Mgeni Rasmi Mkurugenzi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Julius Migeha, (wapili kutoka kulia) akimwakilisha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (TAMISEMI), anayeshughulikia elimu Maalum, akizindua mradi wa elimu Jumuishi kwa kukata utepe kitabu chenye andiko la mradi huo.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
MASHIRIKA matatu yasiyo ya kiserikali yameungana kwa pamoja kutekeleza Mradi wa Elimu Jumuishi, ambao utawajengea mazingira Rafiki wanafunzi wenye ulemavu kusoma na kutimiza ndoto zao, huku wakifichuliwa watoto wenye ulemavu waliofichwa ili wapate haki yao ya elimu.
Mashirika yaliyoungana kutekeleza Mradi huo wa Elimu Jumuishi ni Add International, Sense International na Leonard Cheshire ambao ndiyo wasimamizi wakuu wa mradi huo, ambao utatekelezwa katika Halmashauri Tatu, ambazo ni Manispaa ya Shinyanga, Halmashuri ya wilaya ya Shinyanga na Halmashauri ya Misungwi mkoani Mwanza.
Mradi huo umezinduliwa leo Marchi 21,2022 na Mkurugenzi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Julius Migeha anayeshughulikia elimu Maalum, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Karena Hoteli Mjini Shinyanga, na kudhuliwa na wadau wa Makundi Maalumu, na Maofisa elimu msingi na Mkoa kutoka Shinyanga na Mwanza.
Meneja mradi wa elimu hiyo Jumuishi Menance Mhombwe, akitoa maelezo ya utekelezaji wa mradi huo kabla ya kuzinduliwa , amesema utadumu ndani ya miaka mitatu kuanzia (2022 -2024) kwa gharama ya Sh.bilioni 1.9, ambao utafikia shule 47 za awali na msingi katika Halmashauri tatu za Manispaa ya Shinyanga, wilaya ya Shinyanga na Misungwi.
Alisema kazi ambazo watakuwa wakizifanya na mashirka hayo matatu, ni kuhamasisha jamii kutowaficha ndani watoto wenye ulemavu, pamoja na kupata Takwimu halisi ya watoto wenye nulemavu ambao hawasomi shule na kwenda kuwaandikisha kuanza masomo.
Alisema kazi nyingine ni kupima utambuzi wa watoto wenye ulemavu ili kujua kiwango chao cha ulemavu, pamoja na kuwaboreshea miundombinu Rafiki ya elimu zikiwamo Ngazi Mtelezo, Vyoo na Madawati maalumu.
Aidha, alisema mbali na uboreshaji wa miundombinu hiyo, pia katika shule hizo 47 watawafundisha walimu wote namna ya kufundisha wanafunzi wenye ulemavu katika shule hizo jumuishi, pamoja na kuwapenda, hali ambayo itapunguza upungufu wa walimu maalum kwenye shule hizo.
“Lengo la mradi huu ni kuwajengea mazingira Rafiki ya elimu wanafunzi wenye ulemavu na kuhakikisha hakuna mtoto mweye ulemavu ambaye ana umri wa kwenda shule asiende ili wapate haki sawa ya elimu kama watoto wengine na kutimiza ndoto zao,”alisema Mhombwe.
Naye Afisa Mwandamizi wa elimu Maalum kutoka Wizara ya elimu Sanyansi na Teknolojia Seleman Chamshama, aliyapongeza mashirika hayo kwa mradi huo, ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha elimu maalum, pamoja na kupunguza upungufu wa walimu maalum hasa pale watakapowajengea uwezo walimu wa kawaida kufundisha wanafunzi wenye uhitaji.
Alisema kwa Takwimu nchi inakabiliwa na walimu maalum kwa silimia 40, ambao waliopo ni asilimia 60, lakini Serikali imekuwa ikijitahidi kutatua tatizo hilo la upungufu wa walimu maalum, pamoja na usambazaji wa vifaa saidizi vya kujifunzia wanafunzi na kuchapisha vitabu vya Nukta Nundu.
Kwa upande wake Mgeni Rasmi Mkurugenzi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Julius Migeha, akimwakilisha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (TAMISEMI), anayeshughulikia elimu Maalum, aliyataka mashirika yao yanapokuwa yakitekeleza mradi huo washirikiane na maofisa wa Serikali ngazi zote.
Pia, aliyapongeza mashirika hayo kwa kazi nzuri ambayo wanaifanya kwa kushirikana na Serikali kutatua changamoto za elimu jumuishi, huku akitaja vipaumbele vinne vya Serikali katika uboreshaji wa elimu maalumu, kuwa ni miundombinu ya shule iwe Rafiki, na upatikanaji wa vifaa saidizi vya kusoma.
Alibainisha vipaumbele vingine ni kuwepo na walimu maalum wa kutosha, na ubainishaji wa watoto wenye ulemavu ambao hawasomi na kuwapeleka shule, huku akieleza kuwa mwaka 2018 Serikali ilifanya hivyo na kubaini watoto zaidi ya 16,000 na mwaka jana ilibaini watoto zaidi ya 28,000 ambao hawasomi na kuwapeleka shule.
Aidha mradi huo wa elimu jumuishi unafadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Ofisi ya mambo ya nje Jumuiya ya Madola na maendeleo, ambao utadumu ndani ya miaka mitatu kwa gharama ya Sh.bilioni 1.9.

Afisa Mwandamizi wa elimu Maalum kutoka Wizara ya elimu Sanyansi na Teknolojia Seleman Chamshama, akizungumza kwenye uzinduzi wa Mradi wa Elimu Jumuishi.
Afisa Mwandamizi mratibu wa masuala ya elimu Jumuishi kutoka (TAMISEMI) Peter Ndomondo, akizungumza kwenye uzinduzi wa Mradi wa Elimu Jumuishi.
Afisa elimu Mkoa wa Shinyanga Dafroza Ndalichako, akizungumza kwenye uzinduzi wa Mradi huo wa Elimu Jumuishi.
Afisa elimu Mkoa wa Shinyanga Mwanza Jovita Mombeki, akizungumza kwenye uzinduzi wa Mradi huo wa Elimu Jumuishi.
Meneja Mradi wa elimu Jumuishi Menance Mhombwe, akielezea mradi huo namna utkavyofanya kazi katika Halmashauri Tatu ,Manispaa ya Shinyanga, Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Misungwi.
Mkurugenzi wa Shirika la Sense International Naomi Lugoe akielezea namna wakatavyotekeleza mradi huo wa Elimu Jumuishi.
Mkurugenzi wa Shirika la ADD International Rose Tesha, akielezea namna watakavyokuwa wakitekeleza mradi huo wa Elimu Jumuishi.
Maofisa elimu wakiwa kwenye uzinduzi wa mradi huo wa Elimu Jumuishi.
Uzinduzi wa Mradi wa Elimu Jumuishi ukiendelea kwa kusikiliza maelezo ya utekelezaji wa mradi huo.
Uzinduzi wa Mradi wa Elimu Jumuishi ukiendelea kwa kusikiliza maelezo ya utekelezaji wa mradi huo.
Uzinduzi wa Mradi wa Elimu Jumuishi ukiendelea kwa kusikiliza maelezo ya utekelezaji wa mradi huo.
Uzinduzi wa Mradi wa Elimu Jumuishi ukiendelea kwa kusikiliza maelezo ya utekelezaji wa mradi huo.
Uzinduzi wa Mradi wa Elimu Jumuishi ukiendelea kwa kusikiliza maelezo ya utekelezaji wa mradi huo.
Uzinduzi wa Mradi wa Elimu Jumuishi ukiendelea kwa kusikiliza maelezo ya utekelezaji wa mradi huo.
Mgeni Rasmi Mkurugenzi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Julius Migeha, (wapili kutoka kulia) akimwakilisha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (TAMISEMI), anayeshughulikia elimu Maalum, akizindua mradi wa elimu Jumuishi kwa kukata utepe kitabu chenye andiko la mradi huo.
Mgeni Rasmi akipiga picha ya pamoja mara baada ya kumaliza uzinduzi wa Mradi wa Elimu Jumuishi.
Mgeni Rasmi akiendelea kupiga picha ya pamoja mara baada ya kumaliza uzinduzi wa Mradi wa Elimu Jumuishi.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464