WAZIRI KIJAJI ATEMBELEA KIWANDA CHA JAMBO, AONYA WAFANYABIASHARA KUPANDISHA BEI KIHOLELA YA VINYWAJI BARIDI

Waziri wa uwekezaji, viwanda na biashara Dk. Ashatu Kijaji, (wapili kushoto) akiangalia bidhaa za Juice ambazo zinazalishwa kwenye kiwanda cha Jambo, (wapili kulia) ni Mmiliki wa kiwanda cha Jambo Salum Hamis, na (kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kushoto) ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.


Na Marco Maduhu, SHINYANGA

WAZIRI wa uwekezaji, viwanda na biashara Dk, Ashatu Kijaji, amefanya ziara mkoani Shinyanga ya kutembelea kiwanda cha Jambo Food Products kuangalia shughuli za uzalishaji wa bidhaa mbalimbali, na kuonya wafanyabiashara kuacha tabia ya kupandisha bei ya vinywaji baridi kiholela.

Dk. Kijaji amefanya ziara hiyo jana, akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa.

Alisema mwaka Jana kuanzia Oktoba hadi Januari mwaka huu, kulitokea tatizo la baadhi ya vinywaji baridi kupanda bei ghafla, ndipo Serikali kupitia tume ya ushindani, ikabidi ifanye uchunguzi ili kubaini tatizo liko wapi, na kupata majibu kasi ya uzalishaji vinywaji hivyo ilipungua, kutokana na kuadimika kwa Sukari ya viwandani.

Alisema uchunguzi huo ulibaini kuwa licha ya kuadimika kwa Sukari hiyo ya viwandani, lakini wazalishaji wa vinywaji baridi hawakupandisha bei, ispokuwa mawakala wa usambazaji na wafanyabiashara ndiyo waliopandisha bei, na kuonya tabia hiyo isijirudie tena na watakaobainika watachukuliwa hatua.

“Baada ya kupanda bei ghafla ya vinywaji baridi, Serikali kupitia Tume ya ushindani ili bidi tufanye uchunguzi na kubaini vinywaji baridi vimeadimika sababu ya kupungua kasi ya uzalishaji kutokana na kutopatikana kwa Sukari ya viwandani sababu ya ukosefu wa Makasha ya kusafirishia Sukari hiyo kuja hapa nchini,”alisema Kijaji.


“Tume ya ushindani ili baini pia tatizo la kupanda kwa bei ya vinywaji baridi halitoke kwa wazalishaji, bali ni Mawakala wa usambazaji na wafanyabiashara ndiyo waliopandisha bei ya vinywaji baridi mara baada ya kuona bidhaa hiyo imeanza kuadimika sokoni,”aliongeza.

Aidha, alisema kutokana na tatizo hilo la ukosefu wa Makasha ya kufungashia Sukari na kuisafirisha, Serikali ilitafuta mbinu mbadala na kutumia Shehena kusafirishia Sukari hiyo, na sasa kuna Tani 25,000 ya Sukari ya viwandani hapa nchini na hakuna upungufu tena.

Katika hatua nyingine, alisema Serikali imeanzisha utoaji wa vibari vya kuagiza Sukari ya viwandani kwa njia ya mtandao, pamoja na kuboresha utoaji wa shehena bandarini ili zitoke kwa wakati, na kuahidi kuendelea kuwaboreshea mazingira mazuri ya wawekezaji hapa nchini.

Pia, Dk, Kijaji alitoa wito kwa wawekezaji kuja hapa nchini kuwekeza viwanda vya Sukari ya viwandani, sababu kuna maeneo mengi yametengwa kwa ajili ya uwekezaji, hali ambayo itasaidia kutotokea tena tatizo la kuadimika kwa Sukari hiyo, sababu itakuwa ikizalishwa hapa nchini na siyo kuagiza nje ya nchi.

Naye Mmiliki wa kiwanda cha Jambo Food Product cha mkoani Shinyanga Salum Hamis, alisema kutokana tatizo hilo la kuadimika kwa Sukari ya viwandani, wao hawa kupandisha bei ya bidhaa, isipokuwa ni wasambazaji na wafanyabiashara, na kutoa wito kwao wauze bidhaa kwa bei halisi.


Waziri wa uwekezaji, viwanda na biashara Dk. Ashatu Kijaji akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kutembelea kiwanda cha Jambo, kuona Shughuli za uzalishaji bidhaa mbalimbali, na kutoa Tamko la Serikali kuwa marufuku wafanyabiashara kupandisha bei ya bidhaa kiholela na pia nchi haina upungufu wa Sukari ya viwandani.

Awali Waziri wa uwekezaji, viwanda na biashara Dk. Ashatu Kijaji,(katikati) akiangalia uzalishaji wa Pipi kwenye kiwanda cha Jambo, (kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kulia) ni Mmiliki wa kiwanda hicho cha Jambo Salum Hamis. Nyuma mwenye Kofia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.

Waziri wa uwekezaji, viwanda na biashara Dk. Ashatu Kijaji, akiendelea kuona shughuli za uzalishaji wa vinywaji katika kiwanda cha Jambo.

Waziri wa uwekezaji, viwanda na biashara Dk. Ashatu Kijaji, (wapili kushoto) akiangalia bidhaa za Juice ambazo zinazalishwa kwenye kiwanda cha Jambo, (wapili kulia) ni Mmiliki wa kiwanda cha Jambo Salum Hamis, na (kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kushoto) ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.

Waziri wa uwekezaji, viwanda na biashara Dk. Ashatu Kijaji, (kulia) akingalia maji ya kunywa ambayo yamezalishwa katika kiwanda cha Jambo, (kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (katikati) ni Mmiliki wa kiwanda cha Jambo Salum Hamis.

Waziri wa uwekezaji, viwanda na biashara Dk. Ashatu Kijaji, akiwa katika kiwanda cha Jambo, akiangalia Shughuli za uzalishaji wa Juice ya Maembe.

Waziri wa uwekezaji, viwanda na biashara Dk. Ashatu Kijaji, akiwa katika kiwanda cha Jambo, akiangalia Shughuli za uzalishaji wa Juice ya Maembe.

Waziri wa uwekezaji, viwanda na biashara Dk. Ashatu Kijaji, (katikati) akiwa ziara katika kiwanda cha Jambo kuona Shughuli za uzalishaji wa bidhaa mbalimbali, (kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kushoto) Mmiliki wa kiwanda cha Jambo Salum Hamis, mwenye Kofia kwa nyuma ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.

Waziri wa uwekezaji, viwanda na biashara Dk. Ashatu Kijaji, (kushoto) akiwa ziara kwenye kiwanda cha Jambo kuona Shughuli za uzalishaji bidhaa mbalimbali. (kulia) ni Mmiliki wa kiwanda hicho Salum Hamis.

Waziri wa uwekezaji, viwanda na biashara Dk. Ashatu Kijaji (kushoto) akiendelea na ziara ya kutembelea kiwanda cha Jambo kuona Shughuli za uzalishaji wa bidhaa mbalimbali, (kulia) ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, Mbele yao ni Mmiliki wa kiwanda hicho Salum Hamis.

Waziri wa uwekezaji, viwanda na biashara Dk. Ashatu Kijaji, akiwa katika ziara kwenye kiwanda cha Jambo kuona Shughuli za uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.
 
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464