Mlengwa wa TASAF Mwashi Masanja mkazi wa kijiji cha Ipeja-Itilima wilayani Kishapu, akiwa kwenye nyumba yake ambayo amejengewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.
Na Marco Maduhu, KISHAPU
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, ametimiza ahadi yake ya kumjengea nyumba ya kisasa mlengwa wa mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) wenye mpango wa kunusuru Kaya Maskini Mwashi Masanja, mkazi wa kijiji cha Ipeja wilayani Kishapu.
Mkuu huyo wa Mkoa Januari mwaka huu, alifanya ziara wilayani Kishapu ya kutembelea walengwa wa TASAF kuona maendeleo yao ya maisha, na alipofika kwenye Kaya ya Mwashi Masanja akamkuta anaishi kwenye nyumba ambayo siyo imara na kuahidi kumjengea nyumba nyingine.
Mjema alisema, mlengwa huyo anaishi na wajukuu zake wawili ambao bado ni wadogo kwenye nyumba ya tope licha ya kuezeka bati kupitia fedha za TASAF, ambapo mvua kubwa ikinyesha nyumba hiyo inaweza kuanguka, ndipo akaguswa na kuamua kutoa fedha Sh.milioni 3.5, ili ajengewe nyumba nzuri ndogo ya kujistili na wajukuu zake hao.
“Rais Samia Suluhu Hassani anataka tuwasaidie wananchi wake ambao wanaishi kwenye mkazi duni hasa wazee, na fedha hizi ambazo nimezitoa kujenga nyumba hii ya mlengwa huyu wa TASAF zinatoka kwake, na leo namkabidhi rasmi nyumba yake ambayo nilimuahidi kumjengea,”alisema Mjema.
“Nyumba hii ambayo nimemkabidhi mlengwa huyu wa TASAF ni ya chumba kimoja, ina umeme wa jua (Solar), Tenki la kuhifadhia maji, na ina choo cha kisasa,”aliongeza.
Naye Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) mkoani Shinyanga Gaspel Kileo, alimuunga mkono Mkuu wa Mkoa na kumnunulia mlengwa huyo wa TASAF kitanda, godoro pamoja na mashuka ili awe analala mahali ambapo ni pazuri.
Diwani wa Itilima wilayani Kishapu Lameck Msubato naye alimkabidhi Mbuzi wawili mlengwa huyo wa TASAF, ambao atawafuga ili apate mbuzi wengi na kumkwamua kiuchumi.
Kwa upande wake Mlengwa huyo wa TASAF Mwashi Masanja, alimshukuru Mkuu huyo wa Mkoa kwa kumjengea nyumba ya kisasa, ambayo ataishi yeye na wajukuu zake, na kuwashukuru na wadau wengine ambao wamemsaidia, huku akimuombea afya njema Rais Samia ili aendelee kuliongoza Taifa vizuri.
Aidha, Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akisoma taarifa ya ujenzi wa nyumba hiyo ya mlengwa wa TASAF, alisema ujenzi wake ulianza Februari 5 mwaka huu, na kukamilika tarehe 17 kwa gharama ya Sh.milioni 5.3 ambapo wadau wengine walitoa Sh. milioni 1.9 na yeye binafsi kutoa Sh. 400,000.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizunguma kwenye hafla fupi ya kumkabidhi nyumba mlengwa wa TASAF Mwashi Masanya mkazi wa kijiji cha Ipeja-Itilima wilayani Kishapu, ambayo alimuahidi kumjengea.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) mkoani Shinyanga Gaspel Kileo, akizungumza kwenye hafla hiyo ya Mlengwa wa TASAF kukabidhiwa nyumba yake, aliyojengewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, ambapo alimnunulia Kitanda, Godoro na Mashuka, ili kumuunga mkono mkuu huyo wa Mkoa.
Diwani wa Itilima wilayani Kishapu Lameck Msubato (kulia) akizungumza kwenye hafla ya mlengwa wa TASAF kukabidhiwa nyumba yake, ambapo alitoa mbuzi wawili kuumunga mkono Mkuu huyo wa Mkoa kwa kumsaidia mlengwa huyo., (kushoto) ni katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Donald Magesa.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, akisoma taarifa ya ujenzi wa nyumba ya mlengwa wa TASAF Mwashi Masanja, iliyojengwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.
Mwashi Masanja mlengwa wa TASAF (kulia) akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kushoto) kwa kumjengea nyumba hiyo ambayo ni imara.
Mlengwa wa TASAF Mwashi Masanja mkazi wa kijiji cha Ipeja-Itilima wilayani Kishapu, akiwa kwenye nyumba yake ambayo amejengewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.
Mlengwa wa TASAF Mwashi Masanja mkazi wa kijiji cha Ipeja-Itilima wilayani Kishapu, akiwa kwenye nyumba yake ambayo amejengewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kulia) ni nyumba yake ya zamani.
Wananchi wa kijiji hicho cha Ipeja wakishuhudia nyumba ya mlengwa wa TASAF ambayo imejengwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.
Jiwe la Msingi likionyesha nyumba hiyo ya mlengwa wa TASAF kuwa imejengwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akiwa na mlengwa wa TASAF Mwashi Masanja, (kushoto) kwenye Tenki la kuhifadhia maji.
Mbuzi wawili ambao amepewa Mlengwa huyo wa TASAF na diwani wa Itilima Lameck Msubato.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akikata utepe kuzindua nyumba ambayo amemjengea Mlengwa wa TASAF Mwashi Masanja (kulia kwake) mkazi wa kijiji cha Ipeja-Itilima wilayani Kishapu.
Na Marco Maduhu, KISHAPU
Na Marco Maduhu, KISHAPU
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464