Na Marco Maduhu, SHINYANGA
MADIWANI Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassani, kwa utoaji wa fedha na kutekelezwa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo Sekta ya Elimu, Afya, Maji na miundombinu ya Barabara.
Walisema katika Taarifa ambazo zimewasilishwa na madiwani wote, changamoto nyingi ambazo zilikuwa zikiwakabili kwa kila Kata zimetatuliwa, kutokana na fedha ambazo zilitolewa na Rais Samia Suluhu Hassani, na kuungana kwa pamoja kumpongeza kwa kazi kubwa ambayo ameifanya, na kumuahidi kuendelea kumuunga mkono.
“Madiwani wenzangu mmeona kazi kubwa iliyofanywa na Rais wetu ya kutoa fedha na kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwamo ujenzi wa vyumba vya madarasa, ambapo tumeondokana na changamoto ya kusumbuana na wananchi kuchangia ujenzi huo, hivyo tuna kila sababu ya kumpongeza Rais wetu Samia kwa kazi kubwa ambayo ameifanya,”alisema Mariam Nyangaka diwani wa Kitangili.
Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, aliungana na Madiwani hao kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassani kwa kazi kubwa ambayo ameifanya, ya kutoa fedha kutekeleza miradi mingi ya maendeleo ikiwamo Sekta ya Afya, Elimu, Maji na miundombinu ya barabara.
Aidha, alisema Rais Samia katika Manispaa hiyo ya Shinyanga pia ametoa kiasi cha fedha Sh. bilioni 3 kwa ajili ya kujengwa shule ya wasichana ambayo itajengwa maeneo ya Ndembezi, na itakuwa ikitoa elimu kuanzia kidato cha kwanza hadi Sita,
Pia. aliwataka madiwani hao kwa kushirikiana na viongozi wa wahakikishe wanafunzi wote ambao wanatakiwa kwenda shule waripoti mara moja, hususani wale wa kujiunga na kidato cha kwanza.
Katika hatua nyingine, amewataka madiwani kuongeza kasi ya kusimamia zoezi la ukusanyaji wa mapato ya ndani, ili kupata fedha za kuendelea kutekeleza miradi mingine ya maendeleo ikiwamo na ujenzi wa matundu ya choo mashuleni.
Mboneko ameonya pia tabia ya wananchi kuachia mifugo yao na kuzurura hovyo ambayo imekuwa ikishambulia miti iliyopandwa, na kuwataka viongozi wa maneo husika kwa kushirikiana na Maofisa mifugo, wazui vitendo hivyo ikiwamo na kuwatoza faini wamiliki wa mifugo hiyo.
Alikemea pia Mabaraza ya Ardhi ngazi ya Kata kuwa yawe sehemu ya kusaidia wananchi kutatuoa migogora ya ardhi na siyo kuwa chanzo cha migogoro hiyo, na kuagiza kama kuna baadhi ya viongozi hawafai kuwapo kwenye Mabaraza hayo waondolewe ili kutoendelea kuumiza wananchi.
Akizungumzia suala la bima ya CHF, aliwataka viongozi na Madiwani kuendelea kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko huo, pamoja na wale ambao kadi zao zimemaliza muda wazihuishe ili kuendelea kuwa na kadi hai, na kuwasaidia katika matibabu pale wanapokuwa hawa pesa.
Sanjari na hayo, aliagiza pia walimu wapya ambao wataajiriwa kwenye Manispaa hiyo wapelekwe wakafundishe maeneo ya pembezoni na mji, ambapo ndipo kuna changamoto kubwa ya upungufu wa walimu.
Kwa upande Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, alisema maelekezo yote ambayo yametolewa kwenye Baraza hilo atayafanyika, huku akibainisha vipaumbele vya Serikali ambavyo vilitolewa na Rais Samia, kuwa ni kuimarisha Sekta ya Afya, Elimu, kukuza uchumi kwa wananchi, kuimarisha mipango miji na usafi wa mazingira.
Aidha, alisema katika suala ujenzi wa matundu ya choo ambayo yanaonekana bado ni changamoto, kuwa kwa hesabu alizopiga kinahitajika kiasi cha fedha Sh.milioni 500 ili kumaliza tatizo hilo kwa shule zote, ambapo wakikusanya vizuri mapato ya ndani changamoto hiyo haitakuwepo tena.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, akiendesha kikao cha Baraza la Madiwani, (kulia) ni Naibu Meya Ester Makune.
Mkurugenzi wa ,Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza.
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza.
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza.
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza.
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza.
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza.
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza.
Madiwani wa vitimaalum Manispaa ya Shinyanga Zuhura Waziri akisoma Makabrasha kwenye kikao cha Baraza hilo la Madiwani.
Wataalam wakiwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Wataalam wakiwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Wataalam wakiwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Wataalam wakiwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Wataalam wakiwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA.