PROFESSOR MWERA FOUNDATION, OFISI YA RC SHINYANGA WATOA TUZO WALIONG'ARA MATOKEO DARASA LA SABA NA KIDATO CHA NNE


Mwenyekiti wa Wamiliki wa shule za taasisi binafsi Mkoa wa Shinyanga, Jackton Koy ambaye ni Mkurugenzi wa Shule za Msingi na Sekondari KOM akipokea cheti kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (wa pili kulia) kwa niaba ya Mkurugenzi wa Shule ya Msingi Kwema Modern kwa kuwa katika 10 bora kitaifa katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba 2021. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Professor Mwera Foundation, Dkt. Hezbon Peter Mwera. Mwenye kiremba chekundu ni Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Taasisi ya Professor Mwera Foundation kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wametoa tuzo kwa shule zilizoongoza ufaulu kwa kiasi kikubwa kitaifa miaka mitatu mfululizo katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba na kidato cha nne ambazo shule ya msingi Nyakadoni iliyopo halmashauri ya Msalala, Manyada halmashauri ya Shinyanga na shule ya sekondari Istiqama Islamic iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.

Tuzo hizo za Vyeti 12 na Ma Tisheti 30 zimetolewa leo Alhamisi Machi 3,2022 katika kikao cha Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga kilicholenga kujadili maendeleo ya elimu ili kuboresha elimu mkoani Shinyanga kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Dafroza Ndalichako amesema Tuzo zingine zimeenda kwa Halmashauri zilizoongoza kwa ufaulu katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2021 katika mkoa wa Shinyanga ambazo ni Manispaa ya Shinyanga ambayo imekuwa ya kwanza kati ya halmashauri sita kwa upande wa shule za msingi na Msalala ikishika nafasi ya pili, na upande wa shule za sekondari Manispaa ya Shinyanga imeshika nafasi ya kwanza na Ushetu ikishika nafasi ya pili.

Tuzo zingine zimetolewa kwa shule zilizoingia kwenye 10 bora kitaifa katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2021 ambazo ni Rocken Hill kutoka Manispaa ya Kahama iliyoshika nafasi ya 3 na Kwema Modern kutoka Manispaa ya Kahama iliyoshika nafasi ya 6 huku tuzo ya mwanafunzi aliyeingia 10 kitaifa ambaye ni Kilugala Ngala Kilugala kutoka shule ya Kwema Modern Manispaa ya Kahama.

Pia tuzo zingine zimeenda kwa shule bora kitaifa zilizofanya vizuri Kimasomo kwenye mtihani wa darasa la saba mwaka 2021 ambazo ni Green Star Junior somo la Kiswahili, Rocken Hill (Hisabati),Kwema Modern (Sayansi na Teknolojia) na Rocken Hill (Sayansi na Teknolojia) zote zipo katika Manispaa ya Shinyanga.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema amezipongeza shule zilizofanya vizuri katika matokeo ya mitihani huku akiomba wadau kushirikiana katika kuboresha elimu mkoani Shinyanga kwani serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali katika kuboresha mazingira ya kujifunzia shuleni ikiwa ni pamoja na kujenga madarasa.

“Tunachokwenda kufanya sasa ni kuboresha mazingira yaliyopo shuleni. Wote tunatakiwa tushikamane, upande wa shule binafsi na za serikali. Tunataka shule zetu ziingie kumi bora kitaifa kila mwaka.Walimu na wadau wote tuwe wabunifu.


Waheshimiwa Ma DC nendeni mkasimamie upatikanaji wa chakula shuleni. Tunataka lishe katika upande wa shule. Tukasimamie pia mdondoko, watoto wafuatiliwe wako wapi, watoto wanatakiwa wawe shule kama tulivyowaandikisha”,amesema Mjema.


Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Professor Mwera Foundation, Dkt. Hezbon Peter Mwera ambaye ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Vyuo vya Ufundi Kanda ya Ziwa amesema taasisi yake imekuwa mdau mkubwa wa elimu na tuzo hizo ni mwendelezo wa tuzo ambazo wamekuwa wakizitoa ili kutoa kuwatambua wanaofanya vizuri na kutoa motisha.

“Taasisi yetu inafanya kazi nyingi ikiwemo kutoa tuzo kwa wanafunzi wanaofanya vizuri katika mitihani ya kitaifa ya darasa la nne,darasa la saba kidato cha pili, nne na sita. Mwaka 2021 tulitoa tuzo za mfano katika mkoa wa Mara na tunaahidi mwaka ujao tutatoa zawadi kubwa zaidi mkoani Shinyanga”,amesema Dkt. Mwera.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wamiliki wa shule za taasisi binafsi Mkoa wa Shinyanga, Jackton Koy ambaye ni Mkurugenzi wa Shule za Msingi na Sekondari KOM ameipongeza Taasisi ya Professor Mwera Foundation na ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga kwa kuandaa tuzo hizo ili kutambua wanafunzi na shule zinazofanya vizuri kwenye matokeo ya mitihani.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Professor Mwera Foundation, Dkt. Hezbon Peter Mwera ambaye ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Vyuo vya Ufundi Kanda ya Ziwa akizungumza kwenye kikao cha wadau wa elimu mkoa wa Shinyanga akielezea kuhusu tuzo zinazotolewa na Taasisi ya Professor Mwera Foundation kuwatambua wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Taasisi ya Professor Mwera Foundation, Dkt. Hezbon Peter Mwera ambaye ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Vyuo vya Ufundi Kanda ya Ziwa akizungumza kwenye kikao cha wadau wa elimu mkoa wa Shinyanga akielezea kuhusu tuzo zinazotolewa na Taasisi ya Professor Mwera Foundation kuwatambua wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza kwenye kikao cha wadau wa elimu mkoa wa Shinyanga na kuishukuru Taasisi ya Professor Mwera Foundation kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kuwatambua wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa na kutoa tuzo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza kwenye kikao cha wadau wa elimu mkoa wa Shinyanga na kuishukuru Taasisi ya Professor Mwera Foundation kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kuwatambua wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa na kutoa tuzo.
Mwenyekiti wa Wamiliki wa shule za taasisi binafsi Mkoa wa Shinyanga, Jackton Koy ambaye ni Mkurugenzi wa Shule za Msingi na Sekondari KOM akiipongeza Taasisi ya Professor Mwera Foundation na ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga kwa kuandaa tuzo hizo ili kutambua wanafunzi na shule zinazofanya vizuri kwenye matokeo ya mitihani ya kitaifa.
Mwenyekiti wa Wamiliki wa shule za taasisi binafsi Mkoa wa Shinyanga, Jackton Koy ambaye ni Mkurugenzi wa Shule za Msingi na Sekondari KOM akipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (kulia) kwa niaba ya Mkurugenzi wa Shule ya Msingi Kwema Modern 
Mkurugenzi wa Shule ya Msingi Rocken Hill, Zephania Madaha akipokea cheti kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema (kulia) kutokana na shule hiyo kuingia kwenye 10 bora kitaifa kwenye matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2021.
Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Shinyanga, Lucas Cleophace Mzungu (kushoto) akipokea cheti kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema. Manispaa ya Shinyanga imekuwa ya kwanza kati ya halmashauri sita kwa upande wa shule za Sekondari katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2021 katika mkoa wa Shinyanga
Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Shinyanga, Lucas Cleophace Mzungu (kushoto) akipokea cheti kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema. Manispaa ya Shinyanga imekuwa ya kwanza kati ya halmashauri sita kwa upande wa shule za Sekondari katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2021 katika mkoa wa Shinyanga
Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Shinyanga, Neema Mkanga (kushoto) akipokea cheti kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema. Manispaa ya Shinyanga imekuwa ya kwanza kati ya halmashauri sita kwa upande wa shule za msingi katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2021 katika mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akiendelea kukabidhi vyeti
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akiendelea kukabidhi vyeti na zawadi mbalimbali
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akiendelea  zawadi mbalimbali
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akiendelea kukabidhi vyeti na zawadi mbalimbali
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akiendelea kukabidhi vyeti
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akiendelea kukabidhi vyeti
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akiendelea kukabidhi vyeti na zawadi mbalimbali
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akiendelea kukabidhi vyeti.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akiwa na Maafisa Elimu Msingi na Sekondari Manispaa ya Shinyanga wakiwa na vyeti vya ushindi. Kulia ni Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Shinyanga, Lucas Cleophace Mzungu. Kushoto ni Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Shinyanga, Neema Mkanga.

Manispaa ya Shinyanga imekuwa ya kwanza kati ya halmashauri sita kwa upande wa shule za msingi katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2021 katika mkoa wa Shinyanga na imekuwa ya kwanza kati ya halmashauri sita kwa upande wa shule za Sekondari katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2021 katika mkoa wa Shinyanga


Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Soma pia:
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464