SERIKALI YA WILAYA YA KAHAMA YAKARIBISHA WAWEKEZAJI WANAWAKE SEKTA YA MADINI.
Na Neema Sawaka
Serikali wilayani kahama inakaribisha wawekezaji wanawake katika sekta ya madini kwani maeneo ya uwekezaji yapo na hawanabudi kuchangamkia fursa hiyo ilii kukuza mitaji na kujikwamua kiuchumi.
Serikali imeweka mazingira rafiki ya uwekezaji katika sekta ya madini , ambapo zamani wanawake walikuwa wanabaguliwa kushiriki kwenye uwekezaji kwenye rasilimali madini.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga alipotembelea mgodi wa Kati wa Canuck mining company limited uliopo katika Kijiji Cha numbi katika kata ya mwakata halmashauri ya Msalala katika ziara yake ya kukagua shughuli za maendeleo wilayani humo.
Kwa sasa kuna baadhi ya wanawake ambao tayari wameingia kwenye sekta ya madini ambao tayari wanamiliki maduara na wengine wanajihusisha na uchimbaji.
Serikali imeweka mazingira wezeshi kwa wanawake kushiriki kwenye shughuli za uchimbaji madini na maeneo ya kuwekeza yapo na leseni zinatolewa kwa wale wanaohitaji kuwekeza kwenye sekta hiyo ya madini.
Kiswaga alisema,ardhi iliyopo kahama ni ya mheshimiwa Rais na mwananchi. anayetaka kushughulika na madini na kuwekeza anafika kwenye mamlaka husika kwa ajili ya kufuata utaratibu wa kuwekeza kwenye eneo alilolidhika nalo.
Kwa upande wake Meneja Rasilimali watu wa mgodi huo wa Canuck David Deogratius alisemaa katika mgodi huo wameajili wafanyakazi 240 Kati yao 22 ni wanawake.
Katika idara mbali mbali ambapo wanawake wana mchango mkubwa katika sekta hiyo."|Mgodi umetoa ajira hizo 240 kwa wananchi waliokaribu na wale wanaotoka katika vijiji vinavyozunguka mgodi huo|".Alisema David
Meneja huyo alisema shilingi milioni 10 zilitumika kulipa kifuta jasho kwa wachimbaji wadogo walikokuwa wakichimba na kumiliki na Maduara kwenye eneo Hilo. Huku milioni 159 zilitumika kulipa fidia za ardhi na mazao. Pamoja na nyumba kwa wananchi waliopisha uwekezaji huo.
Mmoja wa wachimbaji wa mgodi huo Leah makoye. Alisema kuwa wanawake. Wengi wamekuwa wakidhani kazi za uchimbaji zinafanywa na wanaume tu. Jambo ambalo hata wanawake wanaweza kufanya shughuli za uchimbaji. Ambapo hata yeye ameajiriwa na kampuni hiyo kwa ajili ya shughuli za uchimbaji na tayari anasomesha watoto kupitia kazi hiyo na anamiliki nyumba na rasilimali zingine kupitia kazi za uchimbaji.