Na Marco Maduhu, SHINYANGA
SERIKALI mkoani Shinyanga, imezundua zoezi la mfumo wa kuweka Anwani za makazi, pamoja na vibao vya barabarani vya kuelekeza maeneo ya mitaa.
Zoezi hilo pia lili hudhuliwa na Wakuu wa wilaya zote mkoani humo, akiwamo Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude, Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga, na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, Wakurugenzi wa Halmashauri, pamoja na viongozi wa CCM.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo la Anwani za makazi, ambalo litakoma April mwaka huu, amesema faida ya Anwani hizo zitasaidia wananchi kutambulika maeneo ambayo wanaishi, na itakuwa virahisi kuelekezana kwa kutumia namba za nyumba zao na kupatikana haraka.
“Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassani anaongea kwa vitendo na kutaka kila Mtanzania awe na Anwani yake ya mkazi, ambayo itawasaidia kufahamika mahali wanapoishi na kuwasaidia katika ufanyaji wa biashara zao sababu namba hizo zitaingia kwenye ramani za miji na nchi kwa ujumla,”amesema Mjema.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa, amewataka wananchi wa Mkoa huo wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa kwenye zoezi la Sensa na Makazi ya watu, ambalo litafanyika Agost mwaka huu, ili Serikali ipate idadi ya watu kamili na kuwa virahisi kutoa huduma kwa jamii ipasavyo, sababu ya kuwa na takwimu sahihi za watu katika sehemu husika.
Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, amepongeza zoezi hilo la uzinduzi la Anwani za makazi, na kutoa wito kwa wananchi kuzitunza alama hizo barabara za kuonyesha mitaa, ambazo zitakuwa na faida ya kuonyesha maeneo ya makazi yao na kusaidia kupata huduma mbalimbali kwa haraka.
Naoa baadhi ya wananchi ambao walihudhulia zoezi hilo la uzinduzi la Anwani za makazi waliipongeza Serikali, kuwa watakapokuwa na Anwani hizo zitasaidia wao kutambulika maeneo ambayo wanaishi, na hata kama likitokea tatizo ni virahisi kupata msaada haraka, kuliko kuelekezana kizamani.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema. akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la Anwani za makazi Mkoani humo.Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza kwenye zoezi hilo la uzinduzi wa Anwani za Makazi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (katikati) akizundua zoezi la Anwani za Mkazi mkoani humo, wapili kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga, mwenye Kofia ya kijani ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, mwenye sweta Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, wakwanza kulia Katibu wa CCM Mkoa Donald Magesa, akifuatiwa na MNEC Gaspel Kileo.
Muonekano wa namba za makazi ambazo zimezinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema katika Jengo la TANESCO.Muonekano wa namba za makazi ambazo zimezinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema katika Jengo la TRA.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464