AGAPE WAENDESHA MAFUNZO KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO WILAYANI SHINYANGA, WANANCHI WAFUNGUKA UKATILI UNAOENDELEA NDANI YA JAMII

Meneja Miradi kutoka Shirika la Agape Peter Amani, akielezea madhumuni ya mradi kwa washiriki wa mafunzo hayo namna utakavyotekelezwa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto Kata Kata za Lyamidati na Lyabukande wilayani Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

SHIRIKA la Agape la mkoani Shinyanga, ambalo linatekeleza mradi wa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto wilayani Shinyanga, limetoa mafunzo kwa wananchi namna ya kupambana na matukio hayo, ili jamii iishi salama pamoja na wanafunzi wa kike kutoozeshwa ndoa za utotoni na kutimiza ndoto zao.

Mafunzo hayo yameendeshwa leo Februari 16,2022 ambayo yameshirikisha baadhi ya wananchi wa Kata ya Lyamidati na Lyabukande wilayani Shinyanga, ambao wanajengewa uwezo namna ya kwenda kutoa elimu kwa wananchi kuachana na vitendo hivyo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Meneja miradi kutoka Shirika hilo la Agape Peter Amani, anasema mafunzo hayo yatadumu ndani ya siku tatu, huku akibainisha shughuli ambazo watakuwa wakizitekeleza kwenye mradi huo ndani ya Kata hizo mbili, kuwa ni kutoa elimu ya malezi na makuzi kwa wazazi, kuunda mabaraza ya watoto, pamoja na kuwajengea uwezo baadhi ya wajumbe wa kamati za Mtakuwwa.

Amesema mradi huo wa kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto kwenye Kata hizo za Lyamidati na Lyabukande, watautekeleza ndani ya miezi mitatu, kwa ufadhili wa mfuko wa Ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT) kwa thamani ya Sh.milioni 19.4

“Tumeanza kutoa mafunzo kwa baadhi ya wananchi kutoka Kata mbili za Lyamidati na Lyabukande wilayani Shinyanga, maeneo ambayo tunatekeleza mradi wetu wa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, ili siku mradi ukiisha waendeleze mapambano ya kupinga ukatili ndani ya jamii,”anasema Amani.

Naye Mwezeshaji wa Mafunzo hayo Afisa Maendeleo ya Jamii wilayani Shinyanga Christopher Malengo, amewataka wananchi wilayani humo waachane na mila kandamizi, ambazo ndizo zimekuwa chanzo kikubwa cha matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kuendelea ndani ya jamii.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo, kwa nyakati tofauti walibainisha matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ambayo bado yapo ndani ya jamii, kuwa kuna vipigo, utelekezaji wa familia hasa kipindi cha mavuno, ambapo wanaume huuza mazao na kwenda kuishi na wanawake wengine hasa kutoka mjini.

Walibainisha ukatili mwingine kuwa ni kukatisha masomo watoto wa kike, na kuwaozesha ndoa za utotoni kwa tamaa za kutaka kupata mifugo.

Meneja miradi kutoka Shirika la Agape Peter Amani, akizungumza kwenye mafunzo hayo ya kujengea uwezo baadhi ya wananchi wa Kata ya Lyamidati na Lyabukande wilayani Shinyanga, namna ya kwenda kupambana kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Meneja miradi kutoka Shirika la Agape Peter Amani, akiendelea kuzungumza kwenye mafunzo hayo.

Afisa Maendeleo ya Jamii wilayani Shinyanga Christopher Malengo, akitoa mafunzo kwa washiriki namna ya kupambana na matukio ya ukatili, pamoja na malezi bora ndani ya familia.

Afisa Maendeleo ya Jamii wilayani Shinyanga Christopher Malengo, akiendelea kutoa elimu kwa washiriki.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.

Mafunzo yakiendelea.

Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464