Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dk. Festo Dugange,akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika wilayani Kahama.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dk. Festo Dugange, ameshiriki maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga, huku akitoa maagizo mbalimbali kwa ajili ya kuwainua wanawake kiuchumi.
Dugange akizungumza wakati akitoa hotuba kwenye maadhimisho hayo ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga kwa niaba ya Waziri wa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa, amewapongeza wanawake wa Mkoa huo kwa kuchangamkia mikopo ya Halmashauri asilimia 4 na kufanya shughuli mbalimbali za kijikwamua kiuchumi.
Alisema Mikopo hiyo ya Halmashauri asilimia 10, ambapo 4 kwa vijana na wanawake, na mbili kwa watu wenye ulemavu, imekuwa ikitolewa na Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassani, kwa ajili ya kuinua makundi hayo kiuchumi, na kuonya ukiritimba juu ya utolewaji wa mikopo hiyo.
“Nimezunguka kwenye mabanda wa wajasiriamali katika maadhimisho haya ya siku wa wanawake duniani mkoani Shinyanga, ambayo yamefanyika hapa wilayani Kahama, na nimeona jinsi walivyotengeneza bidhaa zao kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi nimefurahi sana kwa juhudi zao,”alisema Dk. Dugange.
“Hivyo naagiza Wakurugenzi na Maofisa maendeleo ya jamii marufuku kuwepo na ukiritiba kwenye utoaji wa mikopo hii, bali itoeni kwa kufuata utaratibu ili kila mtu anufaike na kumkwamua kiuchumi,”aliongeza.
Aidha, alisema pia katika utolewaji wa mikopo hiyo waangalie namna ya kuviwesha vikundi vichache vya ujasiriamali kwa kuvipatie fedha nyingi ambayo wataanisha miradi yenye tija na kuwa kwamua kiuchumi, kuliko kuwa na vikundi vingi lakini vinapewa pesa kidogo ambayo haiwezi kukidhi mahitaji yao.
Pia alisema amefurahishwa na Mkoa huo wa Shinyanga kwa kuendelea kutoa fedha za mikopo asilimia 10 kwa ajili ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, ambapo katika mwaka wa fedha (2020-2021) umetoa kiasi cha fedha Sh.bilioni 1.6 kwa ajili ya kuwezesha makundi hayo.
Aliupongeza pia Mkoa huo wa Shinyanga kwa kuzindua kitabu cha mpango mkakati wa kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto, pamoja na jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi, mipango ambayo itaongeza chachu ya kumkomboa mwanamke kimaendeleo.
Katika hatua nyingine, aliwataka wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa ukimwi, ambapo Mkoa huo maambukizi yake yapo juu asilimia 5.9 ikilinganishwa na takwimu kitaifa asilimia 4.7, huku akiwa sisitiza pia kuendelea kujikinga na ugonjwa wa UVIKO-19 pamoja na kupata chanjo ili kupata kinga dhidi ya ugonjwa huo.
Naibu Waziri Dugange, aliwataka pia wananchi wa Mkoa huo wa Shinyanga, wajitokeze kwa wingi siku ya zoezi la kuhesabiwa Sensa na makazi ya watu, zoezi ambalo litafanyika Agost Mwaka huu, ili Serikali ipate idadi kamili ya watu wake na kuwa rahisi kupanga mipango yake na kutoa huduma stahiki kwa wananchi kulingana na idadi yao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa watoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum, Sebastian Kitiku aliwapongeza wanawake kote kwa kuendelea kujituma kufanya kazi, na kubainisha kuwa asilimia 80 ya wakulima ni wanawake, na asilimia 60 ndiyo wazalishaji wa chakula hapa nchini.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, alisema maadhimisho hayo yametoa fursa kwa wanawake kujenga mtandao wa kibiashara, ambapo wamekutana wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali na wamebadilishana uzoefu namna ya kufanya biashara na kujikwamua kiuchumi.
Alisema wao kama Mkoa wa Shinyanga, walianza maadhimisho hayo ya siku ya wanawake Marchi 5 kwa kufanya makongamano ya wanawake kwa kujadili mambo mbalimbali, na kubainisha kuwa makongamano hayo yatakuwa endelevu, pamoja na kuweka mazingira rafiki ya ufanyaji biashara.
Nao baadhi ya wanawake wajasiriamali kwa nyakati tofauti wameipongeza Serikali kwa kuwakutanisha na wenzao pamoja na taasisi za kifedha, ambapo wamepata elimu mbalimbali namna ya kupata mikopo ili kupanua wigo wa biashara zao na kuinuka kiuchumi.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dk. Festo Dugange,akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika wilayani Kahama.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dk. Festo Dugange,akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika wilayani Kahama.
Mkurugenzi wa watoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum, Sebastian Kitiku, akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika wilayani Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani humo yaliyofanyika wilayani Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani humo yaliyofanyika wilayani Kahama.
Katibu tawala Mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary, akizungumza kwenye siku ya maadhimisha hayo ya wanawake duniani.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya siku ya wanawake duniani.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Kishapu Joseph Mkude, akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya siku ya wanawake duniani.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga, akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya siku ya wanawake duniani.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mabala Mlolwa, akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika wilayani Kahama.
Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Shinyanga Christina Mzava akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika wilayani Kahama.
Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Shinyanga Santiel Kirumba akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika wilayani Kahama.
Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Shinyanga Ruth Mayenga akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika wilayani Kahama.
Afisa maendeleo ya jamii mkoani Shinyanga Tedson Ngwale, akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika wilayani Kahama.
Mzee wa kimilia Nshoma Haiwa,akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika wilayani Kahama. Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dk. Festo Dugange, akiwa kwenye mabanda wa wajasiriamali kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake mkoani Shinyanga, maadhimisho yaliyofanyika wilayani Kahama.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dk. Festo Dugange, akiendelea kutembelea mabanda ya wajasiriamali kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake mkoani Shinyanga, maadhimisho yaliyofanyika wilayani Kahama.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dk. Festo Dugange, akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, wakiwa sikiliza wajasiriamali walipotembelea mabanda ya wajasiriamali kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake mkoani Shinyanga, maadhimisho yaliyofanyika wilayani Kahama.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dk. Festo Dugange, akiwa kwenye banda la (TRA) kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika wilayani Kahama.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dk. Festo Dugange, akiwa kwenye banda la (TANESCO) kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika wilayani Kahama.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dk. Festo Dugange, akiwa kwenye banda la benki ya CRDB kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika wilayani Kahama.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dk. Festo Dugange, akiwa kwenye banda la benki ya TCB kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika wilayani Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kulia)akiwa na Katibu tawala wa Mkoa huo Zuwena Omary wakiteta jambo kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga, yaliyofanyika wilayani Kahama.
Viongozi wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika wilayani Kahama, watatu (katikati) ni Naibu Waziri wa TAMISEMI, Dk Festo Dugange.
Makatibu wa CCM wilaya wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga, yaliyofanyika wilayani Kahama.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kulia) akiwa kwenye maadhimisho hayo ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika wilayani Kahama.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye maadhimisho hayo ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika wilayani Kahama.
Wananchi wa mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye maadhimisho hayo ya siku ya wanawake duniani mkoani humo yaliyofanyika wilayani Kahama.

Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Dk. Festo Dugange, akigawa sare za shule kwa wanafunzi ambao wanaishi maisha magumu.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Dk. Festo Dugange, akitoa kadi za bima ya afya CHF kwa wanafunzi wenye Ualbino, ambapo jumla za kadi ambazo watapewa watoto hao ni 228
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Dk. Festo Dugange, akipokea Pis 200 za Taulo za kike ,kutoka katika Shirika la HQ,ambazo watagawiwa watoto wanaishi katika mazingira magumu
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Dk. Festo Dugange, akikabidhi mfano wa hundi ya Sh.milioni 50 katika kikundi cha ujasiriamali Ushetu.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Dk. Festo Dugange (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya Sh.milioni 277,500,000 katika kikundi cha ujasiriamali Kahama, kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Anderson Msumba.
Msanii Osca Nyerere akitoa burudani kwenye maadhimisho hayo ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga, yaliyofanyika wilayani Kahama.
Msaani Msagasumu,akitoa burudani kwenye maadhimisho hayo ya siku ya wanawake duniani mkoani Shinyanga, kulia akipewa sapoti na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Awali wananchi wakiingia na maandamano kwenye maadhimisho hayo ya siku ya wanawake mkoani Shinyanga yaliyofanyika wilayani Kahama.
Awali wananchi wakiingia na maandamano kwenye maadhimisho hayo ya siku ya wanawake duaniani mkoani Shinyanga yaliyofanyika wilayani Kahama, wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko mwenye kiremba chekundi kichwani.
Awali wananchi wakiingia na maandamano kwenye maadhimisho hayo ya siku ya wanawake mkoani Shinyanga yaliyofanyika wilayani Kahama.
Awali wananchi wakiingia na maandamano kwenye maadhimisho hayo ya siku ya wanawake mkoani Shinyanga yaliyofanyika wilayani Kahama.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464