Kikao cha baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Kishapu kilijadili kupitisharasimu ya bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 kiasi cha zaidi y ash Billioni 44.9
Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Kishapu Peter Mashenji akisisitiza ukusanyaji wa mapato kwa madiwani wa halmashauri hiyo.
Na Kareny
Masasy,
MADIWANI wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu imepitisha rasimu ya bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 kiasi cha zaidi y ash Billioni 44.9 huku wakisisitiza kushirikiana katika ukusanyaji wa mapato ya ndani kupitia vyanzo vipya walivyoviibua.
Kabla ya
kuipitisha bajeti hiyo jana katika kikao maalum cha baraza la madiwani ambacho kilikuwa na ajenda ya kupitisha rasmi
ya mapendekezo ya bajeti mkurugenzi wa halmashauri hiyo Emanuel Jonson amesema
kuwa katika bajeti hiyo ukusanyaji wa mapato ya ndani ni sh Billioni
4,matumizi ya kawaida shBillioni moja na miradi ya maendeleo ni sh Bilioni 16.
“Ushirikiano
unatakiwa na taarifa za ukusanyaji ziwe ajenda kwa watendaji wa vijiji na kata katika vikao vyao na kueleza vyanzo vipya walivyoviibua ambapo nina ahidi bajeti hiyo itakwenda kama ilivyopangwa”amesema
Jonson.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo William Jijimya
amesema kuwa mpango wa bajeti wa zaidi
ya sh Billioni 44.9 hii ni dira ya Kishapu
wamepitisha bajeti hiyo na kutaka kuibua vyanzo vipya vya ukusanyaji
mapato na kuelekeza kwenye matumizi ili
kuondoa changamoto kwa wananchi na
kuhakikisha fedha hizo kuzipata kwa asilimia 100.
Baadhi ya madiwani hao akiwemo diwani viti maalum Felister Yahula na Bushi Mpina kutoka kata ya Mwamalasa wamepongeza bajeti hiyo na kudai ni nzuri kwani wamepitisha kwa nguvu zote na wako tayari kushirikiana kwani kuna vyanzo vingi vya mapato.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude amesema kuwa kamati ya fedha ndiyo inatakiwa kusisitiza ukusanyaji wa mapato na kusimamia matumizi yake na siyo bajeti ilivyopangwa kuivuruga na kuitumia kwenye masuala ya dharura .