MKURABITA KUWAINUA KIUCHUMI WAFANYABIASHARA SHINYANGA


Mtaalamu wa Sheria kutoka Mkurabita makao makuu Jijini Dodoma Harvey Kombe, akizungumza kwenye mafunzo hayo.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MPANGO wa kurasimisha Rasilimali na biashara za wanyonge Tanzania (Mkurabita), imeanza kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara na Madereva wa bodaboda na bajaji Manispaa ya Shinyanga, kuwajengea uwezo namna ya kufanya biashara zao kwa mfumo rasmi na kuwakuza kiuchumi.

Mafunzo hayo yameanza kutolewa leo Februari 9,2022 katika viwanja vya Zimamoto na Soko la Nguzo Nane, ambayo yatakoma Tarehe 16, kwa kukutana na wafanyabiashara 2,000, wakiwamo na madereva hao wa bodaboda na bajaji.

Mtaalam wa Sheria kutoka Mkurabita Makao Makuu jijini Dodoma Harvey Kombe, alisema kwa kushirikiana na uongozi wa Manispaa ya Shinyanga, wameamua kutoa mafunzo hayo kwa wafanyabiashara, pamoja na kuwaleta karibu na watoa huduma zikiwamo Taasisi za kifedha na kuwainua kiuchumi.

"Lengo la mafunzo haya kwa wafanyabiashara na madereva wa bodaboda na bajaji, ni kuwafanya wafahamu biashara zao ni kama biashara zingine, hivyo watumie fursa zilizopo kupitia Taasisi mbalimbali za kifedha, ambazo zitawafanya wainuke kiuchumi kupitia mikopo mbalimbali,"alisema Kombe.

Aidha, alisema mbali na kutoa mafunzo hayo, pia Marchi mwaka huu katika Manispaa hiyo ya Shinyanga, watafungua kituo jumuishi cha urasimishaji, uendeshaji wa biashara na uwekezaji, ambapo wafanyabiashara watakuwa wakikutana na wataalam mbalimbali na kupewa elimu ya kukuza biashara zao na namna ya kupata mikopo.

Naye Afisa Mfawidhi kutoka Latra mkoani Shinyanga Bahati Musiba, aliwataka madereva wa bodaboda na bajaji, kuzingatia sheria za kukata Leseni za usafirishaji, pamoja na kulipia Ada nyingine ili kufanya biashara zao kwa uhuru, pamoja na Serikali kupata mapato ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo.

Kwa upande wake Mkuu wa usalama barabarani wilaya ya Shinyanga (DTO) Dezidery Kaigwa, aliwataka madereva hao wa bodaboda na bajaji, kuendesha vyombo hivyo wakiwa na lesseni, pamoja na kuzingatia sheria zote za usalama barabarani, na kuacha kuendesha mwendokasi.

Nao baadhi ya ma Mameneja biashara kutoka Taasisi za kifedha, ikiwamo benki ya TCB, CRDB, NMB, na Exim, kwa nyakati tofauti walitoa wito kwa madereva hao wa bodaboda  bajaji na wafanyabiashara kuchangamkia fursa za mikopo kwenye Taasisi hizo ili wajikwamue kiuchumi.


Mtaalamu wa Sheria kutoka Mkurabita makao makuu Jijini Dodoma Harvey Kombe, akizungumza kwenye mafunzo hayo na wafanyabiashara wa bodaboda na bajaji.
Mtaalamu wa Sheria kutoka Mkurabita makao makuu Jijini Dodoma Harvey Kombe, akizungumza kwenye mafunzo hayo na wafanyabiashara wa Soko la Nguzonane.

Afisa Mfawidhi kutoka Latra mkoani Shinyanga Bahati Musiba, akizungumza kwenye mafunzo hayo.

Mkuu wa usalama barabarani wilaya ya Shinyanga (DTO) Dezidery Kaigwa,akizungumza kwenye mafunzo hayo.

Afisa Oparation kikosi cha usalama barabarani wilayani Shinyanga Emmanuel Palangyo akizungumza kwenye mafunzo hayo.

Afisa kutoka Benki ya NMB Ayubu Jonas akizungumza kwenye mafunzo hayo.

Neema Mongi kutoka benki ya TCB, akizungumza kwenye mafunzo hayo.

MwanaHamisi Iddy kutoka Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga akizungumza kwenye mafunzo hayo.

Afisa matekelezo kutoka NSSF Janety Evance, akizungumza kwenye mafunzo hayo.

Madereva bodaboda na bajaji wakiwa kwenye mafunzo hayo.

Madereva bodaboda na bajaji wakiwa kwenye mafunzo hayo.

Wafanyabiashara Soko la Nguzonane wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Wafanyabiashara Soko la Nguzonane wakiwa kwenye mafunzo hayo.


Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464