SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROL TANZANIA(TPDC) LIMEWAHASA WAKAZI WA MKOA WA SHINYANGA KUTUMIA FURSA YA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA.
Wadau kutoka mkoa wa Shinyanga walioweza kushiriki Mkutano wa kutambulisha mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kwa mkoa wa Shinyanga.
Mhandisi Mhina kiondo akiwasilisha mada kuhusu fursa sheria ya nishati na mafuta ya mwaka 2015 na uwepo wa kanzidata ya Ewura ya kukusanya taarifa za kamapuni ya wazawa ili kusaidia kupata fursa katika mradi.
Busegi Kulwa,Mkandarasi Mkuu wa kampuni ya East Africa Logistic services company limited(E.A.L.S) akizungumzia namna ya kuweza kushirikisha wakandarasi wazawa katika ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kwa mkoa Shinyanga.
Baadhi ya wadau kutoka mkoa wa Shinyanga walioweza kushiriki mkutano wa kutambulisha ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kwa mkoa wa Shinyanga.
Na mwandishi wetu.
Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) limewahasa wakazi wa mkoa wa Shinyanga kuweza kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi katika mradi wa ujenzi wa boma la mafuta ghafi (EAST AFRICA CRUDE OIL PIPELINE) litakalo pita katika wilaya ya Kahama.
Hayo yameelezwa leo Februari 9,2022 na Beatrice Peter, Afisa Habari wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika Mkutano wa kutambulisha wakandarasi watakaohusika na ujenzi wa boma la mafuta ghafi katika mkoa wa Shinyanga katika wilaya ya Kahama. Mkutano huu umehudhuriwa na wakandarasi, taasisi za usalama na ulinzi, taasisi za kifedha na wafanya biashara kutoka mansipaa ya kahama na Shinyanga.
Beatrice alisema kuwa lengo kuu la Mkutano huu ni kuwatambulisha wakandarasi wakubwa watakahusika na ujenzi wa mradi huu na kuwaonesha fursa ambazo wakazi wa mkoa wa Shinyanga wanaweza kunufaika nazo kwa kujishughulisha na utoaji wa huduma na bidhaa mbalimbali katika kipindi cha utekelezaji wa mradi.
Beatrice aliongeza kuwa, TPDC ni msimamizi mkuu wa ardhi kwa niaba ya serikali katika mradi huu na wanafanya mikutano kila mkoa inayopitiwa na mradi huu ili kuwapa fursa wananchi kuweza kutambua maeneo yao ya kuweza kushiriki kwa kutoa huduma na bidhaa ili kupata fursa za kiuchumi.
“Tumefanya mkutano huu ili kuwatambulisha namna ya kuweza kushiriki kwa kutumia fursa zilizopo kwa mradi huu hasa kwa wazawa wa mkoa wa Shinyanga kwa kuweza kunufaika na mradi”
“Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania linamiliki hisa asilimia 15% katika kampuni ya EACOP (EAST AFRICA CRUDE OIL PIPELINE COMPANY) na jukumu letu kuu ni usimamizi wa masuala yote ya ardhi ya Tanzania katika utekelezaji wa mradi huu, mradi unapitia mikoa nane ya Tanzania ikiwa ni Kagera, Tabora Geita, Shinyanga, Singida, Manyara na Tanga, Hivyo tunawakilisha serikali katika maamuzi yote juu ya ardhi ya Tanzania”
Mradi huo unatarajia kutoa fursa za mbalimbali ikiwa ni huduma ya ulinzi,chakula,mahita ya vifaa vya ofisi,shughuli za uhandisi,uzoaji taka,usafiri ,usambazaji vifaa vya ujenzi,huduma za fedha,mawasiliano ya simu,usambazaji wa mafuta,upimaji wa ardhi nk.Ambapo watanzania wengi watapata fursa ya kushiri juu ya ujenzi wa mradi huo.
Kwa upande wake Eng, Mhina Kiondo wa EWURA alisema, jukumu la taasisi yake ni kusimamia sheria ya nishati na mafuta ya mwaka 2015 ambazo zimebainisha ushiriki wa wazawa wa ndani katika mradi. Pia alisema EWURA inayo kanzidata maalum ya kuweza kusaidia wakandarasi wakubwa kutoka nje kutumia wakandarasi wazawa kwa kujua taarifa zao katika kanzidata.
“EWURA ina mfumo maalum wa na taarifa za makapuni yote ya wazawa hapa chini ili kusaidia waweze kushiriki miradi mikubwa kwa kushirikiana na makapuni kutoka nje, Hadi sasa kanzidata ina imesajili makapuni 1295, mengi ya makapuni ni yale yanajihusisha na umeme, ujenzi na uzalishaji wa bidhaa katika mfumo wetu” Alisema Mhina.
Aidha naye Busegi Kulwa mwakilishi wa East Africa Logistic Service Company limited (E.A.L.S) kutoka kampuni ya ukandarasi inayohusika na mradi huo alisema ni fursa njema kwa wakazi wa mkoa wa Shinyanga kunufaika na mradi mkubwa kama huo.
“Tunafanya vikao kila mkoa na viongozi wa mkoa na watumishi wa serikali ili iwe rahisi kwa wao kuweza kuwafikisha ujumbe kwa wananchi wao ili waweze kupata fursa za ushiriki wa mradi huu: Alisema Busegi.
Kwa upande wake Juliana Stephen Mashaka Mkazi wa Kahama anayejishughulisha na biashara mbalimbali amenufaika na ushiriki wa kikao hicho kwa kuwa kimemsaidia kubadilisha taarifa za kuweza kumpa nafasi ya kushiriki katika mradi wa bomba la mafuta ghafi.
Neema Mwakasoge mwakilishi wa Baraza la Taifa la uwekezaji kiuchumi akizungumzia fursa katika mradi wa boma ma mafuta ghafi kwa mkoa wa Shinyanga.
Anod Max mwakilishi wa kampuni ya China petrolium pipe line akizungumzia uwepo wa fursa katika mradi wa bomba la mafuta ghafi kwa mkoa wa Shinyanga.
Baadhi ya wakandarasi kutoka makapuni ya nje wanashiriki katika ujenzi wa mradi wa bomba la mafutaghafi walioshiriki Mkutano wa utambulisho wa mradi katika mkoa wa Shinyanga.
TAZAMA PICHA ZA MATUKIO.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464