Afisa Maendeleo ya jamii mwandamizi kutoka Bonde la Kati la Maji mkoani Singida Nelea Bundala, akipanda mti kutunza chanzo cha Maji cha bwawa la Mhumbu lililopo Songwa wilayani Kishapu.
Na Marco Maduhu, KISHAPU
BONDE la kati la maji lenye makao yake makuu mkoani Singida, wameadhimisha siku ya kitaifa ya upandaji miti, kwa kupanda miti 3,000 katika chanzo cha Maji katika bwawa la Mhumbu lililopo Songwa wilayani Kishapu.
Afisa Maendeleo ya jamii mwandamizi kutoka bonde la kati la maji mkoani Singida Nelea Bundala, akizungumza leo kwenye zoezi hilo la upandaji miti, amewataka wananchi kutofanya shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji, ili kulinda vyanzo hivyo na kunufaisha vizazi na vizazi.
Amesema wameamua kuadhimisha siku hiyo ya upandaji miti kitaifa, kwa kupanda miti kwenye chanzo hicho cha maji katika bwawa la Mhumbu wilayani Kishapu, ambalo kwa kiasi kikubwa limeathiriwa na shughuli za kibinadamu, na kusababisha kina chake kupungua hali ambayo ni hatari kwa chanzo hicho kutoweka.
“Natoa wito kwa wananchi ambao wanaishi kwenye bwawa hili la maji la Mhumbu lililopo hapa Songwa wilayani Kishapu, waache kufanya shughuli za kibinadamu kando kando na vyanzo vya maji, ili kulinda vyanzo hivi vidumu miaka mingi,”alisema Bundala.
“Leo tumeamua kupanda miti kwenye chanzo hiki cha maji katika bwawa hili la maji la Mhumbu wilayani Kishapu, ili kurudisha uoto wa asili na kuzuia wananchi kutofanya shughuli za kibinadamu kando kando na vyanzo vya maji umbali wa mita 60,”aliongeza.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Emmanuel Jonhson, aliwasihi wananchi wilayani humo kutunza vyanzo vyote vya maji, pamoja na kuacha tabia ya kukata miti hivyo na uchomaji wa mikaa, kitendo ambacho ni chanzo cha uharibifu mkubwa wa mazingira Kishapu.
Kwa upande wake Mgeni Rasmi kwenye Zoezi hilo la upandaji miti Afisa Tarafa wilayani Kishapu Given Noah, akimwakilisha Mkuu wa wilaya hiyo Joseph Mkude, aliwataka wananchi ambao wapo jirani na vyanzo vya maji wilayani humo, kutofanya shughuli za kilimo na uvuvi ili vidumu na kuwahudumia katika shughuli zingine za matumizi ya maji.
Aidha, msimamizi wa vyanzo vya maji kutoka mgodi wa Almasi Wiliamson Diamond Mhandisi Rafael Matola, alisema bwawa hilo lilichimbwa na mgodi huo miaka ya 1955 hadi 57, lengo likiwa ni kupata maji ya matumizi kwenye mgodi huo, lakini kwasasa kina chake kimepungua sana kutokana na shughuli za kibinadamu.
Nao baadhi ya wananchi wa eneo hilo akiwamo Stephen Masanja, alisema walikuwa wakifanya shughuli za kibinadamu kando kando ya chanzo hicho cha maji, kutokana na kukosa uelewa juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji, lakini baada ya kupata elimu kwa sasa hawafanyi tena shughuli hizo kwa wingi, na kubaki watu wachache ambao bado ni wagumu kuelewa.

Afisa Maendeleo ya jamii mwandamizi kutoka bonde la kati la maji mkoani Singida Nelea Bundala, akizungumza kwenye zoezi la upandaji miti, katika Chanzo cha Maji bwawa la Mhumbu lililopo Songwa wilayani Kishapu.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Emmanuel Johnson, akizungumza kwenye zoezi hilo la upandaji miti kwenye chanzo cha bwawa la maji Mhumbu wilayani Kishapu.
Mgeni Rasmi kwenye Zoezi hilo upandaji miti Afisa Tarafa wilayani Kishapu Given Noah, akimwakilisha Mkuu wa wilaya hiyo Joseph Mkude, kwenye zoezi la upandaji miti katika chanzo cha maji kwenye bwawa la Mhumbu wilayani kishapu.
Msimamizi wa vyanzo vya maji kutoka mgodi wa Almasi Wiliamson Diamond Mhandisi Rafael Matola, akizungumza kwenye zoezi hilo la upandaji miti katika chanzo cha maji bwawa la Mhumbu wilayani Kishapu.
Afisa Maendeleo ya jamii mwandamizi kutoka Bonde la Kati la Maji mkoani Singida Nelea Bundala, akipanda mti, kulinda chanzo cha Maji cha bwawa la Mhumbu lililopo Songwa wilayani Kishapu.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Emmanuel Johnson, akipanda mti kulinda chanzo cha Maji bwawa la Mhumbu wilayani Kishapu.
Mgeni Rasmi kwenye Zoezi h upandaji miti, Afisa Tarafa wilayani Kishapu Given Noah, akimwakilisha Mkuu wa wilaya hiyo Joseph Mkude, akipanda mti kulinda chanzo cha Maji bwawa la Mhumbu lililopo Songwa wilayani Kishapu.
Zoezi la upandaji miti likiendelea.
Zoezi la upandaji miti likiendelea.
Zoezi la upandaji miti likiendelea.
Zoezi la upandaji miti likiendelea.
Zoezi la upandaji miti likiendelea.
Awali zoezi la uchimbaji mashimo kwa ajili ya kupanda miti likiendelea.
Awali Afisa maendeleo ya jamii mwandamizi kutoka bodi ya maji bonge la kati la maji mkoani Singida, Nelea Bundala akichimba mashimo kwa ajili ya kupanda miti kwenye chanzo hicho cha maji katika bwawa la Mhumbu wilayani Kishapu.
Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Emmanuel Johnson, akichimba mashimo kwa ajili ya kupanda miti kwenye chanzo cha maji katika bwawa la Mhumbu lililopo Songwa wilayani Kishapu.
Muonekano wa miti iliyopandwa.
muonekano wa miti iliyopandwa.
Miti ikiwa inashushwa kwa ajili ya kupandwa kwenye chanzo hicho cha maji.
Muonekano wa chanzo cha maji katika bwawa la Mhumbu lililopo Songwa wilayani Kishapu namna lilivyopungua kina cha maji kutokana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kuathiriwa na shughuli za kibinadamu.
Na Marco Maduhu, KISHAPU.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464