RC MJEMA AENDESHA KIKAO CHA KUJENGA UELEWA KUHUSU UTEKELEZAJI WA TASAF, TATHIMINI YA LISHE NA UTOAJI HUDUMA ZA CHANJO


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza kwenye kikao cha kujenga uelewa kuhusu utekelezaji wa TASAF, tathimini ya Lishe na utoaji wa huduma za Chanjo.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKUU wa mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, ameendesha kikao cha kujenga uelewa kuhusu utekelezaji wa TASAF, tathimini ya lishe na utoaji wa huduma ya chanjo ikiwamo ya UVIKO- 19, na kuwataka watendaji wa Serikali kila mmoja afanye kazi kwa bidii kwenye utekelezaji wa majukumu yake.

Kikao hicho kimefanyika leo Februari 3, 2022 katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, wakiwamo pia Maofisa Lishe, waratibu wa TASAF, Chanjo, Wakuu wa wilaya, pamoja na Kamati ya ulinzi na usalama Mkoa.

Akizungumza kwenye kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, asema watendaji wa Serikali mkoani humo, wanapaswa kufanya kazi kwa ushirikiano (Teamwork) na kila mmoja awajibike vizuri kwenye eneo lake na kuleta matokeo chanya.

Anasema kwenye Mkoa huo kila mipango inayoratibiwa inapaswa itekelezwe kwa asilimia 100 na siyo kusuasua, ambapo wakifanya kazi kwa kujituma na ushirikiano adhima hiyo itafanikiwa na kufikia malengo waliyojiwekea kama Mkoa, ikiwamo kuwahudumia wananchi.

“Natoa wito kwa watumishi wa Serikali mkoani Shinyanga fanyeni kazi kwa kujituma, kushirikiana na kila mmoja atekeleze majukumu yake na mkifanya hivyo mtafanya vizuri kwenye mipango yetu na kuwahudumia wananchi,”alisema Mjema

Akizungumzia upande wa TASAF amewataka waratibu wa TASAF, kutatua changamoto zote ambazo zinawakabili walenga hao, pamoja na kuwapatia elimu ya kuzitumia vizuri fedha hizo, ili ziwatoe kwenye umaskini na siyo kuzitumia kwa mambo ya Anasa.

Amesema kwa kipindi cha kuanzia Julai 2015 hadi Dicemba 2021 Mkoa huo ulipokea kiasi cha fedha Sh. bilioni 37.3 kwa ajili ya malipo kwa walengwa TASAF wapatao 45.487, huku akielezea mafaniko yaliyopatikana kwenye utekelezaji wa mpango huo, ambapo Kaya 24,600 zimejiunga na Bima ya Afya CHF iliyoboreshwa.

Ameendelea kusema kuwa Kaya 22,411 zimeanzisha miradi midogo ya kujiongezea kipato ikiwamo ufugaji wa mifugo, kilimo, uvuvi, na ujasiriamali, pia Kaya 4,119 ambazo zilikuwa zikiishi kwenye mkazi duni, zimeboresha makazi yao kwa kujenga nyumba bora na kuziezeka kwa bati, na nyingine kula milo mitatu kwa siku.

Pia amewataka Waratibu wa Chanjo na viongozi mbalimbali mkoani humo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili waendelee kujitokeza kwa wingi kupata Chanjo ya UVIKO 19 ili wapate kinga pale watakapoambukizwa virusi vya Corona.

Amesema mkoa huo ulipokea Chanjo ya UVIKO 19 jumla ya dozi 151,971, ambapo jumla ya dozi 113,121 sawa na asilimia 74 zimeshatumika na kubaki na salio la dozi 38,850.

Katika hatua nyingine amewataka Maofisa Lishe kuendelea kutoa huduma na elimu kwa wananchi juu ya kuzingatia lishe bora, ili kupunguza tatizo la udumavu kwa watoto, na Taifa hapo baadae lipate wataalamu wake pamoja na kuwa wanakaa vikao vya Tathimini cha Lishe kila Robo mwaka.

Kwa upande wao Wakuu wa wilaya, kwa nyakati tofauti kila mmoja akizungumza kwenye kikao hicho, waliahidi kusimamia utatuzi wa changamoto zote ambazo zinawakabi watendaji wa Serikali kwenye utekelezaji wa majukumu yao, ili wafanye kazi zao kwa ufanisi.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza kwenye kikao cha kujenga uelewa kuhusu utekelezaji wa TASAF, tathimini ya Lishe na utoaji wa huduma ya Chanjo.

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary akizungumza kwenye kikao hicho.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye kikao hicho.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwenye kikao hicho.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga akizungumza kwenye kikao hicho.

Mratibu wa TASAF Mkoa wa Shinyanga Dotto Maligisa akiwasilisha taarifa za Mpango wa TASAF kwenye kikao hicho.

Mratibu wa Chanjo ya UVIKO -19 mkoani Shinyanga Timoth Sosoma akiwasilisha Taarifa ya Chanjo ya UVIKO-19 kwenye kikao hicho.

Mratibu wa Lishe mkoani Shinyanga Denis Madeleke, akiwasilisha Taarifa ya hali ya Lishe kwenye kikao hicho.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kulia), (katikati) ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, na (kushoto) ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga, wakiwa kwenye kikao hicho.

 Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ikiwa kwenye kikao hicho.

 Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa ikiwa kwenye kikao hicho.

wajumbe wakiendelea na kikao.

wajumbe wakiendelea na kikao.

wajumbe wakiendelea na kikao.

wajumbe wakiendelea na kikao.

wajumbe wakiendelea na kikao.
wajumbe wakiendelea na kikao.

wajumbe wakiendelea na kikao.

wajumbe wakiendelea na kikao.

wajumbe wakiendelea na kikao.

wajumbe wakiendelea na kikao.

Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya kikao kumalizika.

Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya kikao kumalizika.

Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya kikao kumalizika.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.
 

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464