Wanahabari wakipewa mafunzo ya uhamasishaji masuala ya Chanjo.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
WANAHABARI kutoka Mkoa wa Simiyu na Shinyanga, wamepewa mafunzo ya kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kupata Chanjo mbalimbali ikiwamo ya UVIKO-19, ili wapate kinga ya mwili na kulinda Afya zao dhidi ya magonjwa ya mlipuko vikiwamo Virusi vya Corona.
Mafunzo hayo yamefanyika leo mkoani Shinyanga, na kuendeshwa na Wizara ya Afya, ambayo yalikuwa na lengo la kuwajengea uelewa waandishi wa habari na uhamasishaji kuhusu masuala ya Chanjo.
Afisa Program kutoka Wizara ya Afya mpango wa Taifa wa Chanjo Lotalis Gadau, alisema waandishi wa habari wana nafasi kubwa ndani ya jamii katika kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kupata Chanjo mbalimbali ikiwamo ya UVIKO-19, ambazo zitawalinda dhidi ya magonjwa ya mlipuko ambayo yanazuilika na Chanjo.
“Hali ya utoaji Chanjo ya UVIKO-19, Mikoa ya Kanda ya Ziwa ipo nyuma sana, hivyo waandishi ambao mmepata mafunzo haya ya Chanjo, tunaomba mkawe mabalozi wazuri wa kwenda kuelimisha wananchi kwa kutumia kalamu zenu, ili wajitokeze kwa wingi kupata Chanjo ya UVIKO-19,”alisema Gadau
Aidha, aliwataka wananchi ambao wamekuwa wakipata Chanjo dozi ya kwanza, warudi pia kupata na ya pili, ili wapate kinga kamili sababu wakikomea dozi moja siku wakipata maambuzi ya virusi vya Corona, wataweza kupata madhara makubwa na hata kusababisha kifo tofauti na yule ambaye amemaliza dozi zote mbili.
Katika hatua nyingine alitaja Chanjo za UVIKO-19 ambazo zimekubaliwa na Serikali kuwa ni Jensen, Sinopharm, Pfizer, Moderna na Sinovac, ambapo Chanjo hizo Nne dozi zake hutolewa mara mbili, kasoro ya Jensen ambayo yenyewe ni dozi moja tu.
Katika hatua nyingine alitaja magonjwa yaliyo katika mkakati wa kupunguzwa ama kutokomezwa kwa kutumia Chanjo mbalimbali, ukiwamo wa Polio, Surua Rubela, na Pepopunda kwa watoto wadogo.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Yudas Ndugile, aliwataja wananchi ambao wapo katika hatari endapo wakipatwa na maambukizi ya virusi vya Corona, kuwa ni wale wenye magonjwa nyemelezi wakiwamo wa Kisukari, Presha, HIV, Pumu na Athima, na kuwataka wachangamkie kupata Chanjo mapema.
Aidha, aliwataka pia Wanahabari wawe mstari wa mbele kuchanja Chanjo ya UVIKO-19, ili wawe chachu ya mabadiliko kwa wananchi, na hata kufikisha Taarifa zao kwa usahihi sababu ya kuwa na uelewa wa kutosha dhidi ya Chanjo.
Nao baadhi ya waandishi wa habari ambao wamepata mafunzo hayo, wameishukuru Wizara ya Afya kwa kulikumbuka kundi hilo, ambalo ni muhimu katika kuhamasisha wananchi kupata Chanjo ya UVIKO-19, huku wakitoa ushauri mafunzo hayo yangetolewa ndani ya siku Tano ili wakawa na ufahamu mpana na siyo kutolewa siku moja.

Afisa Program kutoka Wizara ya Afya mpango wa Taifa wa Chanjo Lotalis Gadau, akitoa mafunzo uhamasishaji masuala ya Chanjo kwa wanahabari Shinyanga na Simiyu.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk.Yudas Ndugile, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Kaimu Mkuu wa Kitendo cha Mawasiliano Serikalini Catherine Sungura, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Wanahabari kutoka Shinyanga na Simiyu wakipewa mafunzo ya uhamasishaji masuala ya Chanjo.
Wanahabari wakiendelea na mafunzo.
Wanahabari wakiendelea na mafunzo.
Wanahabari wakiendelea na mafunzo.
Wanahabari wakiendelea na mafunzo.
Wanahabari wakiendelea na mafunzo.
Wanahabari wakiendelea na mafunzo.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464