SHIRIKA LA RAFIKI SDO LAUNDA MABARAZA YA WATOTO KWA AJILI YA KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA

 


   Wanafunzi kutoka kata za usule na ilola  wakisikiliza maelekezo ya wakufunzi juu ya shughuli za mabaraza ya watoto.

 

 Mariam Maduhu ,afisa mradi wa TUWALEE  kutoka shirika la RAFIKI SDO akizungumza  na watoto wakati wa kufungua baraza la watoto kata ya ilola.

 Afisa maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Halima Tendega akitoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa watoto wakati wa kuunda baraza la watoto.

 Na Elizabeth Nyanda.

 Shirika lisilo la kiserikali Linalojishughulisha na utetezi wa haki za wanawake na watoto mkoani Shinyanga la Rafiki SDO limeendesha zoezi la kuunda mabalaza ya watoto kwa kata mbili za Usule na Ilola katika halimashauri ya wilaya ya Shinyanga mkoni Shinyanga kwa lengo la kuwajengea uwezo watoto hao kupambana na vitendo vya ukatili katika jamii

Zoezi hilo la kuunda mabalaza ya watoto limefanyika kupitia mradi wa Tuwalee utakao dumu kwa muda wa miezi mitano kwa ufadhili wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (WFT)

Akizungumza wakati hafla ya kuunda mabaraza hayo afisa maendeleo ya jamii wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Halima Tendega amesema mabaraza hayo yatawasaidia kuwajengea uelewa watoto juu ya masuala mbalimbali ya ukatili, kujua haki zao na kujua namna ya kutolea taarifa matukio ya ukatili.

"Baraza la watoto ni chombo cha watoto kujisemea wenyewe tunaamini watoto wanafahamu vitu vingi saana na Kama wakipewa mafunzo kuhusiana na masuala ya ukatili na haki zao wanaweza kufikisha ujumbe vizuri kwa jamii lakini pia wanaweza kufichua vitu vingi kuhusu ukatili" amesema Tendega.

"Tuna mabaraza mengi ambayo yamesaidia kujua taarifa za matukio ya ukatili baada ya kuunda mabaraza na  na tumengundua watoto wanafahamu vitu vingi" ameongeza .

Akielezea malengo ya mradi huo mratibu wa mradi wa Tuwalee kutoka shirika la Rafiki SDO Mariam Maduhu amesema wameamua kutokomeza ukatili kuanzia ngazi ya familia kwa kutumia watoto.

" kupitia mradi huu watoto watajengewa uwezo na  kufundishwa sehemu sahihi za kutolea taarifa za matukio ya ukatili lakini watajua kujitetea wao kwa wao kwa sababu  wanafahamina na changamoto zao na kupitia utekelezaji wa mradi huu tunatarajia kuwa na jamii inayoelewa juu ya ukatili kwani watoto hawa watakuwa wakiwa na uelewa zaidi kuhusu vitendo vya ukatili",amesema Mariam

Kwa upande wao watoto walioshiki zoezi la uundaji wa mabaraza hayo wamesema elimu hiyo itawasaidia kuwa mabalozi wazuri katika jamii ili kudhibiti vitendo vya ukatili huku mwenyekiti wa baraza la watoto Ilola Janeth Beda ikibainisha namna mabaraza hayo yatasaidia kutetea watoto hususani wa kike kupata haki ya elimuKama watoto wa kiume.

 Wadau kutoka kata ya ilola walioweza kushiriki katika uundaji wa mabaraza ya watoto.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464