Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Ipeja wilayani Kishapu.
Na Marco Maduhu, KISHAPU
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, amefanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Ipeja Kata ya Itilima wilayani Kishapu kwa kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Mkuu wa Mkoa, akijibu kero za wananchi, likiwamo na suala la kumkataa mtendaji wa kijiji hicho Vicent Budotela, alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ya Kishapu. Kumsimamisha kazi kwa muda mtendaji huyo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma ambazo zinamkabili za kuihujumu Serikali ya kijiji, utendaji kazi mbovu, pamoja na kugomea maagizo ya viongozi kurudi kuishi kwenye kijiji hicho.
Mjema, alisema baada ua uchunguzi kukamilika ikionekana yupo salama, aendelea na kazi yake na ikibainika ana makosa basi achukuliwe hatua za kinidhamu, na kwenye kijiji hicho apelekwe mtendaji mwingine akawatumikie wananchi.
“Kutokana na malalamiko ambayo nimeyapata juu ya huyu mtendaji wa kijiji na kuagiza Mkurugenzi msimamishe kwa muda ili apishe uchunguzi wa tuhuma zake, na uchunguzi ukikamilika na akiwa salama basi apelekwe kwingine siyo kwenye hiki kijiji sababu wananchi hawamtaki na akirudi hapa anaweza kufanyiwa vitendo vibaya,”alisema Mjema.
Aidha, alizitatua kero mbalimbali za wananchi likiwamo suala la ukosefu wa huduma ya umeme, kuwa kwenye Halamshauri hiyo ya Kishapu kuna mradi wa umeme wa jua unakuja wenye Megawats 150 ambao utasambazwa kwenye vijiji vyote.
Pia alizungumzia suala la ukosefu wa Zahanati kwenye kijiji hicho, kuwa Serikali italifanyia kazi, sababu ndiyo ajenga kubwa hata ya Rais Samia Suluhu Hassani ya kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma za Afya, na ndiyo maana sasa hivi kuna ujenzi maeneo mengi ya Zahanati na vituo vya Afya.
Alizungumzia pia ubovu wa miundombinu ya barabara hasa kutoka kwenye kibao cha Shule ya Msingi Ipeja kwenda Shuleni na kuagiza Barabara hiyo ifanywe matengenezo ya haraka, ili kuondoa changamoto ya wanafunzi kupata usumbufu wa kwenda shule hasa kipidi hiki cha msimu wa mvua.
Alisema katika suala la maji safi na salama, wananchi watapata maji hayo sababu Serikali imeshasaini miradi 10 ya maji na wakandarasi, ambapo maji hayo yawafikia pia.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa, aliwataka hao wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa kwenye zoezi la Sensa na Makazi ya watu, ambalo litafanyika Agost mwaka huu, ili Serikali ipate idadi ya watu kamili na kuwa virahisi kutoa huduma kwa jamii ipasavyo sababu ya kuwa na takwimu sahihi za watu katika sehemu husika.
Awali mwenyekiti wa kijiji hicho cha Ipeja Juma Bundala, akizungumza kweye mkutano huo wa hadhara , alisema wananchi wa kijiji hicho hawamtaki mtendaji wa kijiji, sababu amekuwa chanzo cha kukwamisha maendeleo yao na pia alishagoma kuishi kwenye kijiji hicho na nimkaidi kutekeleza maagizo ya viongozi.
Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kishapu Shija Ntelevu, aliunga Mkono agizo la Mkuu wa Mkoa la kumsimamisha mtendaji huyo wa kijiji Vicent Budotela, kwa madai kuwa hata wao kama chama walisha mkalisha chini lakini akapuuza maagizo yao ikiwamo na kuishi kijijini humo.
Kwa upande wake Mtendaji huo wa kijiji Vicent Budotela alipopewa nafasi ya kujibu tuhuma hizo, alisema viongozi wa kijiji hicho wanamfanyia majungu, huku akifafanua kuwa suala la utozaji ushuru kwenye chanzo za mapato Mto Soka, kuwa fedha ambazo hua anazikusanya kwenye magari hayo ya mchanga hua anazipeleka zote Halmashauri.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Ipeja wilayani Kishapu.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Donald Magesa akizungumza kwenye Mkutano wa Hadhara katika kijiji cha Ipeja wilayani Kishapu.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC), Gaspel Kileo akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kishapu Shija Ntelezu, akizungumza kwenye mkutano huo wa hadhara.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, akizungumza kwenye mkutano huo wa hadhara.
Mwenyekiti wa kijiji cha Ipeja wilayani Kishapu Juma Bundala, akizungumza kwenye mkutano huo wa hadhara.
Mtendaji wa kijiji cha Ipeja wilayani Kishapu Vicent Budotela, ambaye amesimamishwa kazi kwa muda.
Wananachi wa kijiji cha Ipeja wilayani Kishapu wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa.
Wananachi wa kijiji cha Ipeja wilayani Kishapu wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa.
Wananachi wa kijiji cha Ipeja wilayani Kishapu wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa.
Na Marco Maduhu, KISHAPU.