WALENGWA TASAF WAFUNGUKA MAFANIKIO MBELE YA MKUU WA MKOA SOPHIA MJEMA


Mlengwa wa TASAF Farida Wiliam, akielezea mafanikio ambayo ameyapa kupitia fedha za TASAF na kubadilisha mfumo wa maisha yake.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

WALENGWA wa mpango wa Kunusuru Kaya Maskini TASAF Manispaa ya Shinyanga, wameeleza mafanikio waliyoyapata kupitia fedha hizo za Ruzuku, na kubadilisha hali za maisha.


Walibainisha mafanikio hayo jana kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, wa kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi, uliofanyika Mtaa wa mapinduzi Kata ya Ndala.

Walengwa hao wa TASAF kwa nyakati tofauti kila mmoja alisimama na kuelezea mafanikio yake aliyoyapata, ambapo wengi wao wa fedha hizo zimewasaidia kubadili hali ya maisha yao na kupata unafuu wa maisha tofauti na kipindi cha nyuma.

Miongoni mwa Walengwa hao Christina Ndimila, ambaye awali alikuwa akiishi kwenye nyumba ya tope ,lakini baada ya kuingia kwenye mpango huo wa TASAF sasa hivi anaishi kwenye nyumba imara ya Bati.

Naye Farida Wiliam, alisema baada ya kuanza kupata fedha za TASAF, alianza kununua Bata na kuzifuga, ambapo wakifika wengi anauza baadhi na fedha hizo ana nunua Bati na sasa ameshafikisha Bati 20 ambazo ana tarajia kuezeka kwenye nyumba yake.

"Sisi walengwa wa TASAF tunaishukuru sana Serikali kwa kutupatia fedha hizi, ambazo zimebadili mfumo wa maisha yetu na kuanza kutoka kwenye umaskini," walisema walengwa hao kwa nyakati tofauti.

"Tunampongeza pia Rais wetu Samia Suluhu Hassani kwa kutujali walengwa wa TASAF, na kutuletea tena fedha katika mpango wa tatu awamu ya pili, ili tuendelee kijiimarisha zaidi na kuuaga kabisa umaskini," waliongeza.

Naye Rahel John, alitaja baadhi ya changamoto kubwa ambazo zinawakabili walengwa wa TASAF, kuwa namna ya kupata malipo kupitia benki, ambapo wazee wanachoka kukaa kwenye mstari muda mrefu na hivyo kupata changamoto za kiafya.

Aliendelea kueleza pia fedha zao zinakatwa benki, na hivyo kushindwa kupata kiasi cha fedha husika, pamoja na kuzitumia katika nauli, jambo ambalo linasababisha kupata pesa pungufu, ambazo wanashindwa kuzitumia vizuri kuwatoa kwenye umaskini.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, alisema changamoto hizo zitafanyiwa kazi, ambapo ameshatoa maagizo kwa waratibu wa TASAF kuzishughulikia, pamoja na wale ambao vidole vyao havisomi kwenye mfumo, bali walipwe kwa njia ya kawaida.

Aidha, alitoa wito kwa walengwa wote wa TASAF mkoani humo, wazitumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa, na siyo kuzitumia kwa mambo ya Anasa, bali wawekeze kwenye miradi yenye tija ambayo ndiyo itawakomboa kimaisha.

Pia, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, alisema suala la wazee kukaa foleni benki muda mrefu limemsikitisha, pamoja na wengine kutoka umbali mrefu, hali ambayo ili sababisha mlengwa mmoja kupoteza maisha, na kubainisha kuwa suala hilo lazima lifanyiwe kazi ili pesa wazipate kwenye maeneo yao.

Naye Mratibu wa TASAF Manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone, alisema Changamoto hiyo ya malipo kwa mfumo wa benki, pamoja na makato ya fedha za walengwa, tayari ameshazunguma na meneja wa benki husika ya NMB ambapo linafanyiwa kazi.

Alitaja pia idadi ya walengwa ambao wapo kwenye mpango wa TASAF 111 awamu ya pili, kuwa ni 800 katika ya 1,215 ambapo Kaya hizo zilipita kwenye mchujo na zingine kukosa sifa, na kubainisha kuwa awamu hiyo pia wamepata Sh.bilioni 1.1 ambazo watawapatia walengwa.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza na walengwa wa TASAF.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye mkutano wa walengwa wa TASAF.

 

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, akizungumza kwenye mkutano wa walengwa wa TASAF.

Mratibu wa TASAF Manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone, akisoma taarifa ya utekelezaji wa mpango huo.

Mlengwa wa TASAF Farida Wiliam, akielezea mafanikio ambayo ameyapa kupitia fedha za TASAF na kubadilisha mfumo wa maisha yake.

Christina Ndimila, mlengwa wa TASAF akielezea mafanikio na changamoto ambazo zinawakabili kwenye mpango huo wa TASAF.

Rahel John Mlengwa wa TASAF, akielezea mafanikio na changamoto ambazo zinawakabili kwenye mpango huo wa TASAF hasa upande wa malipo kwa njia ya benk.

Walengwa wa TASAF wakiwa kwenye mkutano na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.

Walengwa wa TASAF wakiwa kwenye mkutano na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.

Walengwa wa TASAF wakiwa kwenye mkutano na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.

Walengwa wa TASAF wakiwa kwenye mkutano na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.

 

Awali Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kulia) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko kushoto, wakikagua ujenzi wa daraja wa watembea kwa miguu lililopo Upongoji- Ndala Manispaa ya Shinyanga ambalo limeshakamilika kujengwa.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

 

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464