Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Mwandishi wetu.Babati
WAZIRI Mkuu wa Tanzania Kassimu Majaliwa, ameagiza viongozi wa Serikali Mkoa wa Manyara, kufatilia ardhi ya wawekezaji ambayo haijaendelezwa katika bonde la Kiru wilayani Babati mkoani Manyara, ili igawanywe kwa wananchi walio na uhaba wa ardhi ya kilimo na ufugaji.
Katika wilaya hiyo Babati, wananchi wamekuwa na changamoto za maeneo ya malisho ya mifugo na maeneo ya kilimo na baadhi kuingia katika maeneo ya hifadhi za taifa na eneo la hifadhi ya jamii ya wanyamapori ya Burunge.
Akizungumza na wananchi wakati akikagua hospitali mpya ya wilaya ya Babati inayojengwa eneo la Mwada,Waziri Mkuu, alisema wawekezaji wenye ardhi kubwa ambayo hawalimi itarejeshwa kwa wananchi.
Waziri Mkuu alisema changamoto ya ardhi pia ipo katika maeneo ya wilaya za Hanang na Mbulu hivyo ni lazima ipatiwe ufumbuzi.
Awali Mbunge wa jimbo la Babati,Daniel Sillo alimuomba Waziri Mkuu, kusaidia kugawanywa kwa wananchi,maeneo ya Mashamba ya bonde la Kiru ambayo hayaja endelezwa.
Katika wilaya Babati, wananchi wamekuwa na changamoto za maeneo ya malisho ya mifugo na maeneo ya kilimo na baadhi kuingia katika maeneo ya hifadhi za taifa na eneo la hifadhi ya jamii ya wanyamapori ya Burunge.
Kutokana na ongezeko la shughuli za kibinaadamu mapito ya wanyamapori hasa eno la kwakuchinja yamevamia lakini pia maeneo ya Burunge WMA.