akitoa mafunzo
hayo Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali linalotetea haki za
wanawake na watoto la Women Elderly Advocacy and Development
Organization (WEADO) Eliasenya Nnko yaliyofanyika katika kata ya
Masengwa halmashauri hiyo, amesema lengo la mafunzo hayo ni kupunguza
matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto katika kata
hiyo.
Nnko amesema ili
jamii iweze kuishi kwa amani na utulivu bila ya kufanyiana vitendo vya
ukatili ni lazima wananchi wapewe elimu, kwani kuna baadhi ya wazazi,
walezi na wanaume wanawafanyia ukatili watoto, wenza wao bila kujua,
lakini wakipatiwa mafunzo watakuwa na uelewa.
"Utafiti
uliofanyika ulionesha matukio mengi ya ukatili yanatokea Majumbani
pamoja na Shuleni, na mengi yamekuwa yakifanywa na watu wa karibu na
familia, hivyo waelimishaji wetu wanatakiwa waelimishe jamii ili jamii
iwe na uelewa na kuachana na ukatili ikiwezekana kuuondoa kabisa na
kubaki amani"amesema Nnko.
"
Pia nawaomba sana wawezeshaji wote tuliowapa mafunzo mkatoe elimu hii
kwa jamii ili iweze kuwa na uelewa kwani wengi wao hawaelewi nini maana
ya ukatili, lakini tukielimisha jamii tunaamini itaelewa kwamba mtu
akifanyiwa ukatili atapata madhara gani, ikiwa na uelewa matukio ya
kijinsia yatapungua "ameongeza.
Kwa
upande wake , Mtendaji wa Kata ya Masengwa wilayani humo Hussein
Majaliwa, wakati akifungua mafunzo hayo amewataka waelimisha jamii
wasikilize kwa makini ili wakatoe elimu kwa jamii inayowazunguka ili
kupunguza ama kuondoa kabisa ukatili katika kata ya Masengwa.
Baadhi
ya waelimisha jamii juu ya ukatili Mayenga Mabula na Sarah Charles
wakazi wa kata ya Masengwa, wamesema elimu wameipata wataenda kuelimisha
jamii na wanaamini matukio ya kijinsia yatapungua.
Mafunzo hayo yameandaliwa na shirika la WEADO la mkoani Shinyanga kwa
ufadhili wa mfuko wa Ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT) wenye thamani ya
Sh.milioni 12.4.ambao utakoma March 2022, ambapo wamepewa mafunzo
waelimishaji nane, kitongoji Cha Ilobashi watu wawili, Ikonda watu
wawili, Bubale watu wawili.
Pia
shirika hilo lilitoa elimu kwenye vijiwe vya kahawa vilivyopo katika
kata hiyo katika vijiji vya Ilobashi, Ikonda, Bubale na Masengwa, ambapo
baadhi ya wazee walisema hawajui maana ya ukatili, hivyo walielimishwa
na kuelewa, nao wakaahidi wataenda kuelimisha kwa mtu mmoja mmoja ili
kuondokana na matukio hayo.
Baadhi
ya wazee na vijana waliokuwa kwenye vijiwe vya kahawa Magembe Kija na
Juma Shilinde ambaye ni Mwenyekiti wa kitongoji cha Nyati walisema kuna
matukio ya ukatili yalikuwa yakifanyika katika kijiji hicho wanaona ni
kawada tu, baada ya kupewa elimu wameelewa kuwa kumbe vitu vingi
vinavyofanywa na baadhi yao ni ukatili.
"Tunawashukuru
sana shirika la WEADO kwa kutuletea elimu hii kwani tulikuwa hatujui
kama usipomnunulia mtoto mavazi, viatu, kukutana ma mama bila idhini
yake, na kutompeleka shule mtoto,ni ukatili, tutaifikisha hii elimu hata
kwa wenzetu ambao hawapo hapa tunaimani jamii ya hapa Masengwa
itabadilika"amesema Shilinde.
Emmanuel Samson mkazi wa kata ya Masengwa alipokuwa akizungumza na mwandishi wa Shinyanga press club blog kuhusu masuala ya ukatili wa jinsia.
Wanaume wakiwa katika vijiwe vya kahawa wakipatiwa elimu ya ukatili wa kijinsia kutoka Shirika la WEADO katika kata ya Masengwa,Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464