Na Marco Maduhu, KAHAMA.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani, kwa kuonyesha umma kuwa wanawake wanauwezo mkubwa wa kiungozi, kwa namna alivyoliletea Taifa maendeleo makubwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja cha utawala wake.
Mjema amebainisha haya leo March 7,2022 kwenye maonesho ya ujasiriamali wilayani Kahama, katika wiki ya maadhimisho ya wanawake duniani, ambapo kimkoa wa Shinyanga yanafanyika wilayani Kahama na kilele chake ni kesho Marchi 8,2022.
Alisema Rais Samia ameonyesha kuwa wanawake wanauwezo mkubwa kiuongozi, na kuwataka wanawake wa mkoa wa Shinyanga wasiogope kujitokeza kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi, pamoja na kisiasa sababu wanauwezo mkubwa wa kuliongoza Taifa na kuwaletea maendeleo wananchi.
“Wanawake wenzagu wa Shinyanga naombeni sana tufanye shughuli za kiuchumi na kupata maendeleo, Rais wetu Samia ameshaonyesha njia kuwa wanawake tunauwezo mkubwa katika mambo mbalimbali ukiangalia mambo ambayo ameyafanya ni makubwa sana, hivyo tusimwangushe mwanamke mwezetu tuchape kazi,”alisema Mjema.
Aidha, alisema wao kama wasaidizi wake ngazi za mkoa, watahakikisha wanaendelea kuweka mazingira rafiki ya wananchi katika kufanya shughuli zao mbalimbali za kiuchumi, pamoja na kuendelea kutoa mikopo isiyo na riba kupitia Halmashauri asilimia 10, ambapo Nne kwa vijana na wanawake, na mbili kwa watu wenye ulemavu.
Katika hatua nyingine Mjema amewataka wananchi wa mkoa huo wa Shinyanga, wajitokeze kwa wingi kwenye zoezi la kuhesabiwa Sensa na Makazi, ambalo litafanyika Agosti mwaka huu, ili Serikali ipate idadi ya watu wake kamili na kuwa virahisi kuwatekelezea shughuli mbalimbali za maendeleo.
“Kauli mbiu ya siku ya wanawake duniani ya mwaka huu inasema “kizazi cha haki na usawa kwa maendeleo endelevu tujitokeze kuhesabiwa”, hivyo nawasihi wananchi mshiriki kikamilifu kwenye zoezi hili la Sensa, ambapo zitahesabiwa na nyumba zetu na kuwekewa anwani za makazi na mitaa,”alisema Mjema.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amewataka wanawake kuendelea kujiunga kwenye vikundi vya ujasiriamali na kuchangamkia mikopo ya Halmashauri, pamoja na mikopo ya kwenye Taasisi za kifedha, ili wapate mitaji na kufanya shughuli za kiuchumi na kuinuka kimaendeleo.
Nao baadhi ya wanawake wajasiriamali ambao walitembelewa kwenye Mabanda yao na Mkuu huyo wa Mkoa, kwa nyakati tofauti waliishukuru Serikali kwa kutoa mikopo hiyo ya Halmashauri, ambayo walisema imekuwa msaada mkubwa kwao kuinuka kiuchumi na kuendesha maisha yao.
Maadhimisho hayo ya siku ya wanawake duniani yanatarajia kuhitimishwa kesho Marchi 8 mwaka huu, yakiwa na kauli mbiu isemayo, kizazi cha haki na usawa kwa maendeleo endelevu tujitokeze kuhesabiwa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza kwenye Maonesho ya ujasiriamali wilayani Kahama, katika kuelekea kilele cha siku ya maadhimisho ya wanawake duniani kesho.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akizungumza kwenye Maonesho ya ujasiriamali wilayani Kahama, katika kuelekea kilele cha siku ya maadhimisho ya wanawake duniani kesho.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa Magreth Cosmas akizungumza kwenye maonesho hayo ya ujasiriamali wilayani Kahama, katika kuelekea kwenye kilele cha siku ya maadhimisho ya wanawake duniani kesho.
Mzee wa kimila wilayani Kahama akizungumza kwenye maonesho hayo,katika kuelekea kwenye kilele cha siku ya maadhimisho ya wanawake duniani kesho.
Mbunge wa Vitimaalum mkoa wa Shinyanga Ruth Mayenga akizungumza kwenye maonesho hayo, katika kuelekea kwenye kilele cha siku ya maadhimisho ya wanawake duniani kesho.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza kwenye maonesho hayo ya ujasiriamali wilayani Kahama, katika kuelekea kwenye kilele cha siku ya maadhimisho ya wanawake duniani kesho.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Zuwena Omary, akizungumza kwenye maonesho hayo ya ujasiriamali wilayani Kahama, katika kuelekea kwenye kilele cha siku ya maadhimisho ya wanawake duniani kesho.
Mwenyekiti wa jukwaa la uwezashaji wanawake kiuchumi mkoani Shinyanga Regina Malima, akizungumza kwenye maonesho hayo ya ujasiriamali wilayani Kahama, katika kuelekea kwenye kilele cha siku ya maadhimisho ya wanawake duniani kesho.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga, akizungumza kwenye maonesho hayo ya ujasiriamali wilayani Kahama, katika kuelekea kwenye kilele cha siku ya maadhimisho ya wanawake duniani kesho.
Mratibu wa dawati la uwezeshaji wananchi kiuchumi mkoani Shinyanga Dotto Maligisa, akizungumza kwenye maonesho hayo ya ujasiriamali wilayani Kahama, katika kuelekea kwenye kilele cha siku ya maadhimisho ya wanawake duniani kesho.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kushoto) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kwenye maonesho ya wajasiriamali wilayani Kahama, katika kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kesho.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akiangalia bidhaa mbalimbali za wajasiriamali kwenye maonesho hayo wilayani Kahama, katika kuelekea kwenye kilele cha siku ya maadhimisho ya wanawake duniani kesho.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kulia) akiwa na Mkuu wa Idara ya maendeleo ya jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Deus Mhoja Wakiangalia bidhaa mbalimbali za wajasiriamali kwenye maonesho hayo wilayani Kahama, katika kuelekea kwenye kilele cha siku ya maadhimisho ya wanawake duniani kesho.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiangalia bidhaa mbalimbali za wajasiriamali kwenye maonesho hayo wilayani Kahama, katika kuelekea kwenye kilele cha siku ya maadhimisho ya wanawake duniani kesho.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akijifunga kitenge cha wajasiriamali kwenye maonesho ya bidhaa mbalimbali za wajasiriamali wilayani Kahama, katika kuelekea kwenye kilele cha siku ya maadhimisho ya wanawake duniani kesho.
Mbunge wa Vitimaalum mkoani Shinyanga Ruth Mayenga, akiangalia bidhaa mbalimbali za wajasiriamali kwenye maonesho hayo wilayani Kahama, katika kuelekea kwenye kilele cha siku ya maadhimisho ya wanawake duniani kesho.
Kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga wakiangalia bidhaa mbalimbali za wajasiriamali kwenye maonesho hayo wilayani Kahama, katika kuelekea kwenye kilele cha siku ya maadhimisho ya wanawake duniani kesho.
Wananchi wakiangalia bidhaa mbalimbali za wajasiriamali kwenye maonesho wilayani Kahama.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akitembelea mabanda ya Taasisi za Serikali kusikiliza shughuli zao katika kuwahudumia wananchi, hapo akiwa kwenye banda la TANESCO.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akiwa kwenye banda la benki ya NBC.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akiwa kwenye banda la benki ya CRDB.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akiwa kwenye banda la benki ya TCB.
Baadhi ya wanawake wilayani Kahama, wakiwa kwenye maonesho hayo ya ujasiriamali katika kuelekea kwenye kilele cha siku ya maadhimisho ya wanawake duniani kesho.
Mwanamke Veronica Anthony akitoa burudani kwa kuendesha pikipiki akiwa amebeba ndoo ya maji kichwani.
Na Marco Maduhu, KAHAMA.