SHIRIKA LA YAWE LATOA MAFUNZO YA AFYA YA UZAZI NA HAKI NA STADI ZA MAISHA KWA WALIMU.


 

Picha ya Pamoja baina ya waalimu kutoka nyinda na puni,wakufunzi na mratibu kutoka shirika la YAWE.

 

 
Mkufunzi kutoka serikali Dr. Greyson Matoko akiwasilisha mada za Afya ya Uzazi.

Felister Melli Kaimu Afisa Ustawi wa jamii akiwasilisha mada za stadi za maisha.

 
 
 

Na mwandishi wetu.

Shirika la lisilo la kiserikali mkoani Shinyanga Youth Women Emancipation (YAWE) linatotekeleza shughuli za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto limewasa walimu kutumia muda wa vipindi vya masomo kutoa elimu ya Afya ya uzazi na stadi za maisha ili kupunguza
changamoto za ukatili wa kijinsia.

Hayo yameelezwa leo tarehe 1.2.2022 na mratibu wa mradii huo Bw, Deus Lyakis alipokuwa akitoa mafunzo hayo kwa waalimu wa kata ya nyida na puni kuhusu umuhimu wa Afya ya uzazi na Haki na Stadi za maisha ili kuwaongezea waalimu uelewa wa kutatua changamoto za watoto mashuleni zinazo sababisha vitendo vya ukatili ndani ya jamii.

Mafunzo hayo yaliyoendeshwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Wanawake Tanzania (Women Fund Tanzania) kupitia mradi wa “Keeping School Children Safe in Shinyanga” unaotekelezwa na shirika la YAWE kwa kipindi cha miezi mitatu katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa ruzuku ya Shs. Million 11.9.

Mafunzo haya yatumiwe na waalimu kutoa vipindi mashuleni kwa ajili ya kufundisha mada za afya ya uzazi stadi za maisha kwa watoto kupitia klabu za shule” Alisema Deus.

Aidha, Aliwaasa walimu kwenda kutoa maarifa hayo kwa watoto ili kuweza kuondoa dhana potofu kwa jamii kuwa mtoto wa kiume ni bora kuliko mtoto wa kike.

Kwa upande wake Dr. Greyson Matoko alisema kuwa jamii yetu inapaswa kuelimishwa zaidi juu ya kuona umuhimu wa usawa wa kijinsia ili kuondoa vitendo vya ukatili wa kijinsia. Alisema

Naye Mwalimu Ally Chifunda alisema kuwa mafunzo ni mazuri na atakwenda kuwapatia uelewa wanafunzi juu ya masuala kijinsia na changamoto zake, Pia ataweleza juu ya stadi za maisha.



 

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464