Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mtaa wa Shinyanga Mjini Lazaro Mbogo, akizungumza kwenye uhitimisha wa siku 10 za maombi, ikiwamo kuliombea Taifa, pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
KANISA la Waandventista Wasabato Mtaa wa Shinyanga mjini, wamehitimisha siku 10 za maombi ikiwamo kuliombea Taifa amani, pamoja na Rais Samia Suluhu Hassani na Serikali yake yote, ili waiongoze nchi kwa kuongozwa na mwenyezi Mungu.
Maombi hayo yalianza januari 5 mwaka huu na kuhitimishwa leo, ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.
Mkude akizungumza wakati wa kutoa hotuba kwenye Kanisa hapo, amewataka viongozi wa dini kutoka Madhehebu mbalimbali nchini kuendelea kuliombea Taifa amani, ambalo kwa sasa linapita kwenye kipindi kigumu cha maadui wengi ambao wanataka kuvuruga amani iliyopo.
"Nalipongeza sana Kanisa hili la Waandventista Wasabato Shinyanga Mjini kwa kufanya maombi na kuliombea Taifa amani na Rais wetu Samia Suluhu Hassan, jambo ambalo ni jema sababu bila Mungu Serikali haiwezi kusonga mbele kuwatumikia wananchi," alisema Mkude.
"Nawaomba viongozi wa dini muendelee kuliombea Taifa amani, ambalo kwa sasa linapita kwenye kipindi kigumu cha maadui, ambao wapo kwa ajili ya kutaka kuvuruga amani, na wameanza kuvumisha elimu kwa sasa ni kulipa Ada," aliongeza.
Aidha, alisema Mkuu wa Mkoa amemuagiza kuwaambia wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kuwa, elimu ni bure na hakuna kulipa hata Shilingi, na wanafunzi wote siku ya jumatatu waende shule na asibaki hata mmoja nyumbani.
Katika hatua nyingine, amelipongeza Kanisa hilo kwa kujali watu wenye Mahitaji maalumu wakiwamo watoto, na kuwapatia misaada mbalimbali, jambo ambalo ameeleza ni kujipatia mibaraka kutoka kwa mwenyezi Mungu.
Kwa upande wake aliyekuwa Mzee wa Kanisa hilo Rafael Lyochi, akisoma Risala kwa niaba ya Mchungaji Lazaro Mbogo, alisema wameendesha maombi hayo ya siku 10 kuliombea Taifa pamoja na Rais Samia Suluhu Hassani.
Alisema katika maombi hayo, walijikita kuliombea Taifa amani, ukuaji wa uchumi wa nchi, kunyesha kwa mvua za kutosha ili wananchi walime na kupata chakula, pamoja na kumuombea Rais Samia Suluhu Hassani Mungu amuongoze katika utawala wake.
Naye Mchungaji Lucas Ndibato kutoka Mtaa wa Ushirombo, ambaye ndiye alikuwa akiongoza maombi hayo ya siku 10, akitoa Ibada kwenye uhitimisha wa maombi hayo, alisema Taifa hili lina hitaji kuombewa zaidi, sababu hakuna kitu kibaya kama kuishi kinafki katikati ya kupendana, ambapo unazani mpo pamoja kumbe wenzako wapo tofauti.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, akitoa hotuba katika Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, wakati wa kuhitimisha siku 10 za maombi ikiwamo kuliombea Taifa, pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan.
Mchungaji Lucas Ndibato kutoka Kanisa la Wasabato Mtaa wa Ushirombo, akiendesha Ibada kwenye uhitimisha wa siku 10 za maombi.
Mchungaji wa Kanisa la Waandventista Wasabato Mtaa wa Shinyanga Mjini Lazaro Mbogo, akizungumza kwenye uhitimisha wa siku 10 za maombi.
Mzee wa Kanisa la Wasabato Shinyanga Mjini aliyemaliza muda wake Rafael Lyochi, akisoma Risala kwa niaba ya Mchungaji wa Kanisa hilo Lazaro Mbogo, kuhusu siku hizo 10 za maombi.
Viongozi wa Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini, wakiwa na Mgeni Rasmi Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, (mwenye skafu), pamoja na wachungaji kwenye ibada maalum ya kuhitimisha siku 10 za maombi.
Mchungaji Lucas Ndibato kutoka Kanisa la Waadventista Wasabato Mtaa wa Ushirombo( kulia), akiongoza maombi ya kuombea viongozi wa Serikali, pamoja na Rais Samia Suluhu Hassani.
Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mtaa wa Shinyanga Mjini, wakiwa kwenye Ibada maalum ya kuhitimisha siku 10 za maombi.

Kwaya ya Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini (SAC) wakiiomba Nyimbo katika Ibada hiyo Maalum ya kuhitimisha siku 10 za maombi.

Kwaya ya vijana ya Kanisa la Waadventista Wasabato Shinyanga Mjini, wakiimba kwenye Ibada hiyo Maalumu kwa ajili ya kuhitimisha Siku 10 za Maombi.
Kwaya ya Kanisa la Waadventista Wasabato Kizumbi kutoka Mtaa wa Shinyanga Mjini, wakiimba kwenye Ibada hiyo Maalumu kwa ajili ya kuhitimisha Siku 10 za Maombi.
Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mtaa wa Shinyanga Mjini Lazaro Mbogo, akiendesha zoezi la ubatizo wa maji mengi kama maandiko yanavyosema, kwenye uhitimisha wa siku 10 za maombi.

Mchungaji Lucas Ndibato kutoka Kanisa la Wasabato Mtaa wa Ushirombo, (kulia) akimpatia Zawadi ya vitabu vya neno la Mungu, Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude.
Mgeni Rasmi Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, (katikati mwenye Skafu Shingoni)akipiga picha ya Pamoja na viongozi wa Kanisa la Wasabato, Wachungaji, na viongozi wa Serikali,mara baada ya kuhitimisha siku hizo 10 za maombi.
Mgeni Rasmi Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, (katikati mwenye Skafu Shingoni)akipiga picha ya pamoja na viongozi wa Kanisa la Wasabato, Wachungaji, viongozi wa Serikali na Pathfinder, mara baada ya kuhitimisha siku hizo 10 za maombi.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464
Na Marco Maduhu, SHINYANGA