RAIS
Samia Suluhu Hassan leo Ijumaa Februari 4, 2022 akiwa njiani Magu jijini
Mwanza akielekea Musoma mkoani Mara ametengua uteuzi wa Wakurugenzi
Watendaji wa Halmashauri za Wilaya ya Buchosa, Iringa, Mbeya na Singida
Mjini kwa matumizi mabaya ya fedha za miradi ya maendeleo na upotevu wa
mapato katika halmashauri hizo.
“Siku
ile tunazitangaza fedha nilisema kama mkurugenzi anataka kuona rangi
yangu halisi achezee hizo fedha, sasa kwa traarifa zilizopo, Buchosa,
Iringa, Mbeya na Singida Mjini, wakurugenzi wamechezea fedha. Mheshimiwa
waziri (Waziri wa Tamisemi) wakurugenzi hao nimewatengua sasa hivi”
amesema Rais Samia na kuongeza
“Yule
wa Geita endeleeni na uchunguzi, na mimi timu yangu iko pale inafanya
uchunguzi naye wakiniletea na makossa kama haya nay eye attatenguliwa”
amesema
Awali,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi), Innocent Bashungwa alisema kuwa Wizara hiyo ilipata taarifa
za ubadhirifu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa kuhusu Wilaya ya Buchosa na maeneo
mengine.
Waziri Bashingwa alianza kwa kutoa pongezi kwa Rais Samia kutokana na ujenzi wa madarasa ya fedha za Uviko-19.
Baada ya kumaliza, Rais Samia alimuagiza Waziri Bashungwa kutaja maeneo mengine ambayo kumefanyika ubadhirifu.
“Hivi
sasa Ofisi ya Rais Tamisemi tunafanya uchunguzi katika halmashauri ya
Jiji la Mbeya, Singida, Iringa Mjini” amesema Bashungwa
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464