Picha ya pamoja ya wanufaika wa mikopo,viongozi wa benki ya CRDB na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga katika zoezi la kupokea hundi ya mikopo iliyotolewa na Halmashauri kupitia benki ya CRDB tawi la Shinyanga.
Upande wa kulia ni Meneja biashara kanda ya Magharibi kutoka Benki ya CRDB Jumanne Wagana akiongea baada ya kukabidhi hundi kwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na upande wa katikati ni meneja wa Benki hiyo tawi la Shinyanga Luther Mneney akiwa na diwani wa kata ya Solwa Awadhi Mbaraka.
Na Mwandishi wetu,
Vikundi 16 vya vijana ,wanawake na watu wenye ulemavu kutoka Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vimeweza kunufaika na mikopo wenye thamani ya Shs 173.8 iliyotolewa kipindi cha robo ya pili oktoba-desemba 2021/2022 na Halmashauri hiyo kwa kupitia mapato ya ndani.
Hayo yameelezwa Alhamisi 3 ,februari,2022 na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Nice Munissy alipokuwa akipokea hundi ya fedha za mikopo iliyokwisha tolewa kwa vikundi vya vijana,wanawake na watu wenye ulemavu na kutoka Halmashauri hiyo kupitia benki ya CRDB tawi la Shinyanga iliyokuwa ikitoa huduma za fedha kwa vikundi hivyo.
Hundi hiyo ilikabidhiwa na kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Nice Munissy mbele ya vikundi vya wanawake na vijana vilivyonufaika na mikopo kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao za ujasiriamali .
Mkurugenzi
wa Halmashauri hiyo Nice Munissy amesema
kuwa tayari wametoa kiasi cha sh millioni 173.8 ambazo zimetokana na mapato ya ndani kwa kuwakopesha wanawake vijana na watu wenye walemavu kupitia asilimia
kumi ya makusanyo ya Halmashauri hiyo.
“Haijawahi
kutokea kutoa kiasi hicho kwenye makundi
maalum ambapo lengo lilikuwa ni kutoa kiasi cha
sh million 192 ambazo
wangekopeshwa bila riba na kundi la
walemavu hawajajitokeza hivi sasa katika
kukopa lakini vipindi vingine vya robo mwaka walijitokeza na kukopa sasa wana
mradi wa mashine ya kusaga”.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Isack Sengerema amesema kuwa takwimu ya juzi iliyotolewa kuhusu ukusanyaji wa mapato halmashauri imekuwa ya tatu na mwaka uliopita ilikuwa ya mwisho na ndiyo maana wameona kutoa fedha kwenye makundi hayo sababu ni kodi zao na wanatakiwa kuzirejesha ili ziweze kuwanufaisha na wengine na fedha hizi walikuwa wapewa wajanja wajanja sasa zinawafikia hata watu wa pembezoni.
Kwa upande mwingine , Said Salehe Mwenyekiti wa Vijana amesema kuwa wanaishukuru serikali kwa kuwapatia mikopo ambao haina riba na wamekopa sh million 12 na kununua pikipiki tano ambazo watakuwa wanarudisha marejesho.
Pia Hawa
Migeto amesema kuwa kikundi chao wamekopa kiasi cha sh millioni 15 kwa ajili ya shughuli za ujasirimia mali na watazingatia kuzirejesha ili kuwapa nafasi watu wengine.
Meneja wa tawi la CRDB Mkoa wa Shinyanga Bw.
Luther Mneney Mneney
amesema kuwa suala la hela linahitaji
uaminifu ninyi vikundi ambao mmekopeshwa na mkazifanyie kazi zenye kuwaletea
manufaa na kurejesha kwa wakati.
Jumanne Wagana Meneja biashara kanda ya
Magharibi kutoka benki ya CRDB amepongeza ukusanyaji wa mapato hayo na kueleza kuwa shughuli wanazo ni nyingi na vikundi vingi
vimekuwa vikikopa hasa wale wenye kipato cha
chini hivyo amewaomba vikundi
hivyo wawe mabalozi kwa wengine na
kufafanua namna ya benki hiyo inavyoweza kutoa
mafao yenye faida ikiwemo bima.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Isack Sengerema akiongea kwenye kikao cha kukabidhiwa hundi huku akiwasisitiza wanavikundi kurejesha kwa wakati.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464