WASICHANA WALIOFAULU KIDATO CHA NNE 2021 KWA DARAJA LA KWANZA -WALIPIWA ADA NA OFISI YA MKUU WA MKOA DODOMA.

 

 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka.

Na mwandishi wetu:

Serikali ya Mkoa wa Dodoma imewalipia ada ya miaka 02 kwa wasichana wa mkoani humo walioweza kufaulu vizuri kitaalum kwa kupata daraja la kwanza kwa alama ya single digiti kwa matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2021. Wasichana walionufaika ni wale waliopata daraja la kwanza kwa alama ya single digiti ya 7 hadi 9 kutoka shule za serikali.

Hayo yameelezwa leo tarehe 7, February 2022 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka kupitia ukurasa wake wa Instagram aliochapishwa juu ya ofisi yake kufanikiwa kutoa zawadi hiyo kwa kundi hilo la wasichana wa mkoani humo.

“Uongozi wa mkoa umewazawadia kwa kulipia ada ya miaka 2(form five na form six) wanafunzi wotewaliofaulu mitihani ya kidato cha nne kwa kupata daraja la kwanza pointi 7(shule za serikali) na wasichana waliofaulu daraja la kwanza single digit point 7,8,9 shule za serikali” Aliandika Mtaka.

Mtaka hakuwacha waalimu katika utoaji wa zawadi hizo kwa shule za sekondari na msingi zilizofanya vizuri kwa kufaulisha kwa alama A katika masomo ya kidato cha nne na darasa la saba kwa shule za serikali.

Tumewazawadia waalimu wetu wote ambao walifaulisha kwa alama A katika masomo yao kwenye mitihani ya kidato cha nne, tumezawadia shule zote za msingi za serikali zimetoa watoto waliofaulu form one kwenda shule za vipaji maalumu” Aliandika Mtaka.

Ujumbe huo wa instragram wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma umeonesha kutoa kipaumbele kwa kundi wa wasichana kwa kuwapa kipaumbele zaidi mabinti waliofaulu kwa kwa alama ya single digiti ya 7 hadi 9 kwa shule za serikali. Mtaka ameonesha kuunga juhudi za watoto wa kike katika kufikia malengo yao ya kielimu kutokana na changamoto kubwa za ukatili wa kijinsia zinazo wakabili wasichana ndani ya jamii ya kitanzania.

Wasichana hao wataweza kusoma kidato cha 5 na 6 bila gharama zozote kutona na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kuwafadhili katika masomo yako kutokana na kufanya vizuri.

Glory Mbia, Mratibu wa Mfuko wa Wanawake Tanzania alitoa maoni yake katika kundi la mitandao ya jamii La mashirika yanayopinga ukatili mkoani Shinyanga kwa kuandika kuwa “uyu baba ana maono sana”.

Naye kwa upande wake, Mustapha Isabuda Mkurugenzi wa Shirika la GREEN COMMUNITY INITIATIVE linajishughulisha na kupinga ukatili mkoani Shinyanga, alitoa maoni yake katika jukwaa la whatsap la Malunde 1 blog kuwa kuandika kuwa “kuna la  ya kujifunza hapa kwa viongozi wetu”.

Estomine Henry, Mratibu wa ofisi ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga alisema kuwa uongozi wa viti maalum wa wanawake mkoa wa Shinyanga una deni kubwa la kufanya kazi zaidi katika agenda za wanawake na wasichana wa mkoa wa Shinyanga.

 

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464