Wakati Tanzania ikiwa na hifadhi kubwa ya gesi asilia, bado imeendelea kupambana kupata nishati ya mafuta ya kuendeshea vyombo vya usafiri na viwandani
Tanzania inakadiriwa kuwa na mita trilioni 230 za ujazo za gesi asilia, ingawa zilizothibitishwa mpaka sasa ni futi trilioni 57.5, hivyo kuiweka kwenye ramani ya dunia ikishika nafasi ya 82.
Gesi hiyo tayari imeanza kuchimbwa katika visiwa vya Songosongo wilayani Kilwa, mkoani Pwani na eneo la Msimbati mkoani Mtwara, ikitumika kuzalisha umeme na kuendesha mitambo ya baadhi ya viwanda nchini.
Pamoja na wingi wa hazina ya gesi hii muhimu, kwa kiasi kikubwa Tanzania bado inategemea mafuta kuendesha mitambo ya viwanda vyake pamoja na magari ya mizigo na abiria na pia baadhi ya majenereta ya kuzalisha umeme unaosambazwa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

SOMA HAPA ZAIDI; CHANZO MWANANCHI.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464