MFUKO WA MAWASILIANO KWA WOTE(UCSAF) KUJENGA MINARA 380 KWA AJILI YA MAWASILIANO

Afisa sheria mwandamizi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) Fredy Kandonga akizungumza wakati wa Mkutano wa wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa leo Jumanne Fabruari 15,2022 katika Ukumbi wa BoT Jijini Mwanza

Afisa sheria wa mwandamizi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) Fredy Kandonga akizungumza wakati wa Mkutano wa wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa leo Jumanne Faberuari 15,2022 katika Ukumbi wa BoT Jijini Mwanza

Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) akifungua Mkutano wa wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa leo Jumanne Faberuari 15,2022 katika Ukumbi wa BoT Jijini Mwanza.

Na mwandishi wetu.

Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) Tanzania umejipanga kujenga minara 380 kwa  ufadhili wa benki ya dunia kwa maeneo mbalimbali ya Tanzania kwa ajili ya kuongeza huduma ya mawasiliano kwa kata zenye changamoto ya mawasiliano kwa kipindi cha miaka mitatu kupitia mradi wa digital Tanzania.

Hayo yameelezwa jijini Mwanza, tarehe 15, February 2022 na Fredy Kandonga, Afisa sheria mwandamizi kutoka Mfuko wa Mawasiliano kwa wote katika Mkutano wa watoa huduma za mawasiliano kutoka mikoa ya kanda ya ziwa ulioratibiwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) umekutana na wadau wa huduma za mawasiliano kutoka mikoa ya kanda ya ziwa ili kutoa elimu juu ya majukumu ya UCSAF kwa watoa huduma za Televisheni, redio, mitandao ya kijamii na wasambazaji wa maudhui kwa njia ya waya.

Kandonga alisema, Mfuko wa mawasiliano kwa wote utajenga minara ya mawasiliano ipatayo 380 kwa fedha zenye thamani ya Shs billioni 62.1 kutoka benki ya dunia kupitia mradi wa digital Tanzania unaotekelezwa kwa miaka mitatu.

Minara ambayo imejengwa na kukamlika ni takribani   700 na minara ambayo inaendelea kujengwa na iko hatua mbalimbali ni 300, Rai yangu ni kwa watoa huduma za mawasiliano waone kwamba ni jukumu la wote katika kutoa huduma za mawasiliano si kwa serikali tu bali tushirikiane wote” Alisema Kandoga

“Aidha, Kandoga aliongeza kwa kusema kuwa mikataba ya ujenzi imesainiwa kwa ajili ya kuwafikia wananchi milioni 12,981,164 katika vijiji 3292 katika kata 1068”

Naye Mkuu wa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania kwa kanda ya ziwa Mhandisi Francis Mihayo aliwashukuru wadau kwa kushiriki mkutano huo na aliwataka kuuliza maswali mbalimbali juu ya changamoto zao ili kuweza kupatiwa majibu.

“Msibaki na maswali yasiyo na majibu, fursa hii ni yenu kwa kuuliza maswali na kupatiwa majibu ya undani kutoka kwetu, ili tuweze kuendelea na mashirikiano na mahusiano ya tija katika eneo la mawasiliano” Alisema Mihayo.

 

Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakipiga katika picha ya pamoja

 

Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa kwenye mkutano ulioandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) 

Wadau wa mawasiliano Kanda ya Ziwa wakiwa kwenye mkutano ulioandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF)

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464