Na Mathias Canal, Wizara
ya Kilimo-Manyara
WAZIRI wa Kilimo,
Profesa Adolf Mkenda ameiagiza Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI)
kutengeneza vipeperushi ambavyo vitasambazwa kwenye halmashauri za wilaya
nchini ili kuitangaza mbolea ya hapa nchini.
Kauli hiyo ameitoa leo
tarehe 7 Januari 2022 wakati alipofanya ziara katika kiwanda cha Minjingu
kilichopo Wilaya ya Babati mkoa wa Manyara akiongozana na Mkurugenzi wa Mazao
Wizara ya Kilimo Ndg Nyasebwa Chimagu, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mbolea
Tanzania (TFRA) Dkt Stephan Ngailo, Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo
(TARI-Mlingano) Dkt Catherine Senkoro.
Profesa Mkenda amesema kwa sasa wanataka kufanya tathimini kama mbolea iuzwe nje kwa kiasi gani hususani ambayo haitumiki hapa nchini bila hivyo mantiki ya kiuchumi haina maana yoyote.
"Vipeperushi
vitengenezwe na TARI mshirikiane na wenzenu muandike maneno tupeleke Mkoani
haraka watu wajue ipi ya kuoteshea mazao gani na ndani ya wiki mbili tuwe
tumehamasisha halafu tuangalie mbolea inakwenda kiasi gani tukiona kwamba bado
ipo ya kutosha tutafanya tathimini haraka kwamba bado tuendelee kuzuia na
tunazuia ili nini" Amekariwa Prof Mkenda
Aidha, amemtaka
Mkurugenzi wa Maendeleo ya mazao kushirikiana na maafisa ugani kuwekeza maeneo
yanayozalisha chakula kwa wingi ili kuondokana na hali ya utegemezi pindi
kunapotokea changamoto ya chakula.
"Tutafute maeneo ya
kufanya mbolea hii kama shamba darasa, tutangazie maafisa ugani Kwa
kushirikiana na TARI na TFRA tutumie vipeperushi vya wizara kuitangaza mbolea
ya ndani ya nchi ili kiwanda cha mbolea kifanye kazi vizuri" Amesisitiza
Waziri Mkenda
Kiwanda kama hiki kisiposimama mkakati wetu hautaenda vizuri, kiwanda Cha mbolea kilichopo Dodoma tayari niliagiza Mkurugenzi wa Maendeleo ya mazao tumempeleka nchini Burundi kwenda kujifunza ndio amerudi nasubiri taarifa," Amesema
Aliongeza: Nenda huko
kaangalie mbolea kama tunaweza kununua kidogo lakini tuchukue uzoefu ambao
tunaweza kutumia ili kama kile kiwanda kikifunguliwa tuwe na kauli ya kusema na
sisi tumejaribu mahali flani tumeona efficiency yake, sasa hatuwezi kufanya
hivyo Kwa kiwanda ambacho hakifanyi kazi.
Aliwahakikishia kuwa
atazungumza na Katibu Mkuu ili kutafuta bajeti za kutengeneza vipeperushi ili
kusambaza kwenye kila wilaya ili kuhamasisha vinawafikia watu wengi zaidi.
Awali, Mkurugenzi wa
Kiwanda cha Minjingu kilichopo Wilaya ya Babati mkoani Manyara, Tosk Hans
alisema wametii agizo la kupeleka mbolea ya kutosha mikoa ya Kanda ya kusini
huku mikoa ya Iringa, Mbeya, Njombe, Songea, Rukwa, Sumbawanga yote ina mbolea
ya kutosha ya kupandia na kulimia licha ya kuwa na changamoto ya mvua.
"Bei yetu ni rafiki
hatutakuangusha kwani mkoa wa mbeya tumepeleka Tani 6200, mpaka mwisho wa
msimu, tuna tani 1600 ambazo zipo mikoa ya kusini, huku tu angoja hadi msimu
utakapoanza, ipo ya kutosha na bado ikihitajika tutapeleka na tuna tani 9000
zipo kwenye maghala hapa kiwandani ikingoja kwenda mahali popote itakapotokea
changamoto ya mbolea," Amesema Hans
Ameongeza kuwa
hawakusafirisha mbolea nje ya nchi mpaka changamoto ya ndani iishe, hivyo
kuomba mchakato huo uanze Kama wataruhusiwa.
MWISHO