Mkuu wa Program kutoka Mfuko wa wanawake Tanzania (WFT-Trust) Carol Mango akizungumza wakati wa kuhitimisha mkutano kazi wao na mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka Mikoa mbalimbali ambayo wameyapatia Ruzuku ya utekelezaji wa miradi ya utetezi wa wanawake na watoto.
Na Marco Maduhu, DAR ES SALAAM
MFUKO wa Ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT-Trust), umehitimisha rasmi mkutano kazi na mashirika yasiyo ya kiserikali, ambayo wameyapatia Ruzuku ya utekelezaji wa miradi ya kutetea haki za wanawake na watoto.
Mkutano kazi huo ulianza jana Marchi 28/ 2022, ambao umehitimishwa leo Marchi 29/ 2022 Jijini Dar es Salaam, uliokuwa na lengo la kuyapatia mafunzo ya utendaji kazi mashirika hayo, na namna ya kuunganisha nguvu ya pamoja (TAPO) katika kuleta mabadiliko ya usawa wa kijinsia na ukombozi wa mwanamke kimapinduzi.
Mkuu wa Program kutoka mfuko huo wa Ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT-Trust) Carol Mango, ameyataka mashirika hayo, yale waliyojifunza kupitia mkutano huo wakayafanyie kazi na kuleta matokeo chanya kwenye utekelezaji wa miradi yao.
Alisema kutokana na changamoto za UVIKO-19 hawakuweza kukutana na Mashirika hayo ndani ya miaka miwili, ili kupata mrejesho wa utendaji kazi wao, pamoja na kufahamu changamoto ambazo zinawakabili na kuzitafutia ufumbuzi, pamoja na kubadilishana mawazo na uzoefu namna ya kufanya kazi za ukombozi wa mwanamke na mtoto wa kike.
“Kwa niaba ya wawezeshaji wote na Mkurugenzi Mwenza wa (WFT-Trust) Rose Marandu, tunawashukuru sana kwa kuhudhulia mkutano huu, na milango yetu ipo wazi msisite kuwasiliana na sisi pale penye changamoto ya aina yoyote ile, ili tuone namna ya kuitafutia ufumbuzi na kusongambele katika utendaji kazi,”alisema Mango.
“Katika Mkutano huu mmejifunza mambo mengi, ambayo naimani mtakwenda kuyafanyia kazi katika utekelezaji wa miradi yenu na kuleta matokeo chanya,” aliongeza.
Nao baadhi ya washiriki wa mkutano huo, akiwamo Msafiri Mwajuma kutoka Shirika la usawa wa kinjisia Tanzania (SUKITA), akizungumza kwa niaba ya washiriki wenzake, alisema wamejifunza vitu vingi ambavyo vimewajenga kiutendaji kazi, na namna ya kuendelea kuandika maandiko vizuri ya kuomba miradi.
“Kupitia Mkutano huu tumejifunza mambo mengi, na maelekezo ambayo yametolewa tutakwenda kuyafanyia kazi ili kuboresha kazi zetu, na kuletea matokeo chanya kwenye utekelezaji wa miradi yetu ya ukombozi wa mwanamke na mtoto wa kike,”alisema Mwajuma.
Mkuu wa Program kutoka Mfuko wa wanawake Tanzania (WFT-Trust) Carol Mango akizungumza wakati wa kuhitimisha mkutano kazi wao na mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka Mikoa mbalimbali ambayo wameyapatia Ruzuku ya utekelezaji wa miradi utetezi wa wanawake na watoto.
Dk.Dinna Mbaga,akizungumza kwenye mkutano huo na kutoa Mada namna ya kuandika maandiko vizuri ya kuomba Ruzuku ya Miradi.
Msafiri Mwajuma kutoka Shirika la usawa wa kinjisia Tanzania (SUKITA) akitoa shukrani ya mkutano huo kwa niaba ya washiriki wenzake.
Awali Godluck Malilo kutoka Shirika la Tree Of Hope akichangia Mada kwenye Mkutano huo.
Charles Salu kutoka Shirika la Kinara For Youth Evolution akichangia Mada kwenye Mkutano huo.
Rehema Katabi kutoka Shirika la WEADO akichangia Mada kwenye Mkutano huo.
Irene Ishengoma kutoka Shirika la Global Peace Foundation Tanzania, akichangia Mada kwenye Mkutano huo.
Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Shinyanga (SPC) Estomine Henry akichangia Mada kwenye Mkutano huo.
Zacharia Ntiganzi kutoka Klabu ya Waandishi wa Habari Manyara akichangia Mada kwenye Mkutano huo.
George Nyanda kutoka Shirika la GCI akichangia Mada kwenye Mkutano huo.
Martha Jerome kutoka Shirika la WPC akichangia Mada kwenye Mkutano huo.
Washiriki wakiwa kwenye Mkutano.
Washiriki wakiendelea na Mkutano.
Washiriki wakiendelea na Mkutano.
Washiriki wakiendelea na Mkutano.
Washiriki wakiendelea na Mkutano.
Washiriki wakiendelea na Mkutano.
Washiriki wakiendelea na Mkutano.
Washiriki wakiendelea na Mkutano.
Washiriki wakiendelea na Mkutano.
Washiriki wakiendelea na Mkutano.
Washiriki wakiendelea na Mkutano.
Washiriki wakiendelea na Mkutano.
Washiriki wakiendelea na Mkutano.
Washiriki wakiendelea na Mkutano.
Washiriki wakiendelea na Mkutano.
Washiriki wakiendelea na Mkutano.
Washiriki wakiendelea na Mkutano.
Washiriki wakiwa kwenye makundi wakijifunza namna ya kuandika maombi ya Ruzuku ya Miradi.
Washiriki wakiwa kwenye makundi wakijifunza namna ya usimamizi wa miradi.
Washiriki wakiwa kwenye makundi wakijifunza namna ya ujenzi wa nguvu ya pamoja TAPO.
Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya kuhitimisha mkutano huo wa siku mbili.
Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya kuhitimisha mkutano huo wa siku mbili.
Kwa mawasiliano zaidi kwa WFT Trust, Piga simu +255 753 912 130, tuma barua pepe kwa info@wftrust.or.tz au tembelea tovuti www.wft.or.tz.