Na kareny Masasy
JUMLA ya vituo 71 vya kulelea watoto mchana (day care center) katika halmashauri ya manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga vimefungwa kutokana na kukiuka utaratibu na muongozo uliopo na badala yake wamiliki wake wamegeuza kuwa shule zisizo rasmi na kuanza kufundisha.
Kibagaya alisema kuwa jumla ya vituo 71 vya kulelea watoto mchana vimefungiwa kwa kukosa sifa na vituo 21 vimepewa muda wa kusajili kwa kuonekana kidogo wameweza kukidhi matakwa ya muongozo kwa kuwa na walezi wenye sifa na eneo la michezo na darasa lenye dhana za ujifunzaji wa awali kwa mtoto.
"Vituo 92 vimebainika kutokuwa na usajili na kuviendesha kinyemela bila kufuata utaratibu na muongozo unaotakiwa kwa maana ya kulea watoto wenye umri wa kuanzia miaka miwili hadi minne na sio kuandika Kama wanavyofanya sasa inatakiwa kuwawekea dhana za ujifunzaji,michezo na kuimba pekee"alisema Kibagaya
Kibagaya alisema kuwa wazazi wamekuwa wakiibiwa fedha zao kwa kutoelezwa ukweli na wamiliki wa vituo wanapowapeleka watoto kulelewa ni wajue ni mbadala wa dada wa kazi kwanza wanawachanganya wenye umri wa miaka miwili na minne darasa moja na kuanza kuwafundisha kuandika na kupewa kazi ya kuandika awapo nyumbani (homework).
"Nimewaomba wenye vituo ambavyo vimesajiliwa wawe mabalozi kwa mtu ambaye ameanzisha vituo bila utaratibu kwani vituo vingi vilivyofungiwa mazingira yake siyo rafiki kwa watoto tundu moja la choo ambalo wanachangia na watu wakubwa na wanao walea ni wale waliomaliza darasa la saba,kidato cha nne na kukosa ajira hawana sifa"alisema Kibagaya.
Martha Masota mmiliki wa kituo cha kulelea watoto mchana kilichopo kata ya Mhongolo ambacho kimepewa mwezi mmoja kuwa na usajili alisema kuwa amesomea suala la malezi na makuzi (ECD) na muongozo uliopo haitakiwi watoto hawa kufundishwa kwa kuandika bali zitumike zana ,kuimba na michezo na kuwepo watoto 25 tu na matundu ya vyoo na mazingira yawe rafiki.
Mratibu wa kitaifa wa mtandao wa malezi ,makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto (TECDEN )Bruno Ghumpi alisema kweli imebainika watoto hawa wanapojiunga na vituo vya kulelea watoto wadogo mchana huishia katika mfumo wa kufundishwa badala ya kujifunza kupitia michezo na kutumia zana kulingana na mazingira yao.
Baadhi ya wazazi manispaa ya Kahama Jeremiah Ndaki na Mariamu Fadhili walisema kuwa wamekuwa wakiwapeleka watoto wao kwenye vituo hivyo lakini watoto wanakwenda na daftari na kalamu na wamekuwa wakiandika kumbe ni kosa mpaka wafikie umri unaotakiwa.
J
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464